Wakazi wa jiji la Dsm wametakiwa kujitokeza kuanzia Nov.20 katika Upimaji Afya kwenye meli kubwa ya Jeshi la majini la China

MAKONDA

Wakazi wa jiji la Dsm wametakiwa kujitokeza kuanzia Nov.20 mwaka huu katika Upimaji Afya ,kupatiwa matibabu ya Upasuaji mdogo na Mkubwa Bure utakaofanyika katika meli kubwa ya Jeshi la majini la China ambayo itakuwa na madaktari bingwa pamoja na wahudumu zaidi ya 385.

Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari pamoja na makamanda wa jeshi la Majini la China ambao tayari wamewasili amesema,kuwasili kwa meli hiyo kutokana na balozi wa China aliyemaliza Muda wake Dr.LU ambae alijionea mafuriko ya wananchi katika Upimaji afya katika Viwanja vya Mnazi mmoja miezi mitatu iliyopita na Kuahidi kuleta madaktari kuunga Mkono jitihada za Bw,Makonda.

Aidha makonda amewataka wananchi waliokuwa wakisubiri kufanyiwa Upasuaji katika hospitali za m/myamala,temeke na amana ambao wako katika foleni ya kusubiri kufika katika meli hiyo ili kufanyiwa upasuaji huku ikiwa na Vifaa vya kisasa vya Tiba.

Meja Chi Song Kutoka katika kikosi cha jeshi la majini katika meli hiyo ambayo ni kubwa kuliko meli zote zilizowahi kuingia hapa nchini amesema Matibabu hayo ya bure ni matokeo mazuri ya Ushirikiano katika ya Tanzania na China pamoja na waasisi wa nchini hizo.

Share on: WhatsApp

The post Wakazi wa jiji la Dsm wametakiwa kujitokeza kuanzia Nov.20 katika Upimaji Afya kwenye meli kubwa ya Jeshi la majini la China appeared first on Channel Ten.

Channelten

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Channelten

Wakazi wa jiji la Dsm wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kampeni ya kupanda miti

screen-shot-2016-09-30-at-3-21-42-pm

Wakazi wa jiji la Dsm wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kampeni ya kupanda miti iliyobeba ujumbe wa MTI WANGU ambapo makamu wa rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza zoezi la upandaji miti katika jiji la Dsm.

Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini dsm amesema maandalizi ya zoezi hilo  yamekamilika ambapo pia makamu wa rais atashiriki zoezi hilo katika wilaya za jiji la dsm ambapo pia atakagua mioundombinu ya maji iliyowekwa kwa ajili ya...

 

1 year ago

Channelten

Wakazi wa jiji la Dsm wametakiwa kujitokeza kesho katika kampeni ya kumeza dawa za kinga

swallow-a-pill-step-16

Wakazi wa jiji la Dsm wametakiwa kujitokeza kesho katika kampeni ya kumeza dawa za kinga Dhidi ya magonjwa ya Matende,mabusha,Vikope,minyoo magonjwa ambayo yamekuwa yakisababisha madhara makubwa na Vifo katika jamii huku wenye mabusha wametakiwa kujitokeza kupata huduma ya Upasuaji bure katika vituo vya afya jijini dsm.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dsm ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Hassan Mgandilwa akizungumza na waratibu afya wa mkoa,wakuu wa wilaya pamoja na wakurugenzi wa manispaa za...

 

1 year ago

Channelten

Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda ametoa wito kwa wakazi wa Jiji la dsm kujitokeza katika zoezi la Bure la kupima afya

screen-shot-2016-09-22-at-3-25-02-pm

Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda ametoa wito kwa wakazi wa Jiji la dsm kujitokeza katika zoezi la Bure la kupima afya ambapo madaktari bingwa wa Moyo,Figo,saratani ya Matiti pamoja na Tezi dume kutoka hospitali kubwa jijini dsm watakuwepo kutoa huduma kuanzisha siku ya jumamosi na Jumapili tar-23 na 24 mwezi huu.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa na jopo la madaktari bingwa watakaotoa huduma hiyo,Makonda amesema Upimaji wa afya huo utaenda sambasamba na utoaji wa dawa na Ushauri wa...

 

6 months ago

Channelten

Zoezi la Upimaji Afya Bure, Mamia ya wakazi wa jiji la DSM wajitokeza

KUPIMA AFYA BURE

Zoezi la Upimaji afya bure kwa wakazi wa mkoa wa limeanza leo katika viwanja vya Mnazi mmoja ambapo mamia ya wananchi wamefurika katika viwanja hivyo kwa ajili ya kupata huduma hiyo iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa Paul Makonda.

Miongoni mwa magonjwa yanapimwa katika viwanja hivyo ni pamoja na Shinikizo la Damu,Kansa ya kizazi,magonjwa ya ini,Moyo ,tezi dume ,saratani ya matiti pamoja na magonjwa yasiyopewa kipaumbele.

Akizungumza na waandishi wa habari, mkuu wa dar es salaam Paul Makonda...

 

2 years ago

Channelten

Ikiwa Kesho ni maadhimisho ya Siku ya Maji Duniani wakazi wa jiji la Dsm wametakiwa hili

Screen Shot 2016-03-17 at 1.35.06 PM

Wakati Tanzania Kesho inaanza kuadhimisha Siku ya Maji Duniani wakazi wa jiji la Dsm wametakiwa kutoa taarifa za Siri za kuwafichua watu wanaoshirikiana na baadhi ya watumishi wa dawasco kujiunganishia maji kinyemela ambapo mwananchi atapata asilimia asilimia 20 fedha zinakazopatikana baada ya mhusika kulipa fidia na Faini dawasco.

Aidha Mwananchi atakayebainika kuhujumu miundombinu ya dawasco pamoja na kuiba maji pia vifaa vyake vitataifishwa mara moja huku hatua stahiki ya kufikishwa...

 

11 months ago

Channelten

Wakazi wa jiji la DSM waliowekewa mtandao wa mabomba ya mchina wametakiwa kwenda DAWASCO kuhakikiwa

dawasco+clip

Wakazi wa jiji la DSM wanaoishi katika maeneo ya Kimara, Tabata pamoja na Kibaha waliowekewa mtandao wa mabomba ya mchina wametakiwa kwenda katika vituo vya utoaji huduma za shirika la maji safi na taka DAWASCO kuhakikiwa ili kuunganishwa na mtandao wa maji kutoka mtambo wa Ruvu Juu unaotarajia kuanza kusambaza maji mwisho wa mwezi huu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Cyprian John Luhemeja akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika eneo la Boko mtaa wa Dovya amesema mradi huo...

 

1 year ago

Channelten

Zoezi la Upimaji Afya kwa wakazi wa Dsm wengi waliopima afya zao wamebainika kuwa na magonjwa haya

makonda-kupima10-768x512

Wakati zoezi la Upimaji Afya kwa wakazi wa jiji la Dsm lililoandaliwa na mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Makonda linakamilika leo wakazi wengi waliopima afya zao wamebainika kuwa na magonjwa ya shinikizo la damu,Matatizo ya moyo ,tezi dume kwa wanaume huku wanawake wakikabiliwa na matatizo ya saratani ya shingo ya kizazi.

Mganga mkuu wa mkoa wa Dsm Grace Maghembe akizungumza katika eneo hilo la Mnazi mmoja ambako zoezi hilo lilifanyika amesema hizo zilikuwa takwimu za awali kabla ya majumuisho...

 

5 months ago

Michuzi

CHINA KUONGEZA NGUVU ZOEZI LA UPIMAJI AFYA BURE DSM

Balozi wa Jamhuri ya watu wa China anaemaliza Muda wake nchini amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo zoezi la upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa Dar es Salaam limeingia siku ya Nne.
Mhe Balozi wa China akiwa ameambatana na Maofisa wa Ubalozi huo hapa nchini Ameshangazwa na UBUNIFU wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda wa kuwasaidia wananchi wengi wa Mkoa kwa WAKATI MMOJA hususani ni wenye vipato vya Chini ambao idadi...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani