Wadau wa habari wakiongozwa na MCT leo wamefungua kesi ya kupinga sheria ya huduma za vyombo vya habari

screen-shot-2017-01-11-at-4-01-00-pm

Wadau wa habari wakiongozwa na Baraza la habari Tanzania MCT leo wamefungua kesi ya kupinga sheria ya huduma za vyombo vya habari namba 12 ya mwaka 2016 katika mahakama ya Afrika Mashariki EACJ jijini Dar es salaam.

Katibu mtendaji baraza la habari Tanzania MCT Kajubi Mukajanga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kesi hiyo mahakamani hapo amedai kuwa sheria hiyo iliyopitishwa na bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania novemba 5 mwaka jana ina baadhi ya vifungu ambavyo vinakandamiza uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza.

Akielezea sababu ambazo zimepelekea wao kufungua kesi katika mahakama ya Afrika ya Mashariki mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu Fulgence Massawe anafafanua.

Wadau wengine wa habari na watetezi wa haki za binadamu nchini wameungana na Baraza la habari Tanzania katika kufungua kesi hiyo ya kupinga sheria ya huduma ya vyombo vya habari ya mwaka 2016.

Hivi sasa wadau mbalimbali wa habari nchini wamemaliza kupeleka mapendekezo ya kanuni za sheria hiyo ya huduma za vyombo vya habari ambazo ziko chini ya mamlaka ya waziri wa habari.

Channelten

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Dewji Blog

MCT, LHRC, THRDC watinga mahakama ya EACJ kupinga Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari

Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Haki za Binadamu Tanzania ( THRDC) leo Jumatano ya Januari 11, 2017 wamefungua kesi ya kuipinga Sheria Mpya ya Huduma za Vyombo vya Habari namba 12 ya mwaka 2016 katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ).

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufunguliwa kesi hiyo, Katibu Mtendaji MCT, Kajubi Mukajanga amesema washirika waliofungua kesi hiyo wanataka baadhi ya vifungu vya sheria vinavyokandamiza...

 

2 years ago

Mwananchi

Mtandao kupinga kortini sheria ya vyombo vya habari

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), unatarajia kufungua kesi kupinga Sheria ya vyombo vya habari baada ya kubaini kuwa ina mapungufu.

 

4 years ago

Michuzi

Mkutano wa mashauriano kati ya Baraza la habari Tanzania(MCT) na Wahariri pamoja na watendaji wakuu wa Vyombo vya habari

Mkutano wa mashauriano kati ya Baraza la habari Tanzania(MCT) na Wahariri pamoja na watendaji wakuu wa Vyombo vya habari wafanyika katika Hotel ya Aishi Protea iliyoko Machame wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro Mtoa mada akiongea wakati wa mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe Novatus Makunga akiongea wakati akifungua katika mkutano huo Picha za pamoja ya mgeni rasmi na washiriki baada ya ufunguzi wa mkutano wa mashauriano kati ya Baraza la habari Tanzania(MCT) na Wahariri pamoja na...

 

3 years ago

Dewji Blog

Wamiliki wa vyombo vya Habari nchini MOAT wapinga mswada wa sheria ya Vyombo vya Habari

Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mswada wa sheria ya vyombo vya habari ambao ulitaka kuwasilishwa bungeni kwa dharula. Kulia ni Mwanasheria, Godfrey Mpandikizi.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Comminication, Samuel Nyalla (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Saed Kubenea kutoka Mwanahalisi Publishers na Mwanasheria, Godfrey...

 

1 year ago

Mwananchi

‘Muswada wa Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari unajadilika’

Msemaji wa Serikali Hassan Abbas amesema hoja ya wadau kuhusu madai ya kuongezwa muda ili kujadili na kuboresha Muswada wa Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2016, inajadilika.

 

1 month ago

RFI

Tanzania: Sheria ya Huduma ya vyombo vya Habari yapingwa Mahakamani

Wanahabari na wanaharakati nchini Tanzania wamekwenda Mahakamani kupinga Sheria ya Huduma ya vyombo vya Habari  kwa kile wanachosema, itatishia uhuru wa wanahabari nchini humo.

 

1 year ago

Ippmedia

Serikali kushirikiana na wadau kumaliza sheria zilizopitwa na wakati za vyombo vya habari.

Serikali imesema iko tayari kushirikiana na wadau katika sekta ya habari kubadilisha baadhi ya sheria na kanuni zinazoongoza tasnia ya habari ambazo zinaonekana kubana kukandamiza tasnia hiyo kwa kuendana na mabadiliko ya wakati na teknolojia.

Day n Time: Jumanne Saa 2:00 UsikuStation: ITV

 

1 year ago

Channelten

Sheria ya Huduma ya vyombo vya Habari Serikali imetangaza kuanza kutumika

Serikali imetangaza kuanza kutumika kwa sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016, baada ya kukamilika kwa kanuni zake za mwaka 2017, ambapo kuanzia sasa sifa ya chini ya kuwa mwandishi wa habari itakuwa ni Diploma ya Uandishi wa habari.

Akitangaza uamuzi huo wa serikali mbele ya waandishi wa habari mjini Dodoma, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Nape Nnauye amefafanua kuwa kwa wale waandishi wasio na sifa, serikali imetoa kipindi cha mpito cha miaka mitano, ili waweze...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani