Wanaosomea diploma kupewa mikopo

SERIKALI imewasilisha pendekezo la mabadiliko ya Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili kuwezesha wanafunzi wanaochukua Stashahada katika vipaumbele vya kitaifa, kupewa mikopo ya kuwawezesha kuchukua elimu husika.

habarileo

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

MillardAyo

AyoTVMAGAZETI: Vilio Mgodi mkubwa nchini kufungwa,Wanaosoma diploma kupewa mikopo

Kila siku asubuhi ungana na Alice Tupa wa AyoTV kwa uchambuzi wa habari zote kubwa kutoka kwenye magazeti ya Tanzania ambapo leo January 18 2017 ameshazisoma zote kubwa ikiwa ni pamoja na Vilio Mgodi mkubwa nchini kufungwa,Wanaosoma diploma kupewa mikopo. ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV JANUARY 19 2017? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI […]

The post AyoTVMAGAZETI: Vilio Mgodi mkubwa nchini kufungwa,Wanaosoma diploma kupewa mikopo appeared first on millardayo.com.

 

2 years ago

Bongo5

Wanaosomea diploma nao kuanza kunufaika mkopo wa HELSB

Serikali imewasilisha pendekezo la mabadiliko ya Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili kuwezesha wanafunzi wanaochukua Stashahada katika vipaumbele vya kitaifa, kupewa mikopo ya kuwawezesha kuchukua elimu husika.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema mabadiliko hayo, yamelenga kuwezesha kasi katika uchumi wa viwanda.

Profesa Ndalichako alisema mabadiliko katika Sheria Namba 4 ya Mwaka 2016 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu...

 

8 months ago

Malunde

BODI YA MIKOPO YASITISHA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA DIPLOMA

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuutaarifu umma kuwa imesitisha mpango wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma stashahada (Diploma) kuanzia mwaka wa masomo 2018/2019 kama ilivyotangaza awali.

Itakumbukwa kuwa tarehe 10 Mei mwaka huu, HESLB ilitoa mwongozo unaosimamia utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019. Mwongozo huo, pamoja na mambo mengine, unaeleza kuwa HESLB itaanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa stashahada na kuwa mwongozo kuhusu utaratibu wa kuomba...

 

3 years ago

Habarileo

Wanafunzi ualimu kuishia diploma, mikopo yafutwa

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha St Joseph (SJUIT) Kampasi ya Arusha (kilichofutiwa usajili), waliokuwa chini ya programu ya shahada ya miaka mitano ya ualimu wa sayansi, wametakiwa kusoma ngazi ya cheti au stashahada. Kama watataka kusoma ngazi ya juu, watapaswa kuomba upya udahili.

 

8 months ago

Malunde

WANAFUNZI 40,000 ELIMU YA JUU KUPEWA MIKOPO 2018/2019

ZAIDI ya wanafunzi 40,000 wa mwaka wa kwanza wa vyuo vya elimu ya juu, wanatarajia kupata mikopo katika mwaka wa masomo wa 2018/2019.
Dirisha la maombi ya mikopo lilifunguliwa jana na linatarajiwa kufungwa Julai 15 mwaka huu huku bajeti ya fedha za mikopo kwa mwaka 2018/2019 ikiwa ni Sh bilioni 427.Hata hivyo wakati dirisha hilo likifunguliwa, bodi hiyo imesisitiza   waombaji ambao wazazi/walezi ni wamiliki wa biashara, mameneja wakubwa katika mamlaka zinazotambulika, hawaruhusiwi kuomba...

 

1 year ago

Malunde

MSAKO MKALI MIKOPO ELIMU YA JUU KUANZA JUMATATU,WANUFAIKA 119,497 KUPEWA KIBANO


BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), inatarajia kuanza kampeni ya kuwasaka jumla ya wanufaika 119,497 nchini, ambao wamekiuka sheria iliyoanzisha bodi hiyo kwa kutoanza kurejesha mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 285, waliyokopeshwa tangu 1994/1995 na mikopo yao imeiva.

Aidha, bodi hiyo inatarajia kuanza kufanya ukaguzi kwa waajiri mbalimbali nchini kote ili kubaini kama katika orodha za waajiriwa wao, kuna wanufaika wa mikopo ambao hawajaanza kurejesha.
Akizungumza na...

 

2 years ago

Habarileo

Wanaosomea chini ya miembe waongoza kimkoa

SHULE ya msingi Kashifa katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi licha ya kukabiliwa na uhaba wa madarasa na walimu, imeshika nafasi ya kwanza kiwilaya na kimkoa katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2016.

 

2 years ago

Dewji Blog

China kufadhili wanafunzi 120 wanaosomea lugha ya kichina kila mwaka

Ushirikiano wa kiutamaduni baina ya nchi ya Tanzania na China unazidi kuimarika ambapo ubalozi wa China nchini umepanga kufadhili wanafunzi wa elimu ya juu 120 kila mwaka ambao wanakwenda kusomea tamaduni na lugha ya kichina nchini humo.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Millao katika maonyesho ya kuenzi watunzi na waandishi wa tamthilia wa nchini China, ametoa wito kwa vijana kuitumia fursa hiyo ya kielimu.

“Vijana wengi wanakwenda China kujifunza...

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani