WANACHAMA CHADEMA KAKONKO WATIMKIA CCM

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
JUMLA ya wanachama 27 wa Chadema wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM)wilayani Kakonko mkoani Kigoma kutokana na kuvutiwa na utendaji kazi wa Serikali ya CCM.
Wanachama hao wamejiunga leo katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya kilichoendeshwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole.
Wakizungumza baada ya kukabidhiwa kadi na kiongozi huyo,wanachama hao wapya wamesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuguswa na kazi zuri inayofanywa na CCM na kukosa demokrasia Katika chama chao cha Chadema kwa madai kipo kwa ajili ya watu wachache.Riberatusi Kamamba ni mmoja kati ya wanachama wa Chadema waliohamia CCM ambapo ameeleza ameamua kuhamia katika chama hicho kutokana na utendaji kazi na utekelezwaji wa ilani ya chama hicho unavyo fanya na Rais wa Chama hicho anavyo hakikisha fedha za Serikali zinatumika ipasavyo.
Amesema mwanzoni viongozi walikuwa hawana utaratibu wa kuwatembelea wananchi na kuangalia changamoto wanazo kutana nazo na kukagua miradi ya maendeleo."Lakini kwa sasa Chama hicho kinafanya kazi hiyo na kuhakikisha kinawachukulia hatua wale wote wanaotumia fedha za Serikali kwa matakwa yao binafsi na watumishi wote wanatembelea wananchi kutatua kero," amesema.
Nae Gidioni Ruhaga aliekuwa Muasisi wa Chadema amesema ana mambo mengi yaliyomfanya ahamie katika chama hicho,miongoni mwa mambo hayo ni sera zilizopo CCM.Amesema kwa sasa chama hicho kimerudisha heshima na utaratibu uliokuwa nao ni na kinajali demokrasia na hakina ubaguzi.Amesema chama alichokuwa akikitumikia kimekuwa kinaubaguzi na hakiwajali wanachama wanaopigana kukiweka madarakani na ni wakwanza kuipinga Serikali haitendi haki lakini hata wao hawafanyi hivyo."Na wamekuwa wa kwanza kujinufaisha na fedha zinazotolewa kwaajili ya kukiendesha chama hicho," amesema.Akizungumza na wanachama waliojitokeza katika kikao hicho Polepole amesema amesikitishwa na kitendo kilicho fanywa na upinzani cha kuwafungia ndani madiwani wote wa chama hicho na kuwanyang'anya simu zao kwa kuhofia watahamia Chama tawala .
Amesema viongozi hao baada ya kusikia yakuwa kuna ugeni wa kiongozi huyo waliamua kuwaweka ndani madiwani na kueleza kila mwananchi anahaki ya kuhamia chama chochote anacho kitaka hata wao wamewaachia viongozi na wanachama wengine kuhamia chama wanacho kihitaji."Imeandikwa hata kwenye vitabu vya dini alaaniwe anae muogopa mwanadamu nimeshangaa sana watu wanatuogopa hadi wanaamua kuwaficha madiwani wao."Ssi hatutamnunua mtu kwa gharama yeyote ile hata huyo Mbunge wenu akija kwetu hatumuhitaji, tunahitaji wananchi wanaoamua wenyewe kujiunga na Chama tawala kwa kuona utendaji kazi na misingi ya chama chetu", amesema Polepole.730236

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

4 years ago

Michuzi

KAMPENI ZA CCM KALENGA ZATINGA KIJIJI ALICHOZALIWA MGOMBEA WA CHADEMA, MWENYEKITI WA CHADEMA NA WANACHAMA 50 WATIMKIA CCM

 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kijiji cha Wangama, Fred Mgata (kulia) akikabidhi kadi za chyama hicho kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga baada ya yeye na wanachama wengine 50 wa Chadema kuamua kukihama na kujiunga CCM katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika  katika Kijiji hicho kilichopo Kata ya Luhota, Iringa Vijijini leo. Mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia Chadema ambaye ni mzaliwa wa kijiji hicho,  Grace Tendega alikuwa chini ya...

 

1 year ago

Michuzi

CCM YASOMBA WANACHAMA WAPYA 102 WAKIWEMO WA CUF,CHADEMA NA ACT WAZALENDO WILAYANI KAKONKO MKOANI KIGOMA


Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma imevuna jumla ya wanachama wapya 102 kutoka chama cha Act Wazalendo na Chama cha Wananchi Cuf.
Wanachama hao ambao wamepokelewa na mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma Prof Joyce Ndalichako ambaye aliwakabidhi wanachama hao wapya kadi 102 , akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha ACT wazalendo Wilaya ya Kakonko pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF Wilayani humo .
Zoezi hilo alilifanya...

 

3 years ago

Mwananchi

Wanachama CCM watimkia ACT- Wazalendo

Zaidi ya wanachama 100 kutoka CCM, Kata ya Chihanga, Manispaa ya Dodoma wamejiunga na ACT- Wazalendo.

 

1 year ago

Mwananchi

Makada wa Chadema watimkia CCM

Makada 15 wa Chadema waliojitambulisha kuwa viongozi wa chama hicho Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza  wamehama chana hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

 

3 years ago

Mtanzania

Vigogo CCM Arusha watimkia Chadema

IMG_20150809_114435NA ELIYA MBONEA, ARUSHA

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Mkoa huo, Isack Joseph, wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha  Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Ole Nangole na Joseph walifikia uamuzi huo jijini hapa jana na kusema kwa nyakati tofauti wamelazimika kuchukua uamuzi huo kwa kuwa utaratibu wa kumpata mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ulikiukwa.

Kwa mujibu wa wana CCM hao, wakati wa mchakato...

 

1 year ago

Global Publishers

Vigogo Chadema Watimkia CCM (+VIDEO)

Said Arfi

DODOMA: Katika mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), amepokelewa Moses Machali Mbunge wa zamani wa Kasulu Mjini kwa Tiketi ya NCCR- Mageuzi.

Moses Machali

Aidha Said Arfi naye ametangaza kujiunga na CCM na wamepokelewa leo rasmi katika mkutano uliyofanyika mjini Dodoma.

VIDEO MKUTANO MKUU WA CCM NEC DODOMA

Salum Milongo/GPL

The post Vigogo Chadema Watimkia CCM (+VIDEO) appeared first on Global Publishers.

 

2 months ago

Zanzibar 24

Madiwani watatu wa Chadema watimkia CCM

Madiwani watatu wa CHADEMA akiwemo Jacob Silas Mollel wa Kata ya Elang’atadapash, Elias Mepukori Mbao wa Kata ya Kamwaga na  Diyoo Lomayani Laizer Kata ya Olmolog katika halmashauri ya Longido mkoa wa Arusha, wametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi ( CCM).

Sababu za kujiunga CCM ni kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika vita dhidi ya ufisadi, kuinua uchumi na pia kurejesha nidhamu kazini.

Tukio hilo limejiri ikiwa ni siku moja tu imepita tangu...

 

3 years ago

Michuzi

NANGOLE NA KADOGOO WA CCM ARUSHA, WATIMKIA CHADEMA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Chama cha Mapinduzi kimeendelea kupoteza wanachama  wake mara baada  Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Onesmo Nangole pamoja na Katibu Mwenezi wa Mkoa huo Isaac Joseph kutangaza rasmi kukihama chama hicho cha CCM na kujiunga na CHADEMA.
Uamuzi huo ulifanyika jana jijini Arusha katika moja ya hotel maarufu ambapo viongozi hao walipata wasaa wa kupokelewa na uongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani