Watiwa mbaroni kwa kumnywesha mtu juisi iliyotiwa dawa za kulevya

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia watu watatu wanaodaiwa kuwa vinara wa kuwawekea watu dawa za kulevya kwenye vinywaji na vyakula katika vyombo vya usafiri.

Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Urich Matei alisema kuwa tukio hilo ni la Novemba 13 mwaka jana katika maeneo ya Chalinze na Morogoro katika moja ya basi la abiria, lililokuwa likitokea Morogoro kwenda Dar es Salaam.

Alitaja watuhumiwa hao kuwa ni Sudi Rutahiwa (32), mkazi wa Mbagala Maji Matitu jijini Dar es Salaam, Aston...

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Bongo5

Arusha: Watu 80 watiwa mbaroni kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya

Jeshi la polisi mkoani Arusha linawashikilia watuhumiwa 80 akiwemo askari moja wa polisi kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya

Aizungumza na wanahabari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema kuwa msako uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu umefanikisha kukamata misokoto 3,845 ya bangi na mirungi Kilogramu 33 pamoja na kete 167.

Alisema, “Katika misako hiyo ambayo ilifanyika wilaya zote sita za mkoa huu, watuhumiwa 54 walipatikana kwenye tuhuma za...

 

2 years ago

Malunde

Makubwa Haya: WAFANYAKAZI WA MOCHWARI DAR WATIWA MBARONI KWA KUMWIBIA MAREHEMU KETE ZA ZA DAWA ZA KULEVYA

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amefunguka kuwa wahudumu wa mochwari ya Mwananyamala wameiba jumla ya kete 32 za dawa za kulevya zilizokuwa kwenye mwili wa Raia wa Ghana aliyefariki dunia akiwa katika nyumba ya wageni.

Kamanda Sirro amesema wahudumu hao wanne wote wamekamatwa na kukiri kwamba baada ya kifo cha raia huyo wa Ghana aliyefariki ndani ya 'Red Carpet' iliyopo Sinza Dar es Salaam walipasua mwili wa raia huyo na kutoa kete hizo kisha kuziuza, na kuongeza...

 

2 years ago

Bongo5

Dawa za Kulevya: Watuhumiwa 11,503 watiwa mbaroni

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema jumla ya watuhumiwa 11,503 wa uzalishaji, usambazaji, uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya wamekamatwa kwa kipindi cha Julai mwaka jana hadi Januari mwaka huu nchini.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Akizungumza Ijumaa hii katika kikao cha Baraza la Mawaziri cha kwanza tangu Serikali kuhamia mjini Dodoma, Majaliwa amesema katika kipindi hicho kesi za kujibu zilikuwa ni 9,811 ambapo watuhumiwa 941 walikutwa na kesi za kujibu huku 238 wakiachiwa huru na kesi...

 

2 years ago

Michuzi

WATUHUMIWA 4,809 WA DAWA ZA KULEVYA WATIWA MBARONI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema katika kipindi cha miezi minne, Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imewakamata watuhumiwa 4,809 na kufungua majalada ya kesi 3,222.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Julai 5, 2017), bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa saba wa Bunge la 11. Bunge limeahirishwa hadi Septemba 5, mwaka huu.
“Katika kipindi kifupi tangu Februari, 2017 Mamlaka hii ilipozinduliwa, imefanikiwa kukamata watuhumiwa 4,809 wakiwa...

 

2 years ago

Channelten

Watuhumiwa 257 watiwa mbaroni, dawa za kulevya zakamatwa

Jeshi la Polisi kanda maalum dsm limewatia mbaroni watuhumiwa 257 pamoja na kete 1526 katika siku mbili zilizopita katika msako mkali wa kupambana na watu wanajihusisha na uuzaji, utumiaji na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Kamanda wa Polisi kanda maalum dsm Kamishna simon Siro akizungumza na waandishi wa habari amesema dawa hizo za kulevya zilizokamatwa ni aina ya Heroin ambapo pia watu hao wamekamatwa na misokoto ya bangi 247 viroba vitatu vya bangi pamoja na lita 372 ya pombe haramu ya...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Watatu watiwa mbaroni kwakukutwa na Dawa za kulevya Unguja

Jeshi là polisi Mkoa wa Kusini Unguja jana 12 February 2018 limewashikilia vijana watatu, wawili waakazi wa paje Mkoa wa Kusini Unguja na mmoja  mkaazi wa Kwarara Wilaya ya Mgharib B Unguja wakiwa na kete za Dawa za kulevya kwa nyakati tofauti. Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Kusini unguja Kamishna msaidizi Makarani Khamis Ahmed amesema kuwa mkaazi wa kwarara amekutwa akiwa na kete za dawa za kulevya 432 pamoja na vijana wawili waakazi paje wakiwa na kete...

 

2 years ago

Malunde

ASKARI POLISI WANNE WALEVI WATIWA MBARONI KWA KUFYATUA OVYO RISASI NA KUJERUHI MTU MWANZA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ahmed Msangi ametoa amri kukamatwa kwa askari polisi wanne wa Kituo Kikuu cha Polisi Nyamagana kutokana na asakri hao kumjeruhi kwa risasi mke wa Mwenyekiti mtaa.
Kamanda Msangi amesema polisi hao tayari wametiwa mbaroni kwa kumjeruhi kwa risasi mguuni Bi. Editha Ntobi ambaye ni mke wa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Majengo Mapya uliopo katika Kata ya Mabatini jijini Mwanza.
Msangi amesema polisi hao wanatuhumiwa...

 

5 years ago

Tanzania Daima

Mlemavu mbaroni kwa dawa za kulevya

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linamshikilia Said Tidwa (36), mkazi wa Vijibweni, Temeke kwa tuhuma za kufanya biashara ya dawa za kulevya. Akizungumza na waandishi wa...

 

3 years ago

Mtanzania

Mbaroni kwa mtandao wa dawa za kulevya

siroASIFIWE GEORGE NA MARTHA LUKUMAY, DAR ES SALAAM

JESHI la Polis Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kujihusisha na mtandao wa kuuza dawa za kulevya, huku wakiendelea kumuhoji mtuhumiwa mwingine kwa tuhuma hizo hizo.

Akizungumza jijini hapa jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna Simon Sirro, alisema watuhumiwa hao ni miongoni mwa wauza dawa wazoefu na walitarajiwa kufikishwa mahakamani jana kujibu mashtaka...

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani