Wasanii wa Bongo Muvi Waandamana Kariakoo Dar (+Video)

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akishirikiana na Wizara ya Habari pamoja na wasanii wa filamu wameendesha operesheni maalum katika mitaa ya Kariakoo Jijini Dar es salaam kwa dhumuni la kupambana na wazalishaji wa CD ‘feki’ za filamu kutoka nje ya nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa katika operesheni hiyo Kariakoo Jijini Dar es salaam.

Hatua hiyo imekuja baada ya wasanii wa filamu nchini kumtembelea RC Makonda na kulalamika juu ya filamu hizo za nje kwa madai zimekuwa zikiwaharibia biashara kwa kuwa zinauzwa kwa bei ndogo na pia hazilipi kodi, ilhali wao wanalipa. RC alitoa siku 10 ambazo zimemalizika jana kwa wazalishaji pamoja na wauzaji wa CD feki kuacha biashara hiyo huku akiwataka wale wenye uwezo kufanya biashara hiyo kufuata taratibu halali za kibiashara.

Akiongea na wafanyabishara hao wakiwa wamefunga maduka yao, RC Makonda amesema hana lengo la kukataza filamu za nje ziuzwe nchini, ila watu ambao wanafanya biashara hiyo wanatakiwa kufuata taratibu kama ambavyo wasanii wa filamu wa ndani wamekuwa wakifanya katika filamu zao.

“Yule anayesambaza na kuzizalisha ndiye ambaye tunamhitaji. Nyie wafanyabiashara tumewaandalia utaratibu wa vitambulisho kutoka Bodi ya Filamu ambavyo vitafanya mtambulike, kwa sababu hakuna biashara isiyotambulika duniani,” alisema RC Makonda. “Hivi vitambulisho vitakuwa na madaraja, mkionana na wahusika wa Bodi ya Filamu watawaelezea nini cha kufanya. “Wale wenye mitambo ya kuzalisha wapo 13 tukutane Polisi Central Jumatatu mkiwa na CD zenu,”

“Hivi karibuni Mh Waziri hapa bandarini alifanikiwa kukamata kontena zenye CD za nje zenye thamani ya shilingi bilioni 4. Wale watu wakawa wanasema ni empty CD, kuja kuzikagua tukakuta zina content ndani. Kwa hiyo lengo letu sio kuwazuia kufanya biashara, bali tunataka mfanye biashara lakini kwa kufuata taratibu zote. leo nimekuja na maafisa 200 wa TRA ambao watazunguka kwenye maduka mbalimbali kuangalia kama watu wanalipa kodi, kwa hiyo kama uko hapa na unajua mambo yako hayapo sawa nakuomba kabisa uwatafute wahusika wakuambie nini unatakiwa kufanya,” aliongeza RC Makonda.

Kwa upande mwingine, mmoja kati ya wafanyabishara aliyejitambulisha kwa jina la Salim Majonjo, amedai wanapata wakati mgumu kuuza kazi za wasanii wa Bongo Movie kwa madai kua hazina ubora na zinazungumzia mapenzi zaidi, ndiyo maana ameamua kugeukia kwenye soko la filamu za nje.

“Mh atufikirie na sisi wafanyabiashara wadodo wadogo, sisi ndo tunajua hali ya soko la filamu likoje. Ni filamu chache za Bongo ambazo unaweza ukauza tena zinahesabika. Yaani unaweza kukaa toka asubuhi mpaka jioni na usiuze filamu hata moja lakini filamu za nje zikawa zinatembea muda wote, stori zao kila siku zile zile watu wanachoka. Lakini ukileta filamu ya marehemu Kanumba inauza tena sana. Jiulize kwanini hao filamu zao haziuzi. Mimi ningewashauri wafanye kazi nzuri ambazo zitawavutia mashabiki wao huo ndio utakuwa muarobani wa hicho wanachokizungumzia,” alisema mfanyabiashara huyo.

Mmoja kati ya wasanii wa filamu ambao walikuwa katika opereshini hiyo, Rado, ameishukuru ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, kwa hatua hiyo huku akiwataka Watanzania kwa ujumla kuwaunga mkono.

“Kwanza namshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa hatua hii nzuri, sisi kama wasanii tunatambua juhudi za serikali katika kuhakikisha wasanii wananufaika na kazi zao, na pia serikali inapata kodi yake. Kila msanii analipa kodi kupitia movies zetu, kila movie ikiuzwa asilimia 30 inaenda kwa serikali, kwa hiyo mnaona ni namna gani tunalipa kodi. Sisi tunataka na hawa ambao wanaingiza fulamu za nje walipe kodi kama sisi kwa sabubu wote tunatumia soko moja tena mbaya zaidi wao filamu zao wanauza kwa bei ya chini zaidi,” alisema Rado.

Muigizaji huyo amewataka wasanii wenzake wa filamu kuendelea na vita hiyo ili kahikikisha wananufaika na kazi zao.

Bongo5

Bongo Movies

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Global Publishers

Wasanii wawili wafa Bongo Muvi

 

BACK-WIKIENDA

Stori: Imelda Mtema, Wikienda
Dar es Salaam: Misiba! Wakati wadau wa Bongo Movies wakiwa kwenye majonzi ya kifo cha Michael Dennis ‘John Woka’, kwenye Bongo nako kuna pigo la kuondokewa na wasanii wawili, Maneno Gongo ‘Mr Gongo’ na Jennifer Vincent ‘Mama Utajiju’.

Gongo alifariki dunia wiki iliyopita katika Hospitali ya Muhimbili baada ya kusumbuliwa na presha kwa muda mrefu.

BACK-WIKIeENDA

Marehemu Gongo aitwaye Hamza Mchuwa.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa masikitiko, ndugu wa marehemu Gongo...

 

2 years ago

Bongo Movies

Wasanii Wawili Wafariki Bongo Muvi

WIKIENDA

Misiba! Wakati wadau wa Bongo Movies wakiwa kwenye majonzi ya kifo cha Michael Dennis ‘John Woka’, kwenye Bongo nako kuna pigo la kuondokewa na wasanii wawili, Maneno Gongo ‘Mr Gongo’ na Jennifer Vincent ‘Mama Utajiju’.

Gongo alifariki dunia wiki iliyopita katika Hospitali ya Muhimbili baada ya kusumbuliwa na presha kwa muda mrefu.

BACK-WIKIeENDA

Marehemu Gongo aitwaye Hamza Mchuwa.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa masikitiko, ndugu wa marehemu Gongo aitwaye Hamza Mchuwa, alisema kuwa msanii huyo...

 

3 years ago

Michuzi

WASANII WA BONGO MUVI WAPEWA SEMINA NA TCRA

 Mkurungezi wa Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA, Dk.Ally Simba akizungumza na waandishi wa habari juu ya semina ya kuwapiga brashi wa wasanii wa bongo Movie leo jijini Dar Dar es Salaam. Afisa Mwandamizi Mkuu wa Kitengo cha Watumiaji wa Huduma za Bidhaa za Mawasiliano wa TCRA,Thadeo Ringo akizungumza na baadhi na wasanii waliohudhuria semina hiyo hawapo pichani iliyoyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi  Makao Makuu,Kitengo cha Kuzuia Uhalifu...

 

2 years ago

Global Publishers

Wasanii Bongo Muvi wachangia damu Palestina

1.Mkongwe wa maigizo, Ahmed Olotu 'Mzee Chilo'akishiriki zoezi la kuchangia damu.Anayemuhudumia ni muuguzi wa Hospitali ya Parestina. Mkongwe wa filamu, Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’akishiriki zoezi la kuchangia damu. Anayemuhudumia ni muuguzi wa Hospitali ya Palestina.2.Wakishiriki zoezi la kuchangia damu. Mzee Chilo na Bakari Makuka wakiwa tayari wanatolewa damu.3. Wasanii wakiongozwa na Davina na Koletha wakiwa kwenye tukio hilo Baadhi ya wasanii wa filamu wakisubiri kuchangia damu katika Hospitali ya Sinza Palestina.4.Msanii,Elizabeth Kilili akiandaliwa kutoa damu na muuguzi wa Hospitali ya Sinza. Msanii, Elizabeth Kilili akiandaliwa kutoa damu na muuguzi wa Hospitali ya Sinza.5.Ummy Mohammed akishiriki kuchangia damu hospitalini hapo. Mmoja wa wasanii waliojitokeza kwenye uchangiaji huo, Ummy Mohammed akiwa kwenye zoezi la kuchangia damu.6.Ummy (kulia) akipata ushauri kabla ya uchangiaji damu. Ummy (kulia) akipata...

 

4 years ago

GPL

STEVE NYERERE: WASANII FEKI WANAICHAFUA BONGO MUVI

Stori: Mayasa Mariwata MWENYEKITI wa Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema kuwa kuna baadhi ya wasanii feki wana tabia chafu zinazoichafua taasisi hiyo, jambo ambalo hawezi kukubaliana nalo. Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ akisisitiza jambo. Akipiga stori na paparazi wetu, kiongozi huyo alisema anashangazwa na wasanii hao wengi wao wakiwa wa kike ambao skendo kwao siyo ishu na...

 

2 years ago

MillardAyo

VIDEO: Oliver Mtukudzi yupo Dar, kayazungumza haya kwa wasanii wa bongo

mtukudhi

Mwanamziki mkongwe wa kimataifa kutoka nchini Zimbabwe Oliver Mtukudzi ambaye aliyetunukiwa tuzo ya tatu iliyobeba heshima ya udaktari kutokana na kuwa mshauri na balozi mzuri wa muziki.  Mwaka 2003 alitunukiwa tuzo kubwa ya heshima na chuo kikuu cha Zimbabwe kwa kutambua miongo kadhaa ya mchango wake na kujitolea katika kujenga muziki na msukumo wa wasanii […]

The post VIDEO: Oliver Mtukudzi yupo Dar, kayazungumza haya kwa wasanii wa bongo appeared first on millardayo.com.

 

2 years ago

Bongo5

Wasanii wa Bongo kukutana Dar leo

20160104202229

Wasanii wa Tanzania Jumanne hii wanakutana jijini Dar es Salaam kuzungumza masuala mbalimbali kuhusu mustakabali wa tasnia yao.

20160104202229

Mkutano huu utafanyika kwenye ukumbi wa Little Theater uliopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Wasanii wote wamealikwa kushiriki.

Jiunge na Bongo5.com sasa Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

 

1 year ago

Bongo Movies

VIDEO: Wasanii ‘Bongo Movie’ Wako Hatarini – JB

Mkongwe wa filamu Jacob Stephen ‘JB’ amefunguka kwamba wasanii wa filamu wapo hatarini kupotea ikiwa hawataweza kwenda sawa na kipindi ambacho tasnia hiyo inapitia kwa sasa.

JB ametoa tahadhari hiyo huku akikanusha hofu iliyopo kwamba tasnia ya movie imekufa ambapo amedai kuwa kuna wasanii wanaoweza kupotea kwenye ramani na kuja wasanii wapya lakini tasnia itaendelea kubaki palepale hivyo mashabiki wasikate tamaa.

Akiwa anabanwa kwa maswali na mashabiki wake jana kwenye kipindi cha...

 

4 years ago

GPL

BONGO MUVI WACHAFUKA!

Na: Gladness Mallya na Imelda Mtema
JAMBO limezua jambo! Baada ya hivi karibuni wasanii wa Bongo Muvi (Movie) kufanya dua kwa ajili ya wenzao waliofariki dunia, baadhi ya ndugu wa marehemu wamecharuka na kudai kuwa waandaaji wa kisomo hicho walifanya kwa manufaa yao binafsi. Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ . Kwa mujibu wa chanzo makini, baadhi ya ndugu wa marehemu wanalalamika kuwa dua hiyo...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani