WAKILI WA MWENYEKITI WA MTANDAO WA WANAFUNZI TANZANIA ABDUL NONDO AKWAMA POLISI

Mwanasheria Jebra Kambole na Wakili wa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo amefunguka na kusema kuwa mpaka sasa ameshindwa kuonana wala kuongea na mteja wake huyo ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi.

Wakili huyo amesema kuwa amejaribu kufika ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ili kujua hali ya mteja wake pamoja na kuweza kuongea naye lakini ameshindwa.

"Mpaka sasa sijafanikiwa kuzungumza wala kumuona kwa sababu mara ya mwisho wakati tunafanya mazunguzo na DCI ambaye ana mamlaka juu ya hilo kwa sababu Abdul Nondo alikuwa anashikiliwa ofisini kwake mpaka dakika ya mwisho, tulipokwenda ofisini kujaribu kumuona akasema sisi huyu mtu tunamshikilia kama kama mlalamikaji lakini siyo kama mtuhumiwa... kwa hiyo nyinyi kama Mawakili hamtakiwi kumhoji ila tukiona kwamba huyu mtu ni mtuhumiwa basi tutawaita muweze kuongea naye na kusikiliza maelezo yake.
"Sisi tulimweleza tunahitaji kumuona ili tuweze kujua afya yake ili tuweze kurejesha mrejesho kwa familia na Watanzania wengine kwa ujumla ambao wanahofia juu ya usalama wake akasema yupo salama" alisema Kombole

Aidha Wakili huyo aliendelea kudai kuwa mpaka sasa Abdul Nondo anashikiliwa kinyume na sheria kwa kuwa sheria ya makosa ya jinai haitoi ruhuusa kwa jeshi la polisi kumshikilia mlalamikaji.

"Anayeshikiliwa ni mtuhumiwa lakini mpaka siku ya leo hajaachiwa kama ni mtuhumiwa kweli kwa sababu mtu ambaye anakwenda kutoa taarifa polisi anaachiwa arudi nyumbani huwezi kushikiliwa huko polisi na kwa kuwa wao wanasema wanamshikilia ana haki ya kupata uwakilishi kwa sababu kwa mujibu wa sheria yetu ya mwenendo wa makosa ya jinai sura namba 20 ya sheria za Tanzania, kifungu cha tano kinasema kwa muda gani mtu atakuwa chini ya dola au polisi.
"Mtu ambaye amewekwa chini tu akiwa hana uhuru wa kwenda anakotaka huyo ina maana yupo chini ya ulinzi kwa hiyo kama upo chini ya ulinzi una haki ya kupata wakili kuweza kuongea naye na kujua nini kinaendelea na hatma yake na kupata fursa ya kuongea na ndugu zake na familia lakini fursa hiyo kwa Nondo haijapatikana kwani saizi ni muda mrefu ameshikiliwa na jeshi la polisi" alisema Kombole

Mbali na hilo Wakili huyo amesema kuwa mpaka sasa wao hawajui Abdul Nondo ameshikiliwa kwa sababu zipi na kusema kuwa kijana huyo ameshikiliwa kinyume na sheria, kinyume cha Katiba, kinyume cha haki za binadam na kinyume na utaratibu wetu kama taifa kiujumla.

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

2 weeks ago

Malunde

MWENYEKITI WA MTANDAO WA WANAFUNZI TANZANIA ABDUL NONDO APOTEA MAZINGIRA YA KUTATANISHA

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Abdul Nondo anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha jana usiku majira ya saa 5 hadi 6 akiwa jijini Dar es Salaam. 


Chanzo cha karibu cha mwanafunzi kikiongea na www.eatv.tv kimesema kuwa Abdul Nondo mpaka saizi haifahamiki yupo wapi na namba zake za simu pia hazipatikani toka jana usiku. 
Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa jana mwanafunzi huyo alituma ujumbe mfupi uliokuwa ukionyesha yupo kwenye hali ya hatari na baadae namba yake...

 

2 days ago

BBCSwahili

Kiongozi wa mtandao wa wanafunzi Tanzania Abdul Nondo apandishwa kizimbani

Kiongozi wa mtandao wa wanafunzi Tanzania Abdul Nondo, amepandishwa mahakamani leo katika mahakama ya wilaya ya Iringa mjini

 

2 weeks ago

BBCSwahili

Kiongozi wa wanafunzi Tanzania Abdul Nondo atoweka

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) umesema mwenyekiti wake Mahmud Abdul Ormari Nondo hajulikani alipo na kulitaka jeshi la polisi kuhakikisha anapatikana akiwa salama kwa haraka.

 

1 week ago

Zanzibar 24

Mtandao wa wanafunzi wamesema hawaamini uchunguzi uliofanywa na polisi kuhusu Nondo

Mtandao wa wanafunzi nchini Tanzania (TSNP) umesema usingeweza kupuuza taarifa za hatari ya usalama iliyokuwa ikimkabili mwenyekiti wao Abdul Nondo. Taarifa za kupotea kwa Bwana Nondo katika mazingira ya kutatanisha ziliibuka tarehe 6 Machi baada ya Nondo kutuma ujumbe kwa mmoja wa marafiki zake usiku wa manane akisema kuwa usalama wake uko hatarini. Hali hiyo ilipeleka taharuki miongoni mwa wanafunzi wenzake na jamii kwa ujumla huku wengi wakidhani kuwa bwana Nondo alikuwa...

 

1 week ago

Malunde

VIONGOZI WA MTANDAO WA WANAFUNZI TANZANIA WAHOJIWA NA DCI SAKATA LA NONDO

Mpaka kufikia leo Machi 14, 2018 saa 7:45 mchana viongozi wawili wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) walikuwa wamekwisha hojiwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Ofisa habari wa mtandao huo Helleh Sisya ambaye naye pia miongoni mwa watakaohojiwa, amesema hadi muda huo waliohojiwa ni mkaguzi wa haki za binadamu , Alphonce Lusako na katibu wa mtandao huo, Malekela Brigthon.

Viongozi wengine ambao hawajahojiwa hadi muda huu ni Sisya na mkurugenzi wa Idara ya sheria, Paul...

 

1 week ago

Malunde

WANAFUNZI TANZANIA HAWANA IMANI NA UCHUNGUZI WA POLISI...NONDO AONGEE

Nondo ,aliyedaiwa kujiteka
Mtandao wa wanafunzi nchini Tanzania (TSNP) umesema usingeweza kupuuza taarifa za hatari ya usalama iliyokuwa ikimkabili mwenyekiti wao Abdul Nondo.

Taarifa za kupotea kwa Bwana Nondo katika mazingira ya kutatanisha ziliibuka tarehe 6 Machi baada ya Nondo kutuma ujumbe kwa mmoja wa marafiki zake usiku wa manane akisema kuwa usalama wake uko hatarini.
Hali hiyo ilipeleka taharuki miongoni mwa wanafunzi wenzake na jamii kwa ujumla huku wengi wakidhani kuwa bwana Nondo...

 

2 weeks ago

Malunde

MWENYEKITI WA MTANDAO WA WANAFUNZI TANZANIA ALIYEPOTEA ATUPWA IRINGA

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania , Abdul Nondo ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) aliyeripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa hai eneo la Mafinga mkoani Iringa.

Imeelezwa kuwa, Nondo alijikuta katika eneo hilo baada ya kuzinduka kutoka katika lindi la usingizi na kuwauliza wenyeji wa eneo hilo kuwa hapo ni wapi? Wenyeji hao walimfahamisha kuwa yuko Mafinga mkoani Iringa na kisha akapelekwa katika kituo cha polisi kilichoko...

 

2 weeks ago

Zanzibar 24

Mwenyekiti Mtandao wa Wanafunzi Tanzania apotea kwa mazingira ya kutatanisha

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Abdul Nondo anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha jana usiku majira ya saa 5 hadi 6 akiwa jijini Dar es Salaam.

Chanzo cha karibu cha mwanafunzi kikiongea na www.eatv.tv kimesema kuwa Abdul Nondo mpaka saizi haifahamiki yupo wapi na namba zake za simu pia hazipatikani toka jana usiku.

Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa jana mwanafunzi huyo alituma ujumbe mfupi  uliokuwa ukionyesha yupo kwenye hali ya hatari na...

 

3 days ago

MwanaHALISI

Abdul Nondo atikisa

JESHI la polisi nchini, bado linaendelea kumshikilia, kinyume na sheria za nchi, Abdul Nondo, mwanafunzi wa mwaka wa tatu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kwa madai ya “kujiteka.” Anaripoti Saed Kubenea…(endelea). Taarifa zinasema, Nondo anayeshikiliwa na jeshi hilo, tokea tarehe 7 Machi mwaka huu – siku zaidi ya 13 sasa – amenyimwa ...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani