Waziri aahidi mashine ya kusagia Mwani kwa Wakulima

Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Hamad Rashid Mohammed amesema  serikali itazidisha juhudi katika kulisimamia zao la mwani ili liweze kutoa tija  kwa wakulima wazao hilo.

 

Akizungumza na Zanzibar24  kufuatia malalamiko ya wakulima  kuwa na  bei ndogo ya zao hilo   na tatizo la mashine za  kusagia mwani kuwa wa unga ili  kutengeneza bidhaa amesema  kwasasa bei ya mwani inashuka  kutokana na  kuuzwa nje ya nchi lakini  ili kuwarahisishia  wakulima  watawapatia  mashine za kusagia  mwani ambazo  zitasaidia  kuondokana na  tatizo hilo.

 

Amesema kwa  sasa wameshaweka mashine  mbili kwa upande  wa unguja na mbili wanatarajia  kupeleka  pemba  ili kurahisisha  upatikanaji wa unga  wa mwani  ambao   unauzwa  kwa bei ghali.

 

Aidha amewataka wakulima  kuongeza jitihada  juu ya kilimo hicho  kwani serikali inaendeleza kila juhudi  za kuhakikisha  zao hilo  linawanufaisha  wakulima  kutokana na umuhimu wake  katika matumizi mbalimbali ya  binadamu.

Kilimo cha mwani  kimewaajiri wanawake wengi kwa kiasi kikubwa ambapo  watu  Ishirini na tatu elfu  tayari wamejiajiri  kupitia  kilimo hicho kwa unguja na pemba.

Amina Omar Zanzibar24

The post Waziri aahidi mashine ya kusagia Mwani kwa Wakulima appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

7 months ago

Michuzi

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR ATEMBELE MASHINE MPYA ZA KUSAGIA TAKATAKA ZA HOSPITALI

Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo amesema tatizo la kuharibika kwa mashine ya kusagia taka katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja siku za karibuni kulipelekea kurundikana kwa taka na kusababisha usumbufu kwa wananchi.
Amesema baadhi ya wafanyakazi wakorofi wa Hospitali hiyo walitumia kasoro hiyo kuzitupa taka kwenye ufukwe wa bahari, nyuma ya Hospitali, ambapo ni kosa kwa mujibu wa sheria na kanuni za afya na uhifadhi wa mazingira.
Waziri Mahmoud ametoa kauli...

 

7 months ago

Zanzibar 24

Waziri wa Afya Zanzibar atembelea mashine mpya za kusagia takataka za hospitali

Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo amesema tatizo la kuharibika kwa mashine ya kusagia taka katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja siku za karibuni kulipelekea kurundikana kwa taka na kusababisha usumbufu kwa wananchi.

Amesema baadhi ya wafanyakazi wakorofi wa Hospitali hiyo walitumia kasoro hiyo kuzitupa taka kwenye ufukwe wa bahari, nyuma ya Hospitali, ambapo ni kosa kwa mujibu wa sheria na kanuni za afya na uhifadhi wa mazingira.

Waziri Mahmoud ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Waziri wa kilimo Zanzibar amefungua Semina ya siku moja kwa wakulima wa mwani

Waziri wa kilimo maliasili, mifugo na uvuvi, Mhe Hamadi Rashid Mohamed ameungua semina ya siku moja kwa wakulima wa Zao la mwani huko katika ukumbi wa hoteli ya Visitors INN Jambiani Mkoa wa kusini Unguja.

Semina hiyo imelenga kutoa mafunzo kwa wakulima wa mwani juu ya utunzaji wa zao hilo

img-20161022-wa0005

img-20161022-wa0006

The post Waziri wa kilimo Zanzibar amefungua Semina ya siku moja kwa wakulima wa mwani appeared first on Zanzibar24.

 

1 year ago

Zanzibar 24

Waziri wa Kilimo Zanzibar awataka wakulima wa mwani kuzalisha bidhaa la zao hilo

Waziri wa Kilimo Mifugo, Maliasili na Uvuvi Zanzibar Hamad Rashid Muhammed  amesema endapo Wakulima wa Zao la mwani watajikusanya pamoja katika kuzalisha bidhaa la zao itawasaidia kuondoa tatizo la  umaskini.

Akizungumza na wadau wa maendeleo na Wakulima wa zao hilo huko Jambiani amesema zao la mwani ni zao linalotumika kwa matumzi mbalimbali si vyema kwa wakulima wa zao hilo kutegemea serikali kulinunua badala yake walitumie katika kutengezea bidhaa.

Aidha amesema serikali  kwa kushirikiana...

 

3 years ago

Michuzi

Dkt. Shein akabidhi Vihori kwa wakulima wa mwani,Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mwakilishi wa VSO Tanzania Jean Van Wetter wakati alipowasili katika viwanja vya Ukimbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo katika hafla ya sherehe ya kukabidhi Vihori kwa wakulima wa Mwani.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia bidhaa mbali mbali zilizotengenezwa kwa kutumia zao la mwani na kikundi cha Ulezi ni Kazi cha shehia ya Fujoni Jimbo la...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Zifa yaandaa ziara ya mafunzo ya kusanifu mwani kwa wakulima wa chwaka

Chuo cha Uongozi wa fedha Zanzibar (ZIFA) kiliandaa ziara ya siku moja ya mafunzo kwa wakulima wa mwani wa Chwaka kutembelea kikikundi cha Ushirika cha Tusife Moyo cha Kijiji cha Kidoti ambacho kimepiga hatua kubwa katika kusanifu zao hilo kwa ajili ya matumizi mbali mbali.

Ziara hiyo  ni moja ya juhudi zinazochukuliwa na chuo katika azma  yake ya  kusaidia jamii kufikia maendeleo  endelevu ya kiuchumi na ustawi wa jamii.

Mhadhiri wa ZIFA Maalim Said  Mohd Khamis alisema kwa mujibu wa...

 

12 months ago

Zanzibar 24

Wakulima wa Mwani epukeni udanyifu

WAKULIMA wa zao la mwani  Kisiwani  Pemba wametakiwa kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwa kuchanganya  takataka , majani pamoja na mchanga katika magunia ya mwani ili kuongeza uzito wakati wanapokwenda kuuza mwani wao .

Akizungumza na wakulima wa zao hilo wa  mikoa miwili ya Pemba katika Ukumbi wa mikutano wa kilimo Weni , Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Mussa Aboud Jumbe amesema kuwa kitendo hicho kimechangia kushuka kwa bei ya zao hilo .

Amesema kuwa wapo baadhi ya wakulima...

 

4 years ago

Habarileo

FAO yawapiga jeki wakulima wa mwani

SHIRIKA la Chakula na Kilimo (FAO) limeweka mikakati kuhakikisha wakulima wa zao la mwani wanapiga hatua kubwa na kuongeza mapato na kuondokana na umasikini wa kipato.

 

12 months ago

Zanzibar 24

Wakulima wa mwani Zanzibar kutafutiwa faraja

Wizara ya Kilimo ,Mali asili,Mifugo na Uvuvi Zanzibar imesema inaendelea na hatua ya kulipatia ufumbuzi tatizo la Bei ya zao la Mwani ili liweze kunufaisha wakulima wa zao hilo.

Akijibu swali kwa Niaba ya Waziri wa wizara hiyo katika kikao cha baraza la Wawakilishi huko Chukwani Naibu Waziri wa Kilimo ,Mali asili,Mifugo na Uvuvi Zanzibar Lulu Msham Abdallah amesema mbali na elimu ya Uhamasishaji wa kilimo cha zao hilo kutolewa kwa wananchi pia serikali inaendelea na juhudi za kutafuta...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani