WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WATAKAOSHINDWA KUSIMAMIA AFYA YA MAMA NA MTOTO KUKIONA

 Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya imesema itawashughulikia wakurugenzi wote wa halmashauri ambao wataonekana kuwa chanzo cha ukosefu wa huduma bora za mama na mtoto katika hospitali za Wilaya na vituo vya afya kote nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu alipokuwa akifungua mkutano wa 24 wa Madaktari bingwa wa magonjwa ya Wanawake na Watoto (AGOTA) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
“ swala la afya ya mama na mtoto ni lililopewa kipaumbele kwa serikali ya Tanzania na Dunia kwa ujumla hivyo wakurugenzi wa halmashauri wanao wajibu wa kuhakikisha wanaboresha huduma hizi kwani ni vitu vidogo ambavyo vipo ndani ya bajeti yao, tutawachukulia hatua wakurugenzi wote ambao watashindwa kutimiza wajibu wao katika kulinda afya ya mama na mtoto” amesema Waziri Ummy.
Amesema zipo changamoto nyingi katika huduma hizi hivyo katika bajeti ya 2017/2018 wizara yake imetenga fedha za kutosha kwa ajili ya huduma za uzazi wa mpango ili ziwe bora na kuepuka kero ya wanawake wanaopata huduma hii kupanga foleni.
Ametaja kuwa katika tafiti inaonyesha kuwa ni wanawake 32 tu kati ya 100 ndio ambao wanatumia huduma ya uzazi wa mpango hivyo serikali itatumia njia nzuri zaidi kuwafikia wanawake wengi.
Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Madaktari bingwa wa masuala ya afya ya Mama na Mtoto (AGOTA), Prof Andrea Pembe amesema kuwa serikali imefanya kazi kubwa sana katika utoaji wa huduma katika vituo vya afya Tanzania .
Ameongeza kuwa uelewa mdogo wa jamii juu ya masuala ya afya ya uzazi yamechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa vifo vya Mama na mtoto.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Watoto na wanawake nchini AGOTA wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 24 wa Taasisi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar leo.Rais wa Shirikisho la Madaktari bingwa wa masuala ya afya ya Mama na Mtoto (AGOTA), Prof Andrea Pembe, akizungumza kabla ya kumkaribisha waziri Ummy Mwalimu kwa ajili ya ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar leo. Daktari Gileard Masenga kutoka Hospitali ya KCMC Moshi akitoa taarifa fupi juu ya tafiti iliyofanywa kuhusiana na Afya ya Mama na Mtoto nchini kwenye mkutano wa 24 wa Madaktari bingwa wa magonjwa ya Wanawake na Watoto (AGOTA) uliofanyika leo. Baadhi ya Madaktari walioshiriki mkutano wa 24 wa Madaktari bingwa wa magonjwa ya Wanawake na Watoto (AGOTA) wakifutilia mada zilizokuwa zinatolewa leo.Waziri Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari 

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Dewji Blog

Wakurugenzi wapya waaswa kusimamia mapato ya ndani ya halmashauri

Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)  Mhe. George Simbachawene amewaasa Wakurugenzi wapya kusimamia mapato ya ndani katika halmashauri zao ili waweze kutekeleza miradi ya maendeleo na kuwahudumia wananchi.

Waziri Simbachawene amesema hayo leo mjini Dodoma wakati wa hafla ya kuwaapisha Wakurugenzi wapya 13 walioteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli iliyofanyika katika jengo la Mkapa, Ofisi ya Rais,...

 

2 years ago

Habarileo

Watakaoshindwa kupeleka watoto shuleni kukiona

SERIKALI imeonya kuwa itawachukulia hatua za kisheria wazazi na walezi watakaoshindwa kuwapeleka watoto shule na kusisitiza kila mtoto anapaswa kupewa haki ya kupata elimu itakayoanza kutolewa bure kuanzia Januari.

 

2 years ago

Dewji Blog

Walimu watakaoshindwa kusimamia madawati Manyoni kukatwa mishahara

MKUU wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida,Geofrey Idelfonce Mwambe,amewaagiza walimu wa shule za msingi na sekondari wahakikishe samani ikiwemo madawati yanatunza vizuri,vinginevyo watakatwa sehemu ya mishahara yao, endapo yataharibika au kuvunjwa.

Mkuu huyo wa wilaya,ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi madawati 100 kwa shule za msingi za Bangayegya na Lulanga za halmashauri ya wilaya ya Itigi.Madawati hayo yametolewa msaada na benki ya NMB tawi la Itigi.

Alisema...

 

1 year ago

Channelten

Ujenzi wa vituo vya afya Waziri mkuu Kassim Majaliwa atoa agizo kwa Wakurugenzi wa halmashauri

screen-shot-2016-12-04-at-5-15-47-pm

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na majiji nchini kujenga vituo vya afya na hospitali za wilaya ili kupunguza msongamano katika hospitali za mikoa.

Waziri mkuu ambaye yupo katika ziara ya kikazi mkoani Arusha ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea hospitali ya mkoa huo ya Mountmeru na kujionea msongamano wa wagonjwa katika wodi ya akina mama na watoto ambapo ameshuhudia wagonjwa watatu wakilala katika kitanda kimoja.

Amesema hali hiyo imekuwa...

 

6 months ago

Michuzi

WIZARA YA AFYA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO KUFIKIA 2020

 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiongea na wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali  hawapo pichani wa Wizara ya afya kuhusiana na kuimarisha huduma bora za afya nchini  leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kushoto ni Naibu wa wizara hiyo Dkt. Faustine Ndungulile na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya. Wakati wa kikao chake na wakuu hao.


NA WAMJW-DAR ES SALAAMWIZARA ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee...

 

2 years ago

Channelten

Mradi wa Afya ya Mama na Mtoto Wakunga wa jadi kushirikishwa kuboresha afya ya uzazi

Screen Shot 2016-02-29 at 4.15.29 PM

Jumla ya akina mama 11 wajawazito, kutoka kata na vijiji vya Mohoro,  Ikwiriri, Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani,wamepoteza maisha katika kipindi cha Januari mpaka Desemba 2015, kutokana na  sababu mbalimbali zikiwemo zinazoelezewa kupuuzia ama kutofahamu umuhimu wa kuhudhuria kliniki wiki 12 baada ya ujauzito pamoja na umbali wa vituo vya afya.

Akizungumza na Channel Ten katika mahojiano wakati wa uzinduzi wa mradi wa majaribio wa ushirikishaji  wakunga wa jadi unaolenga kuboresha afya ya...

 

2 years ago

Channelten

Utekelezaji wa Afya ya mama na mtoto kwa Watumishi wa Afya

Screen Shot 2016-03-21 at 5.05.48 PM

Watumishi wa Afya ya mama na mtoto wametakiwa kutanguliza maslahi ya Umma katika utekelezaji wa majukumu yao huku wakitakiwa kuacha lugha zisizo na Staha wakati wa utoaji wa huduma.

Mkuu wa mkoa wa DSm Paul makonda ametoa wito huo wakati akizungumza na wauguzi na manesi kutoka mikoa ya Tanzania bara na zanzibar katika mafunzo ya siku mbili yanayoendelea jijini dsm yakiwa na lengo la kuimarisha utendaji kazi wao.

Amesema watumishi wa Afya wanawajibu mkubwa wa kuhakikisha wagonjwa wanapatiwa...

 

1 year ago

Dewji Blog

Wataalamu wa Afya watakiwa kupigania Afya ya Mama na Mtoto

Wataalamu wa  afya  wametakiwa kutumia utaalamu na wajibu wao katika kuokoa maisha ya mama na mtoto ili kuepuka vifo vitokanavyo na uzazi  kwa ajili ya kujenga taifa lenye kizazi imara.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa mkutano katika ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa huduma za afya ya uzazi na mtoto uliofanyika Mkoani Dodoma.

“Tumieni utaalamu wenu na wajibu mliopewa kuleta mabadiliko ya kiutendaji na ufanisi...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani