VIONGOZI WA KIROHO TUSAIDIE KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA MATUMIZI YA BANGI - RC TABORA

Na Tiganya Vincent, RS-Tabora
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imetoa wito kwa viongozi wa dini mbalimbali mkoani hapa kutumia nafasi zao katika kusaidia mapambano dhidi ya kilimo na matumizi dawa za kulevya aina ya bangi katika jamii. Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji, Wakuu wa Idara na viongozi wa dini mkoani hapa.
Alisema kuwa vitendo vingine vya uhalifu katika jamii vinasababishwa na matumizi ya dawa za kulevya kama vile bangi ambazo zinawapelekea baadhi ya vijana kuchukua maamuzi mwngine ya kujichukulia sheria mikononi. Mwanri alisema kuwa pamoja na kuwa Serikali ya Mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imekuwa ikiendesha zoezi la kufyeka mashamba ya bangi katika mapori mbalimbali bado viongozi wa kiroho wanayo nafasi ya kuwaelimisha Waumini wao kuepuka matumizi na kilimo cha zao hilo haramu ili kuhakikisha vijana wanakuwa katika maadili mazuri na sio yale ya kuelekezwa na bangi.
Alisema kuwa matumzi ya bangi yamesababisha baadhi ya vijana kukosa hata heshima hata kuwa tayari kupambana na wazee au watu wanaowazidi umri bila kuzingatia kuwa kufanya hivi ni kinyume na utamaduni mwa Mtanzania ambao unawataka vijana kuwa heshimu watu wazima. Mwanri aliongeza kuwa vitendo vya matumizi ya bangi viachwa vikaendelea na hatimaye vikajipenyeza hadi mashuleni upo uwezekano wa kuharibu na wanafunzi na kusababisha vurugu.
“Tunawaomba sana viongozi wetu wa kiroho mtusaidie kuhusu suala la bangi…utamkuta kijana ameshavuta na kuanza kusema bangi ni bangue …bangi nipe nguvu nikapigane na fulani…jambo linaonyesha kuwa bangi umsababisha kijana kupenda kutafura shari” alisisitiza Mkuu huyo Mkoa.
Akitoa mada kuhusu hali ya ulinzi na usalama kwa kipindi cha Januari hadi Septemba mwaka huu , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa alisema kuwa katika kipindi hicho kumekuwepo na matukio 167 ya watu kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi.
Alisema kuwa jeshi la Polisi mwaka huu limefanikiwa kukamata dawa nyingi za kulevya ikiwemo bangi kutokana na misako kuongezeka na kufanikiwa kuwakata watuhumiwa na kugundua maeneo ambao wamekuwa wakilimia bangi katika mapori mbalimbali. Aidha Kamando hiyo wa Mkuu wa Tabora alitoa wito kwa viongozi wa kiroho kusaidia kutoa elimu juu ya kuepuka imani ya kishirikina ambazo ndizo zimekuwa zikisababisha mauaji wa wazee na walemavu.
Kwa upande wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Askofu Mkuu Mihayo Tabora (AMUCTA) Padre Dkt. Juvenalis Asantemungu alisema anakusudia kutunga kitabu kitakachohusu maadili kwa ajili ya kuelimisha jamii ya wakazi wa Tabora na maeneo mengine ili kuzingatia maadili na kuepukana na vitendo vya kuwachoma wazee kwa imani za kishirikina. Alisema kuwa mtu anayezingatia maadili hawezi kutenda uovu huo wa kukatisha maisha ya wazee kwa sababu ya kuona kuwa wamekuwa na macho mekundu kutokana na mazingira wanayoishi.
Mkutano huo wa siku tatu ambao mada mbalimbali zinajadiliwa na ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora umewahusisha Wakuu wa Wilaya zote, Wakurugenzi Wote , Wakuu wa Idara zote , Taasisi za Umma zote na viongozi wa dini kwa lengo la kumbushana majukumu ya kila mmoja ili kuboresha huduma kwa wananchi.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Vijimambo

VIONGOZI WA DINI WAJITOSA MAPAMBANO DHIDI YA UJANGILI

WAZIRI WA Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akizungumza katika mkutano wake na viongozi wa dini mbalimbali uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree mjini Dar es Salaam, leo. Katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi wa juu wa dini mbalimbali masuala mbalimbali kuhusiana na madhara ya ujangili wa wanyama kama tembo na faru yalijadiliwa. Viongozi wa dini mbalimbali wakimsikiliza Nyalandu Waziri Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini mbalimbali baada ya mkutano huo....

 

4 years ago

Michuzi

VIONGOZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WATAKIWA KUTOA KIPAUMBELE MAPAMBANO DHIDI YA MAABUKIZI MAPYA YA VVU.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na wajumbe wa kikao cha majumuisho ya ziara ya siku nne ya viongozi  na watendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam. Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Dkt. Fatma Mrisho akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano wa majumuisho ya hali ya maambukizi mapya ya VVU katika jiji la Dar es salaam mara baada ya kukamilisha ziara...

 

3 years ago

Michuzi

IPTL/PAP ya wekeza katika mapambano dhidi ya Malaria

Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ambayo ni kampuni tanzu ya kampuni ya Pan Africa Power Solutions (T) Limited imetoa msaada wa vyandarua 700 vyenye viwatilifu kwa vituo vya afya vilivyopo kwenye kata za Wazo, Kunduchi na Kawe kwenye wilaya ya Kinondoni katika kuadhimisha ya siku ya Malaria duniani. Akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa IPTL na PAP, Katibu na mshauri mkuu wa sheria wa kampuni hizo, Bw. Joseph Makandege alisema: “IPTL inakubaliana kabisa na...

 

3 years ago

Dewji Blog

IPTL/PAP yawekeza katika mapambano dhidi ya Malaria

11

Kina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ni sehemu ya walengwa wakuu wa msaada wa vyandarua vyenye viwatilifu ulipotolewa na makampuni ya IPTL na PAP. Hapa kina mama wenye watoto wadogo wakiwa kwenye foleni ya kupokea msaada kata ya Wazo.

1

Kina baba hawakuwa nyuma katika kuunga mkono jitihada za kupambana na Malaria kwa kuungana na kina mama kupokea msaada wa vyandarua vyenye viwatilifu uliotolewa na Kampuni za IPTL/PAP katika kata za Wazo na Kundunchi.

6

Mama huyu...

 

1 year ago

VOASwahili

Hollande ayashukuru majeshi ya Ufaransa katika mapambano dhidi ya ugaidi

Wanajeshi 500 wa Ufaransa wanasadikiwa wanashiriki kampeni ya kuwaondoa wapiganaji wa Islamic State kutoka Mosul ngome yao kuu nchini Iraq.

 

9 months ago

Michuzi

SERIKALI YA USWISI YA UNGANA NA TANZANIA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA


Na Sixmund J. Begashe 
Serikali ya Uswisi imeamua kuinga mkoni Serikali ya Jamhuuri ya Muungano wa Tanzania katika mapambano dhidi ya Rushwa kwa kuziwezesha program tano kiasi cha Dola za kimarekani 100,000 ambazo ni takribani Shilingi milioni 220/= ili ziweze kutoa elimu kwa njia za burudani ya mapambano dhidi rushwa nchini.
Akizungumza kabla ya kusaini mikataba ya program hizo, Balozi wa Uswisi hapa nchini Mh ARTHUR MATTLI amesema kuwa Tanzania kwa sasa inafanya vizuri zaidi katika ...

 

9 months ago

Channelten

Mapambano dhidi ya uvuvi haramu, Mkoa wa Mara watakiwa kuendeleza mapambano

uvuvi-haramu

Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan ameziagiza kamati ya ulinzi na usalama mkoani Mara kuhakikisha inasimama kuendeleza mapambano dhidi ya uvuvi haramu kwa kuhakikisha wanaimarisha doria ikiwemo kukomesha matukio mbalimbali ya uhalifu yanayofanyika katika ziwa Victoria ili kulinda rasilimali samaki iliyopo ziwani humo.

Amesama hayo alipokua akizungumza katika mkutano wake uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mkendo vilivyopo manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Makamu wa Rais ameitaka...

 

2 years ago

Dewji Blog

Wanahabari watakiwa kuunganisha nguvu zao katika mapambano dhidi ya majangili nchini

MKURUNGENZI  wa Shirika lisilo la Kiserikali la Rafiki Wildlife Foundation, Mchungaji Clement Matwinga, amewahimiza waandishi wa habari nchini kuunganisha nguvu zao na wadau wengine, ili kuharakisha kutokomeza matukio ya ujangili yanayotishia kutoweka kwa wanyamapori.

Mchungaji Matwinga ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanyamapori duniani, iliyofanyika kwenye uwanja wa Namfua mjini hapa.

Alisema rasilimali ya wanyamapori ni mali ya Watanzania wote...

 

2 years ago

Michuzi

SERIKALI KUWEKA UTASHI WA KISIASA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UTAPIAMLO- MAKAM WA RAIS.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.SERIKALI imesema kuwa itaweka utashi wa kisiasa katika kupambana dhidi ya utapiamlo kwa kuongeza elimu hususani katika maeneo ya vijijini.
Hayo ameyasema leo Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Dunia iliyoandaliwa na Jukwa la Lishe Nchini (PANITA) , amesema kuwa suala la lishe likiwekewa utashi wa kisiasa litaweza kufanikiwa kutokana na jitihada ambazo zimeanza kuonekana kwa wadau.
Amesema serikali inatambua kuwa mojawapo ya...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani