WAHAMIAJI HARAMU 236 WAKAMATWA TANGA

Wahamiaji haramu 236 wamekamatwa mkoani Tanga kwa kuingia nchini bila kibali katika maeneo mbalimbali kwa kipindi cha Januari hadi Mei 16 mwaka huu.

Kaimu Ofisa Uhamiaji, Mkoa wa Tanga Salum Farahani amesema hayo leo Mei 16, wakati akizungumza na Mtanzania Digital na kuongeza kuwa wahamiaji hao wamekuwa wakiingia mkoani hapa kama njia kuelekea nchini Afrika Kusini.

“Wahamiaji hao walikamatwa kwa kipindi hicho kwa miezi tofauti tofauti ambapo 49 walikamatwa Januari, 77 walikamatwa Februari, 18...

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Zanzibar 24

Wahamiaji haramu 55 wakamatwa Tanga

Zaidi  ya wahamiaji 50 raia kutoka nchini Ethiopia wamekamatwa eneo la Duga wilayani Mkinga mkoani Tanga kwa kosa la kiungia nchini kinyume cha sheria. Wahamiaji  hao wamekamatwa ndani ya kipindi cha mwezi Desemba mwaka huu kufuatia operesheni zilizokuwa zikiendeshwa na Idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha wanadhibiti wimbi la uingiaji wa wageni. Akithibitisha kukamatwa kwa Wahamiaji hao Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Tanga DCI, Crispian Ngonyani hapo jana...

 

2 years ago

Michuzi

WAKALA WA WAHAMIAJI NA WAHAMIAJI HARAMU 72 WAKAMATWA PWANI.

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani.JESHI la Polisi Mkoani Pwani, linamshikilia mfanyabiashara, Rajabu Hitaji (30) mkazi wa Vigwaza, Bagamoyo anaedaiwa kuwasafirisha wahamiaji haramu 72 raia kutoka nchini Ethiopia.
Aidha jeshi hilo linawashikilia pia wahamiaji haramu hao kwa kosa la kuingia nchini bila kibali .
Akitolea ufafanuzi juu ya tukio hilo ,kamanda wa Polisi mkoani Pwani(ACP) Jonathan Shanna, alisema uchunguzi unaendelea na watafikishwa ofisi za uhamiaji kwa hatua nyingine stahiki. Alieleza...

 

5 years ago

Tanzania Daima

Wahamiaji haramu 21 wakamatwa

IDARA ya Uhamiaji mkoani hapa, imewakamata wahamiaji haramu 21 kutoka nchi ya Ethiopia walioingia nchini kwa kutumia roli la kubebea saruji katika eneo Mashujaa mjini Makambako. Naibu Kamishna wa Idara...

 

3 years ago

Habarileo

Wahamiaji haramu 59 wakamatwa

IDARA ya Uhamiaji mkoani Pwani imewakamata wahamiaji haramu 59 kutoka nchini Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini bila ya kibali, wakiwa na lengo la kuelekea Kusini mwa Tanzania ili waende Afrika ya Kusini.

 

5 years ago

Mwananchi

Wahamiaji haramu 57 wakamatwa K’njaro

Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro inawashikilia wahamiaji haramu 57 raia wa Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria.

 

5 years ago

Tanzania Daima

Wahamiaji haramu 69 wakamatwa Kilimanjaro

IDARA ya Uhamiaji mkoani Kilimanjaro inawashikilia raia 69 wa Ethiopia wanaodaiwa kuingia nchini kwa njia za panya katika wilaya za Mwanga na Moshi Vijijini. Akizungumza na TanzaniaDima jana, Ofisa Uhamijaji...

 

3 years ago

Channelten

Wahamiaji haramu 18 wakamatwa Mtwara

Screen Shot 2016-07-26 at 5.07.09 PM

Idara ya Uhamiaji Mkoani Mtwara imewakamata wahamiaji haramu kumi na nane raia wa Ethiopia ambao walikuwa wakivuka mpaka wa kilambo kuelekea Msumbiji.

Wahamiaji hao ambao wamekamatwa wakiwa wanatembea kwa miguu watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili.

Kamshina msaidizi wa idara ya uhamiaji na afisa uhamiaji mkoa wa Mtwara Rose Mhagama amesema wahamiaji hao 18 ambao wametambulika kuwa ni raia wa Ethiopia walikuwa wanajaribu kuvuka mpaka wa Tanzania na Msumbiji wa kijiji cha...

 

2 years ago

Habarileo

Wahamiaji haramu 8,100 wakamatwa

JUMLA ya wahamiaji haramu 8,100 wamekamatwa katika maeneo mbalimbali nchini katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Novemba, mwaka huu.

 

3 years ago

Michuzi

Wahamiaji haramu wakamatwa Tabata Segerea

Na Shamimu Nyaki-Maelezo
Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limewakamata wahamiaji haramu 105 raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria wakiwa wanasafirishwa kwenda nchi nyingine za Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaamu Kamishna Suleiman Kova amesema wahamiaji hao ambao wote ni wanaume wamekamatwa kutokana na ushirikiano wa wasamaria wema wanaoshi eneo hilo la Tabata Segerea.
Ameongeza...

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani