Watiwa mtegoni waliomuhusisha Ofisa Polisi na tukio la Lissu

Msemaji wa Jeshi hilo Barnabas Mwakalukwa.

Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi kuwabaini waliohusika kusambaza taarifa zinazodai ofisa wa polisi kuhusishwa katika tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa risasi kwa Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, Septemba 7, mwaka huu.

Sambamba na uchunguzi huo, jeshi hilo limewataka wananchi kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya na badala yake itumike kuelimisha na kuhabarisha jamii juu ya masuala ya maendeeleo.

Msemaji wa Jeshi hilo, Barnabas Mwakalukwa, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam ikiwa siku chache baada ya kutolewa kwa taarifa za ofisa huyo, akidaiwa kuonekana akifanya ukachero Nairobi nchini Kenya, ambako Lissu anapatiwa matibabu.

Mwakalukwa alisema taarifa hizo zilizoenezwa kuanzia juzi ni za uongo na zenye lengo la kumharibia ofisa huyo na jeshi kwa ujumla na kwamba hayuko Nairobi kama ilivyoelezwa.

“Kuhusu safari ya Nairobi, askari huyo alikuwa nchini Kenya kwa mafunzo kuanzia Septemba 4 hadi 8, mwaka huu, aliporejea nchini wakati Lissu alipatwa na mkasa huo Septemba 7 na kufika Septemba 8 alfajiri  mjini Nairobi,” alisema.

“Suala la Lissu liko chini ya uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na hatimaye kuwafikisha mahakamani. Ni vyema wananchi na wanasiasa wakaliacha jeshi la polisi lifanye kazi yake bila kuliingilia na kupata ukweli wa jambo hili.”

Aidha, Mwakalukwa aliwatahadharisha wananchi kuwa jeshi hilo kupitia kitengo cha upelelezi wa makosa ya mitandao, linaendelea na uchunguzi wake ili kuwabaini wote waliohusika kusambaza taarifa hizo za uongo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

The post Watiwa mtegoni waliomuhusisha Ofisa Polisi na tukio la Lissu appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

2 weeks ago

Malunde

KAULI YA JESHI LA POLISI KUHUSU TUKIO LA TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amezungumzia tukio la kupigwa risasi mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, akiwaomba wananchi wenye taarifa kulisaidia jeshi hilo.

Muroto amesema leo Alhamisi kuwa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na wameshafika eneo la tukio nyumbani kwa Lissu.
“Tunaomba mwananchi wenye taarifa atusaidie. Jeshi la Polisi tumeanza uchunguzi, tumefika eneo la tukio na tunaendelea,” amesema.
Kamanda Muroto amesema taarifa za awali zinaonyesha kuna gari...

 

2 weeks ago

Michuzi

JESHI LA POLISI MAKAO MAKUU LAUNDA TIMU YA KUPELELEZA TUKIO LA TUNDU LISSU.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kutangaza kuwa Jeshi la Polisi  limeunda Timu maalum kwaajili ya kuchunguza na kufuatilia tukio la kushambuliwa kwa risasi hapo jana Mkoani Dodoma nyumbani.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JESHI la Polisi  Makao Makuu  imeunda timu ya upelelezi ya kufatilia tukio la kushambuliwa kwa risasi  kwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

 

3 years ago

Michuzi

Wawili watiwa mbaroni katika tukio la Ujambazi,Darajani Zanzibar mchana wa leo

Watuhumiwa wawili katika tukio la Ujambazi lililotokea Mchana wa leo eneo la Darajani Jua Kali,Zanzibar wametiwa mbaroni baada ya kuzidiwa nguvu na wananchi wenye hasira wakati walipokuwa wakiwakimbia Polisi.

Inadaiwa kuwa watuhumiwa hao walikua watatu na walitaka kuiba katika maduka na mawakala wa huduma za pesa yaliyopo eneo la Mnazi,baada ya kushtukiwa walikimbia na kufukuzana na Polisi hadi katika maeneo ya Darajani ndipo wananchi kwa kushirikiana na polisi wakawadhibiti na...

 

1 year ago

Michuzi

BREAKING NYUZZZZ.....: WATU WAWILI WATIWA MBARONI KWA TUKIO LA UJAMBAZI KARIAKOO MCHANA HUU

 Watuhumiwa wa Tukio la Ujambazi, wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi mara baada ya kukamatwa mchana huu katika eneo la Kariakoo, Jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Umati wa watu wakishuhudia tukio la kukamatwa kwa Watuhumiwa hao wa tukio la Ujambazi.Taarifa kamili itakujia baadae kidogo.

 

2 weeks ago

Bongo Movies

Rais Magufuli atoa tamko tukio la Lissu

Rais John Magufuli amesikitishwa na taarifa alizozipata tukio la kupigwa kwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiwa nyumbani kwake Dodoma leo na kuviagiza vyombo vya dola viwasake waliyofanya uhalifu huo.

Rais Magufuli amesema hayo kupitia ukurasa wake wa twitter jioni ya leo na kutaka vyombo vya usalama kuwatafuta watu waliofanya tukio hilo la kinyama.

“Nimepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mh.Tundu Lissu, namuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka....

 

2 weeks ago

CHADEMA Blog

PICHA ZA TUKIO LA KUPIGWA RISASI GARI LA MHE TUNDU LISSU

Gari la Tundu Lissu lililopigwa risasi na kumjeruhi Picha za matundu ya risasi zilizoshambulia gari la Tundu Lissu na kumjeruhi Dereva wa Tundu Lissu aliyeshika nguo na viatu baada ya tukio la kushambuliwa kwa risasi gari ya mheshimiwa Tundu Lissu Mwenyekiti wa chadema mheshimiwa Freeman Mbowe akiwa na dereva wa Tundu Lissu

 

2 weeks ago

Zanzibar 24

IGP Sirro azungumzia tukio la kushambuliwa kwa Tundu Lissu

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha kuwatia mbaroni wahalifu waliohusika kumshambulia kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

IGP Sirro ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kudai usalama wa nchi upo vizuri na jeshi la polisi limeongeza nguvu ya upelelezi mjini Dodoma ili kuhakikisha linawapata watu ambao wamefanya uhalifu wa kumpiga risasi mbunge Tundu Lissu , huku akiwataka...

 

2 weeks ago

Channelten

Kushambuliwa kwa Mbunge Tundu Lissu, Chadema walaani tukio hilo

CHADEMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema hali ya mwanasheria mkuu wa chama hicho ambae pia Rais wa chama cha mawakili Tanganyika TLS TUNDU LISSU inaendelea vizuri akiwa anapatiwa matibabu mjini Nairobi Kenya.

Bwana Tundu Lissu alishambuliwa jana na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake eneo la Area D mjini Dodoma ambapo inaelezewa kuwa takribani risasi tano zilimpata mwilini mwake na kulazimika kufikisha hospitali ya mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu ya awali.

Akizungumza na...

 

3 years ago

GPL

POLISI FEKI WATIWA MBARONI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi akiwaonyesha maaskari  feki ambao walikuwa wakifanya utapeli katika mikoa ya Iringa na Morogoro. Kulia ni Brazil Nyakunga ambaye ni mwalimu akiwa na sare za polisi na katikati ni bosi wake Goodluck Mbehale.
Askari Polisi mkoani Iringa (kushoto) akiwa na maaskari  feki katika ofisi…

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani