WAKILI WA CHADEMA AMVAA IGP SIRRO KUZUIA MJADALA KUHUSU TUNDU LISSU

Wakili wa CHADEMA, John Malya amefunguka na kuzungumzia juu ya kauli ya IGP Sirro kuhusu kuzuia wanasiasa kuzungumzia sakata la Lissu na kusema IGP hana mamlaka hayo kuzuia wananchi kuzungumzia jambo lolote na kufanya hivyo ni kuvunja sheria.

John Malya amesema hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho yaliyopo Kinondoni na kusema kuwa Sirro anapaswa kukaa kimya sasa na kuendelea na uchunguzi wa sakata hilo ila hana mamlaka ya kuzuia wananchi wasitoe mawazo yao wala kuzungumzia jambo fulani.

"Kamanda Sirro alinukuliwa akiwa Mbeya anasema amepiga marufuku wanasiasa kujadili masuala yanayomuhusu Tundu Lissu na kujadili watu ambao labda wanasadikiwa au wanashukiwa kwamba wameshiriki jaribio la kumuuwa Lissu.Nimefikiri ni muhimu kumkumbusha IGP Sirro kuwa yeye ni kamanda wa Polisi na si kamanda wa raia hana mamlaka ya kutoa amri wananchi wajadili nini na nini wasijadili mamlaka hayo hana na nitatoa ufafanuzi.


"Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa haki na fursa ya wananchi kutoa maoni, kuzungumza mawazo yao na kubadilishana habari, ndiyo ibara ambayo inawapa wananchi na nyinyi waandishi wa habari uhuru wa kufanya kazi zenu katika nchi hii pamoja na sheria zingine lakini ibara ya 18 ndiyo msingi haswa wa kwanini wananchi wana uhuru wa kupashana habari na kuwa na uhuru wa mawazo" alisema Malya 

Malya alisema kuwa IGP naye anaongozwa na sheria na kanuni mbalimbali na kusema katika hizo sheria na kanuni ambazo zinamuongoza IGP katika kutenda kazi zake za kila siku hakuna sehemu ambapo anapewa mamlaka ya kuzuia wananchi kujadili jambo fulani na kusema anaweza kufanya hivyo kwa askari lakini si kwa wananchi.

"Kamanda Sirro anaongozwa na sheria kadhaa lakini kubwa anaongozwa na sheria ya jeshi la polisi na huduma saidizi, na msaafu anaotumia unaitwa 'Police General Order' (PGO). Kwenye jeshi la polisi hii ni sheria maarufu sana wao wenyewe wanaijua ndiyo inasema IGP anamuamuru nani na nani hawezi kumuamuru sasa huko anaweza kuwaamuru askari wake wasijadili au wasifanye kitu fulani, lakini kusema yeye amuru raia mamlaka hayo hana kwenye sheria wala kanuni" alisisitiza Malya

Aidha Malya anasema kuwa wananchi wanasubiri kusikia kauli ya IGP Sirro kuhusu upelelezi wa jambo hilo, au kusikia watu ambao wamekamatwa na kupelekwa mahakamani lakini si kuwazuia watu wasijadili shambulio alilolipata Tundu Lissu na kudai kuendelea kufanya hivyo ndiko kunapelekea hata wananchi pamoja na wao kuwa na mashaka na jeshi la polisi katika kufanya uchunguzi wa jambo hilo.

"Wakati huu ambapo wanasiasa, wapiga kura wanajadili juu ya hali ya Tundu Lissu yeye Sirro anapaswa kunyamaza, hapa yeye ndiyo anapaswa kunyamaza na siyo wanasiasa, yeye anyamaze afanye kazi ya upelelezi kitu cha pili tunachotaka kusikia amepeleka watu mahakamani, hivyo kufanya hicho anachokifanya anazidi kutufanya kukosa imani zaidi na jeshi la polisi" alisisitiza Malya

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

6 months ago

Zanzibar 24

Tundu Lissu amfungukia mkuu wa majeshi IGP Sirro.

Rais wa chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) na Mwanasheria Mkuu wa chama cha CHADEMA, Tundu Lissu amewata wakuu wa vyombo vya usalama nchini wawaelekeze watumishi wao kazi za kufanya na siyo kupoteza muda na rasilimali za nchi.

Lissu amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliyoitishwa na CHADEMA wenye lengo la kuzungumzia namna nchi inavyoenda kufilisika na ndipo alipomtaka Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Kamanda Modestus Francis Kipilimba na Mkuu wa...

 

5 months ago

Zanzibar 24

IGP Sirro upelelezi tukio la Tundu lissu umekwama

Kutokuwepo kwa dereva wa Lissu nchini, ambaye anapewa matibabu ya kisaikolojia Jijini Nairobi, kumesababisha kukwama kwa upelelelzi wa polisi kuhusiana na tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Mkuu wa Jeshi la polisi (IGP), Simon Sirro aliyasema hayo jana Jumatano, Oktoba 4 na kueleza kuwa Polisi wanamsubiria dereva wa Tundu Lissu ili aweze kuwasaidia katika kukamilisha uchunguzi kuhusiana na tukio hilo lililotokea Septemba 7, mwaka huu, wakati mbunge...

 

6 months ago

Zanzibar 24

IGP Sirro azungumzia tukio la kushambuliwa kwa Tundu Lissu

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha kuwatia mbaroni wahalifu waliohusika kumshambulia kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

IGP Sirro ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kudai usalama wa nchi upo vizuri na jeshi la polisi limeongeza nguvu ya upelelezi mjini Dodoma ili kuhakikisha linawapata watu ambao wamefanya uhalifu wa kumpiga risasi mbunge Tundu Lissu , huku akiwataka...

 

5 months ago

Malunde

IGP SIRRO: BADO TUNA SHIDA NA DEREVA WA TUNDU LISSU

 
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro amesema wanaendelea na upelelezi wa tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.IGP Sirro akizungumza leo Jumatano akiwa ziarani mkoani Mtwara amemtaka dereva wa Lissu kulisaidia jeshi hilo katika kukamilisha upelelezi.Lissu ambaye anapata matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya, alishambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7 nyumbani kwake Area D mjini Dodoma na watu...

 

5 months ago

Malunde

MSIGWA AMPINGA MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIA IGP SIRRO SAKATA LA TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI

Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA) Mchugaji Peter Msigwa amefunguka na kuonyesha kutoridhishwa na kauli ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro kusema Tundu Lissu hakuwahi kutoa taarifa juu ya watu wanaomfuatilia.

Mbunge Msigwa ambaye sasa yupo nchini Kenya kwenye matibabu ya Tundu Lissu ameonyesha kusikitiswa na taarifa hiyo ya IGP ambayo aliitoa Septemba 8, 2017 katika mkutano wa waandishi wa habari na kusema kiongozi huyo hakuwahi kutoa taarifa yoyote polisi juu ya gari...

 

1 week ago

MillardAyo

Agizo la Dr. Mwigulu kwa IGP Sirro kuhusu Kiongozi wa CHADEMA aliyeuwawa

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dr. Mwigulu Nchemba leo amefanya ziara mkoani Kagera kwa lengo la uzinduzi wa vitambulisho vya Taifa NIDA, ambapo amewasihi Watanzania kuhakikisha wanajiandikisha ili kuepukana na matatizo yanayoweza kuwakuta hapo baadae. Akiongea na wananchi Waziri Mwigulu amegusia suala la mauaji ya kada wa CHADEMA ambaye pia alikuwa Katibu wa […]

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani