WALLACE KARIA RAIS MPYA WA TFFKutoka mjini Dodoma katika ukumbi wa St Gasper ulipofanyika mkutano mkuu wa shirikisho la soka Tanzania TFF, mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Revocatus Kuuli ametangazwa matokeo ya uchaguzi Mkuu wa TFF kwa wajumbe, makamu na Rais wa TFF.Aliyekuwa makamu wa Rais na kaimu wa Rais wa TFF Wallace Karia ametangazwa rasmi kuwa Rais mpya wa TFF kwa kupata jumla ya kura 95 na kuwashida Ally Mayay, Emmanuel Kimbe, Shija Richard, Iman Madega na Fredrick Mwakalebela.

Kwa ushindi huo sasa rasmi Wallace Karia atatawala nafasi ya Rais wa TFF hadi 2021 makamu wake akiwa ni Michael Richard Wambura aliyewashinda wagombea wenzake wengine watano.
Matokeo ya Urais
Kura ziliopigwa-128Zilizoharibika-3Iman Madega- 8Mwakalebela- 3Emmanuel Kimbe- 1Shija Richard- 9Ally Mayay- 9Wallace Karia- 95 (Mshindi)

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

1 month ago

Michuzi

RAIS WA TFF WALLACE KARIA AOMBOLEZA KIFO CHA OMARY KAPERA:


Kufuatia kifo cha beki wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Omary Kapera (wa tatu toka kulia) ,Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kifo cha beki huyo wa zamani. Rais Karia akitoa salamu za rambirambi amesema ni masikitiko makubwa kumpoteza mmoja wa wachezaji wa zamani aliyeitumikia pia timu ya taifa. "Nimeshtushwa na taarifa hizo za kifo cha Kapera hasa ikichukuliwa bado tupo kwenye majonzi ya kumpoteza...

 

2 months ago

Michuzi

RAIS WA TFF WALLACE KARIA KUKUTANA NA WAHARIRI WA HABARI DEC 27 MWAKA HUU

Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia (kulia, akiwa na Makamu wake Michael Wambura) atakutana na Wahariri wa Habari za Michezo Jumatano Desemba 27, 2017.
Pamoja na mambo mengine Rais Karia atazungumzia miezi minne tokea uongozi uliopo umeingia madarakani pamoja na vitu vilivyofanyika katika muda huo.Aidha Rais Karia ataelezea changamoto mbalimbali zilizopo TFF pamoja na njia gani inatumika/Itatumika kuweza kupiga hatua kwa mpira wa Tanzania.Taarifa zaidi za mkutano...

 

8 months ago

Michuzi

WALLACE KARIA NA SALUM MADADI KUKAIMU NAFASI ZA RAIS NA KATIBU MKUU TFF, TWFA YAPITISHA MAJINA YA WAGOMBEA

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, iliyokutana leo Jumamosi Julai 01, 2017 kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam imempitisha Wallace Karia (kushoto) kuwa Kaimu Rais wa shirikisho. Kadhalika, Kamati hiyo ya Utendaji ya TFF, imempitisha Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi (kulia) kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF.Viongozi hao watakaimu nafasi hizo tajwa hadi hapo mahakama itakavyoamua kuhusu kesi zinazowakabili kwa sasa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu,...

 

6 months ago

Zanzibar 24

Urais TFF: Ni Wallace Karia

Matokeo ya uchaguzi mkuu wa viongozi wapya wa TFF yametangazwa rasmi mjini Dodoma baada ya zoezi zima la uchaguzi kukamilika.

Rais mpya wa TFF ni Wallace Karia ambaye ameshinda kwa kura 95 kati ya 128 za wajumbe waliopiga kura kwenye uchaguzi huo.

Karia amewashinda Iman Madega, Shija Richard, Ally Mayay, Emanuel Kimbe na Fredrick Mwakalebela ambao walikuwa wakiwania nafasi ya urais wa TFF.

Kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa TFF, Karia alikuwa makamu wa Rais chini ya Jamal Malinzi ambapo...

 

7 months ago

Michuzi

IDARA YA UHAMIAJI:MGOMBEA URAIS WA TFF WALLACE KARIA NI RAIA HALALI WA TANZANIA

Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ally MtangaNa Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Idara ya Uhamiaji Nchini imethibitisha kuwa  Kaimu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wallace John Karia ambaye ni Mgombea Urais wa TFF  katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika August 12  mwaka huu ni Raia halali wa Tanzania.
 Akizungumza na waandishi habari makao makuu ya Idara hiyo, Msemaji Mkuu wa Uhamiaji,  Ally Mtanga amesema kuwa mmoja wa wagombea wa Urais wa TFF alimkatia rufaa mgombea mwenzake...

 

8 months ago

Mwananchi

Karia, Sima waruka kihunzi cha pingamizi TFF

Wagombea wa uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka (TFF), Wallace Karia na Mussa Sima wameshinda mapingamizi yao waliyowekewa na John Kijumbe na Hussen Mwamba.

 

8 months ago

Mwananchi

Kufa kufaana: Karia, Madadi wakaimu nafasi za Malinzi, Mwesigwa TFF

Makamu wa rais, Wallace Karia ameteuliwa kukaimu nafasi ya rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi aliyeko  rumande akituhumiwa kwa makosa 28 tofauti.

 

6 months ago

Michuzi

BREAKING NYUUUZZZZZ.....: WALLES KARIA ASHINDA URAIS WA TFF, MICHAEL WAMBURA KUWA MAKAMU WAKE

Shirikizo la mpira wa miguu nchini (TFF), limepata uongozi mpya leo baada ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa shirikisho hilo, kufanya uchaguzi hii leo huko Mkoani Dodoma, na kupatikana Rais mpya wa Shirikisho ambaye ni Walles Karia aliyeibuka na ushindi wa kishindo wa kura  95, huku Michael Wambura akiibuka kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo kwa Kura 85. Wajumbe wa Mkutano Mkuu waliopiga kura leo ni 127.Rais mpya wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Walles Karia Makamu wa Rais mpya wa...

 

1 month ago

Michuzi

RAIS KARIA AMPONGEZA DAMAS NDUMBARO UBUNGE SONGEA MJINI

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Ndugu Wallace Karia kwa niaba ya Shirikisho anatoa pongezi kwa mwanamichezo daktari wa Sheria Dr.Damas Ndumbaro kwa kushinda kiti cha Ubunge Jimbo la Songea Mjini.
Rais Karia amesema ushindi wa Dr.Ndumbaro unaongeza wanamichezo zaidi katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wanaweza kuwa chachu ya maendeleo ya michezo ikiwemo mpira wa miguu.
Amesema uzoefu wa Dr.Ndumbaro katika mpira wa miguu utasaidia katika nyanja hiyo na...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani