WAKUU WA MIKOA KANDA YA ZIWA VICTORIA WAKOSOA VIKALI TABIA YA WANASIASA KUIPAKA MATOPE DHAMIRA NJEMA YA SERIKALI KUPAMBANA NA UVUVU HARAMU

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akihutubia  hadhara ya kikosi kazi cha watu 260 alichokiunda kwa ajili ya operesheni Sangara 2018 na Wakuu wa Mikoa mitano inayozunguka Ziwa vicktoria  wakati wa mkutano wa kufanya tathimini ya Operesheni  hiyo. Picha na John Mapepele
NA JOHN MAPEPELE, MWANZA
WAKUU wa mikoa inayozunguka Ziwa Victoria wamekosoa vikali tabia ya baadhi ya wanasiasa kuipaka matope dhamira njema ya Serikali ya kupambana na uvuvi haramu ulioshamiri katika ziwa hilo na kutaka viongozi wa aina hiyo kutangaza masilahi yao kwenye eneo la uvuvi kabla ya kuwashambulia viongozi wanaosimamia zoezi hilo kwa misingi ya kisheria.
Wakizungumza kwenye kikao cha tathmini ya operesheni sangara awamu ya pili iliyowahusisha Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Makamanda wa Polisi wa mikoa na Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa wa mikoa yote inayozunguka Ziwa Victoria jijini Mwanza jana viongozi hao wametaka hatua zaidi zichukuliwe ili kunusuru rasilimali hizo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka alielezea kuchukizwa na tabia inayoanza kuota mizizi ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kuipaka matope dhamira nzuri ya Serikali ya kukabiliana na uvuvi haramu na kutaka viongozi wa aina hiyo watangaze masilahi yao kabla ya kuanza kuwashambulia viongozi wanaosimamia operesheni hiyo inayotekelezwa kwa mujibu wa sheria .   Viongozi wakuu wa Wizara  ya  Mifugo na Uvuvi waliokaa  wakiwa katika picha ya pamoja na makamanda wakuu wa Operesheni Sangara 2018 (waliosimama) wakati wa mkutano wa kufanya tathimini ya Operesheni  hiyo. 
“Viongozi wanaopinga operesheni ya kupambana na uvuvi haramu ni muhimu watangaze kwanza masilahi yao kuhusu eneo la uvuvi ili wasiendelee kuchafua taswira za viongozi wanaosimamia wizara hii”alisema Mtaka.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela alisema kumekuwepo na dhana zinazojengeka kwamba viongozi wa mikoa inayozunguka Ziwa Victoria hawaungi mkono mapambano ya kukabiliana na uvuvi haramu operesheni jambo ambalo alisema ni upotoshaji mkubwa na kwamba Serikali ya mkoa iko mstari wa mbele na kuwabana watendaji wa ngazi zote watakaobanika kufadhili uvuvi haramu.
Alisema ni muhimu operesheni hiyo iwe endelevu na kubainisha kuwa suala la uvuvi haramu haliwezi kumalizika kama hakuna dhamira ya dhati miongoni mwa wasimamizi wa sheria na kwamba uongozi wa mkoa huo hautakubali kuendelea kuwa na watumishi wazembe wataoshindwa kusimamia suala hilo.
Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina alitangaza kuanza kwa awamu ya tatu ya Operesheni Sangara yenye lengo la kupambana na uvuvi haramu katika Ziwa Victoria sambamba na kutangaza operesheni katika maziwa yote na kuagiza viongozi wakuu wa mikoa na wilaya kuwachukulia hatua kali viongozi wa chini wanaobanika kujihusisha na kufadhili uvuvi haramu. Viongozi wakuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi waliokaa wakiwa katika picha ya pamoja na sekretarieti ya Operesheni Sangara 2018 (waliosimama) wakati wa mkutano wa kufanya tathimini ya Operesheni hiyo. 
Pia alitangaza kuunda kanda mpya ya udhibiti na usimamizi rasilimali za uvuvi katika wilaya za Ukerewe na Sengerema huku akiunda ofisi mpya ya Kanda jijini Mwanza itakayokuwa inaratibu shughuli zote katika kanda hizo saba ili kuongeza usimamizi madhubuti wa rasilimali hizo.
Aidha Mpina aliongeza kuwa katika awamu ya tatu ya operesheni hiyo itahusisha pia Mahakama zinazotembea ili kuweza kutoa hukumu huko huko ziwani hali itayowezesha kuondokana kabisa na uvuvi haramu.
Aidha aliwataka watu wote wanaopinga operesheni ya uvuvi haramu wasome takwimu ili kujua ukubwa wa tatizo katika Ziwa Victoria ambapo jumla ya watuhumiwa 3,284 wamekamatwa kujihusisha na uvuvi haramu huku samaki wasioruhusiwa kilo 326,751 , mabondo kilo 5,142 zilikamatwa zikitoroshwa kwenda nje ya nchi na nyavu haramu 566,497 nazo zilikamatwa na kuteketezwa. Pia magari 257, mitumbwi 1278 , pikipiki 269 na injini za mitumbwi 564 vilikamatwa vikihusishwa na makosa ya uvuvi haramu.
Alisema katika baadhi ya maeneo ya Bushengere wilayani Ukerewe wazazi wamewaonya watoto wao kutotumika na mafisadi kwenye uvuvi haramu kwani wakikamatwa wao ndio wanaopata tabu na kutelekezwa ambapo wameweka azimio la kukataa kutumika tena kwenye jambo hilo.
Alisema kutokana na operesheni hizo zinazoendelea za kupambana na uvuvi haramu hadi kufikia mwezi Disemba mwaka huu watu wote wanaopinga na hata kuwaombea mabaya viongozi wa operesheni watapata aibu kubwa kwani idadi ya samaki itaongezeka huku akitoa wito kwa viongozi wa ngazi zote wenye mapenzi mema na nchi kuunga mkono vita hiyo kwa manufaa ya Taifa.
Katibu Mkuu Uvuvi, Dk. Yohana Budeba alisema wizara hiyo imejipanga kikamilifu kuhakikisha sekta ya uvuvi inatoa mchango mkubwa katika pato la Taifa na kwamba operesheni hiyo itaendelea hadi pale uvuvi haramu utakapokoma.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Tano Mwera alisema wamekuwa wakipokea malalamiko mengi kuhusu operesheni hiyo lakini kila walipofuatilia kupata ushahidi wa malalamiko hayo waliukosa jambo ambalo wamebaini kuwa ni njama za makusudi za kutaka kuhujumu nia njema ya Serikali ya kupambana na kutokomeza uvuvi haramu.
Kamanda Mkuu wa operesheni hiyo kutoka Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Hassan Shelukindo alisema katika operesheni hiyo jumla ya watuhumiwa 22 wakiwemo wenyeviti wa vijiji na vitongoji na viongozi wa BMU wamefungwa jela huku wengine 17 mashauri yao yakiwa yanaendelea Mahakamani kwa makosa ya kujihusisha na uvuvi haramu.
Shelukindo alisema pia watumishi 6 walikuwa kwenye operesheni hiyo waliondolewa kwa makosa mbalimbali ikiwemo ukiukwaji wa maadili ya kazi ambapo watumishi hao watachukuliwa hatua za kinidhamu na taasisi zao huku jumla ya sh. bilioni 7.5 zikikusanywa kutokana na faini pamoja mauzo ya mabondo,samaki na kayabo.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

4 years ago

Michuzi

KITUO CHA UWEKEZAJI CHAWAPONGEZA WAKUU WA MIKOA KATIKA JITIHADA ZAO ZA KUHAMASISHA UWEKEZAJI MIKOA YA KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji amewapongeza Wakuu wa Mikoa wa Kanda ya Ziwa katika juhudi zao za kuhakikisha Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa linafanyika.
Mikoa ambayo itashiriki katika Kongamano la Uwekezaji la Kanda ya Ziwa ni Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Kagera na Shinyanga Kongamano ambalo kwa pamoja litawakutanisha Wawekezaji pamoja na Serikali katika kujadili vivutio vya Uwekezaji vinavyopatikana katika mikoa hiyo ya kanda ya Ziwa.
Kituo cha Uwekezaji Kimejizatiti...

 

4 years ago

Michuzi

TIC YAINGIA MKATABA WA MAKUBALIANO YA UWEKEZAJI NA WAKUU WA MIKOA YA KANDA YA ZIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki (wa pili kushoto) akisaini Mikataba ya Makubaliano ya Uwekezaji na Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa,wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo (wa pili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mh. Yohana Balele (kushoto).Wanaoshuhudia ni Waziri wa Viwanda na Biashara,Mh. Abdallah Kigoda pamoja na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),Mh. Aggrey Mwanri.na Kulia ni Mwenyekiti wa Kongamano la...

 

4 years ago

Michuzi

TIC YASAINI MIKATABA YA MAKUBALIANO YA UWEKEZAJI NA WAKUU WA MIKOA YA KANDA YA ZIWA

 Makamu wa Rais,Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki wakati alipotembelea Banda la Kituo hicho kwenye Maonyesho ya Kongamano la Uwekezaji yaliyoanza jana kwenye hoteli ya Malaika jijini Mwanza .Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Everist Ndikilo ambaye ndie Mwenyeji wa Kongamano hilo.  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Julieth Kairuki (katikati) akisaini Mikataba ya...

 

11 months ago

Michuzi

Viongozi wa Dini kanda ya Ziwa Wabebeshwa mzigo, Utunzaji wa Mazingira Ziwa Victoria

Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwa, akifungua kikao hicho, pembeni kulia ni Mratibu wa LVEMP Bw. Omari Myanza.Na Atley Kuni,  Mwanza.
Serikali mkoani hapa, imewapa jukumu kubwa viongozi wa dini kutoka baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa kuhakikisha wanakuwa bega kwa bega katika kulitunza ziwa Viktoria na Maliasili zake ili liweze kuwa tegemeo kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Akifungua Semina ya siku moja mkoani hapa Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, na risala yake kusomwa na Mkuu wa...

 

2 years ago

Habarileo

Uvuvi haramu washamiri Ziwa Victoria

UVUVI haramu wa kutumia sumu na nyavu zenye matundu madogo unadaiwa kukithiri katika Ziwa Victoria wilayani Rorya mkoani Mara.

 

2 years ago

Habarileo

Samia akerwa uvuvi haramu Ziwa Victoria

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na kuendelea kushamiri kwa uvuvi haramu katika Ziwa Victoria unaosababisha samaki zipungue na kuharibu mazingira.

 

1 year ago

VOASwahili

Wanasiasa wataka sheria za uvuvi ziwa Victoria zitungwe upya

Mara nyingi, tanzania haijihusishi katika migogoro ya matumizi ya ziwa Victoria licha ya kuwa na mgao mkubwa wa asilimia 37.5.

 

2 years ago

CHADEMA Blog

Mbowe awaonya vikali wakuu wa mikoa na wilaya Nchini

Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe amelaani vikali tabia ya wakuu wa wilaya na mikoa nchini kuingilia mamlaka zisizo zao.Kiongozi huyo alikuwa alikuwa akizungumza na wanahabari mjini Arusha mara baada ya kuhudhuria kesi ya Rufaa ya aliyekuwa mbunge wa Longido Onesmo Ole Nangole.Kiongozi huyo wa upinzani bungeni ameonya na kulaani tabia ya mkuu wa mkoa wa Arusha akishirikiana na wakuu wake

 

4 months ago

Michuzi

RC MARA TOKOMEZA UVUVI HARAMU ZIWA VICTORIA-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza  Mkuu wa Mkoa wa Mara, Bw. Adam Malima kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa  wahakikisha wanatokomeza uvuvi haramu katika ziwa Victoria.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumapili, Januari 21, 2018) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa huo katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi  mkoani Mara.
“Kuna tatizo kubwa la uvuvi haramu katika Ziwa Viktoria. Fanyeni doria za mara kwa mara na watakaobainika hatua stahiki za...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani