Wanne washikiliwa wakielekea kujiunga na kundi la kigaidi Al-Shabaab

Watu wanne wanaoaminika kuwa raia wa Burundi wameshikiliwa na polisi nchini Kenya baada ya kugundulika walikuwa wakielekea Somalia kujiunga na kundi la al-Shabaab .

Msemaji wa Polisi George Kinoti, amebainisha kuwa Maafisa wa ujasusi walikuwa wakiwafuatilia washukiwa hao baada ya kupata habari kuhusu mipango yao ya kwenda kujiunga na kundi la Al-Shabaab.

Amefafanua kuwa washukiwa hao wanne walikamatwa katika kizuizi cha polisi mjini Isiolo takriban kilomita 350 kaskazini mwa mji mkuu wa nairobi wakielekea katika mji wa mpakani wa Mandera.

Maafisa wa polisi pia wanasema wanne hao waliingia nchini Kenya kama watalii kupitia visa huru ya ushirikiano kati ya Burundi na Kenya.

Maafisa katika Ubalozi wa Burundi mjini Nairobi wanasema kuwa watatoa taarifa kamili kuhusu kukamatwa huko baada ya kushauriana na mamlaka ya Kenya.

Mnamo mwezi Januari mwaka huu raia mwengine wa kigeni, ambaye alikuwa Mtanzania alikamatwa mjini Mandera akijaribu kuvuka na kuingia Somalia kwa lengo la kujiunga na kundi hilo la al-Shabaab.

The post Wanne washikiliwa wakielekea kujiunga na kundi la kigaidi Al-Shabaab appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Ippmedia

Wanawake 4 washikiliwa na polisi kwa kuwapa mafunzo ya kigaidi watoto jijini DSM.

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam inawashikilia wanawake wanne waliokutwa wamejificha porini na watoto kadhaa wakipewa mafunzo ya kigaidi.

Day n Time: Jumatano saa 2:00 UsikuStation: ITV

 

3 years ago

BBCSwahili

Misri:Hamas si kundi la kigaidi

Mahakama nchini Misri imefuta hukumu ya awali ambayo ilikitaja chama cha Hamas cha Palestina kama kikundi cha kigaidi.

 

4 years ago

BBCSwahili

Muslim Brotherhood ni kundi la kigaidi

Serikali ya Misri yakipiga marufuku chama cha Muslim Brotherhood na kukitangaza kuwa kundi la kigaidi

 

2 years ago

BBCSwahili

Arab League:Hezbollah ni kundi la Kigaidi

Muungano wa mataifa ya kiarabu Arab League umetangaza kuwa vuguvugu la kishia nchini Lebanon Hezbollah ni kundi la kigaidi

 

3 years ago

GPL

TASWIRA KUTOKA TANGA KATIKA MAPAMBANO YA POLISI NA KUNDI LA KIGAIDI

Helkopta ya polisi pamoja na gari vikiwa eneo la mapango ya Amboni, Tanga wakati wa mapambano ya polisi na kundi linalodhaniwa kuwa la kigaidi. Eneo la mapango ya Amboni.…

 

8 months ago

VOASwahili

Shambulizi la kigaidi laua watu wanne Kenya

Bomu lililokuwa limetengenezwa kienyeji limeua watu wanne waliokuwa wanasafiri kwenye gari la abiria kaskazini ya Kenya katika kile kilichoelezwa kuwa inadhaniwa ni shambulizi la kigaidi,

 

2 years ago

Mwananchi

Walimu wanne na wanafunzi wanane washikiliwa uchomaji shule moto

Jeshi la polisi wilayani Monduli Mkoa wa Arusha, linawashikilia kuwahoji walimu wanne na wanafunzi wanane kutokana na tuhuma za uchomaji moto Shule ya Sekondari Ole Sokoine.

 

10 months ago

VOASwahili

Sweden yaomboleza shambulizi la kigaidi lilouwa watu wanne

Taifa la Sweden lilifanya maombelezo kwa kukaa kimya dakika moja Jumatatu kwa ajili ya kuwakumbuka wahanga wa shambulizi la kigaidi lililotokea Ijumaa ambapo watu wanne waliuawa na wengine 15 kujeruhi.

 

3 years ago

BBCSwahili

Al Shabaab ni kundi la aina gani?

Haya hapa maelezo kuhusu kundi hilo katika sekunde 60.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani