Wasifu wa Rais wa Tanzania: Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

Mtandao wa  MO BLOG leo Jumamosi ya 4 Machi 2017, wasomaji wetu tunawaletea historia ya Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye yupo madarakani kutoka 05-11-2015  mpaka sasa. (Yaani akitumikia kipindi cha kwanza ambacho kitakuwa cha miaka mitano). Lengo la kuwaletea Makala ya wasifu wa Rais wetu ni baada ya maoni ya watu wengi kutaka hivyo, Wasigu huu umetoka moja kwa moja katika Ikulu ya Rais, na MO BLOG haijaongeza  wala kupunguza neno, Asante (Soma usome hapa chini).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John P. Magufuli alizaliwa  Oktoba 29, 1959 Wilayani Chato Mkoa wa Kagera ambayo hivi sasa ipo Mkoa wa Geita. Dkt. Magufuli amemuoa Mwalimu Janet na wamejaliwa kupata watoto.

Kazi

Mwaka 1982 hadi 1983 alikuwa Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati na  mnamo mwaka 1989 hadi 1995 alikuwa Mkemia wa Chama cha Ushirika cha Nyanza  (Nyanza Cooperative Union Ltd) Mwanza.

Harakati zake za kisiasa zilianza mwaka 1995 alipogombea kiti cha ubunge katika jimbo la Chato na kuteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Ujenzi. Mwaka 2000 Dkt. Magufuli aligombea na kushinda kwa mara ya pili na kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Ujenzi.

Aidha, katika chaguzi za mwaka 2005 na 2010, aliendelea kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Chato na kushinda uchaguzi huo na kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi hadi mwaka 2008 alipohamishiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambayo aliiongoza hadi mwaka 2010. Mwaka 2010 alipochaguliwa tena kuwa mbunge wa Chato aliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi.

Elimu

Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alipata elimu ya msingi  katika shule ya msingi Chato kuanzia mwaka 1967 hadi 1974. Pia alijiunga na elimu ya Sekondari katika shule ya Seminari Katoke-Biharamulo na Lake Sekondari-Mwanza kati ya mwaka 1975 hadi 1978. Aidha, mwaka 1979 hadi 1981 aliendelea na masomo yake ya kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Mkwawa Mkoani Iringa.

Dkt. Magufuli pia alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria akianzia Makutupora, Dodoma (Julai – Desemba 1983), kisha akaenda kambi ya Makuyuni, Arusha (Januari hadi Machi 1984) na akamalizia katika kambi ya Mpwapwa mkoani Dodoma (Machi – Juni 1984). Mwaka 1985 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akisomea Shahada ya Sayansi ya Elimu akibobea kwenye masomo ya Kemia na Hisabati na alihitimu mwaka 1988.

Kati ya mwaka 1991 na 1994 alijiunga na masomo ya Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza na baadaye mwaka 2006-2009 alijiunga na masomo ya Shahada ya Uzamivu ya Kemia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kutokana na taaluma yake  Dkt. Magufuli ameandika vitabu na machapisho mbalimbali.

Chanzo IKULU YA TANZANIA, Unaweza kusoma hapa zaidi:http://www.ikulu.go.tz 

Dewji Blog

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Michuzi

WASIFU WA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI

WASIFU WA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI
MGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI WA CCM

1.0.  MAISHA YAKE
Ndugu John Pombe Joseph Magufuli alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1959 katika kijiji cha Chato, Wilayani Biharamulo katika Mkoa wa Kagera. Hivi sasa Chato ni Wilaya katika Mkoa wa Geita. Ndugu Magufuli ni Daktari wa Falsafa (PhD) ya Kemia. Ana mke  na watoto saba.  Alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba, 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (C.C.M). Aliapishwa na kuanza...

 

2 years ago

Dewji Blog

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akabidhiwa rasmi ofisi na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo Ikulu, Dar

 Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais leo Novemba 12, 2015   Rais Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono kwa furaha na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais   Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Obeni Sefue alipofika Ikulu...

 

2 years ago

Michuzi

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AKUTANA NA MABALOZI IKULU

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Balozi wa Vatican hapa nchini anayemaliza muda wake Francisco Montecillo Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi huyo wa Vatican alifika Ikulu kwa ajili ya kuagana na Rais Dkt. Magufuli mara baada ya kumaliza muda wake ya Ubalozi nchini. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Balozi wa Vatican hapa nchini anayemaliza muda wake nchini Francisco Montecillo.  Rais wa...

 

2 years ago

Michuzi

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI NA WAKUU WA WILAYA WAPYA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI, Mhe George Simbachawene, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe wakiwa na sehemu ya...

 

2 years ago

Michuzi

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AKABIDHIWA RASMI OFISI NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA NNE DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE LEO IKULU, DAR ES SALAAM

 Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais leo Novemba 12, 2015  Rais Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono kwa furaha na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Obeni Sefue alipofika...

 

2 years ago

Michuzi

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AKIONESHA UMAHIRI WAKE WA KUSHONA

 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akionesha umahiri wake wa kutumia Cherahani na kushona nguo za wafanyakazi wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kuvifahamu vitengo mbalimbali na watumishi wake wa  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 20, 2016  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kushona kwa ustadi wa hali ya juuRais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimalizia moja ya nguo za wafanyakazi wa Ikulu.

 

2 years ago

Dewji Blog

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aonesha umahiri wake wa kushona

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akionesha umahiri wake wa kutumia Cherahani na kushona nguo za wafanyakazi wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kuvifahamu vitengo mbalimbali vya Ikulu jijini Dar es salaam Januari 20, 2016

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kushona kwa ustadi wa hali ya juu.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimalizia moja ya nguo za wafanyakazi wa Ikulu.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani