WAZIRI LUKUVI: SERIKALI IMEDHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

Na Said Mwishehe, Globu ya jamiiWAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kumaliza changamoto ya migogoro ya ardhi nchini. 
Lukuvi ametoa kauli hiyo wakati anazungumza na Globu ya jamii ambapo amefafanua kuna jitihada na mikakati mbalimbali inafanya kutatua migogoro ya ardhi. 
Amesema migogoro ambayo wizara yake inatafuta ufumbuzi mingi ni ile ya kuanzia mwaka 2015 kurudi nyuma kwani tangu Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani hakuna mgogoro wa ardhi. 
"Kwa sehemu kubwa mimi na wasaidizi wangu tunakwenda vizuri katika kuhakikisha tunamaliza migogoro ya ardhi kama ambavyo dhamira ya Serikali hii inavyotaka. 
"Migogoro mingi imeshughulikiwa na hata iliyokuwepo ilitokana na kutoshughulikiwa kwa wakati.Baadhi ya watendaji hawakuwa  wakichukua hatua kwa haraka. 
"Kwa sasa wizarani wanajua nataka nini na ndio maana tunakwenda vizuri maana hatutaki kutumia muda mwingi kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa ardhi,"amesema Lukuvi. 
Ameongeza kwa kutambua namna ya utendaji kazi wa baadhi ya maofisa wake ndio maana anatumia mfumo wa kuita wananchi wenye matatizo ya ardhi na kisha kutafuta ufumbuzi wake tena hadharani. 
Waziri Lukuvi amesema kwa mwenendo wanaokwenda nao anaamini Serikali ya awamu ya tano itafika mahali hakutakuwa na migogoro mingi ya ardhi. 
Akizungumzia migogoro ya ardhi kwa Jiji la Dar es Salaam, Lukuvi amesema kwa siku tatu ambazo amekuwa akitatua migogoro ya ardhi kwa wale waliofika wizarani ameipatia ufumbuzi.
Amesema migogoro ya ardhi ambayo hajaishughulikia ni ile ambayo kesi zipo mahakamani kwani wizara yake haina uwezo wa kuingilia uamuzi wa mahakama. 
Alipoulizwa iwapo migogoro ya ardhi kwa Dar es Salaam ipo siku itakwisha, amejibu ana uhakika wa kuimaliza. 
"Kwa hali ilivyo itafika wakati hata tukiita watu wenye migogoro ya ardhi waje tuitatue hawatakuwepo maana tunakwenda vizuri katika kuishughulikia,"amesema.Amefafanua kwa sasa atakuwa na ratiba katika wilaya mbalimbali ambapo atakwenda kwa ajili ya kushughulikia migogoro ya ardhi. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Dar es Salaam aliyefika katika wizara hiyo wakati anasikiliza wenye migogoro ya ardhi jana.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Michuzi

WAZIRI LUKUVI: SERIKALI TUMEDHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

Na Sheila Simba- MAELEZO


Waziri wa Aridhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa Serikali imeanza kazi ya kupima ardhi  nchi nzima kuanzia mkoani Morogoro.
Akizungumza  katika kipindi kipya cha "TUNATEKELEZA" kinachoandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO na TBC1 ,alisema utekelezaji wa zoezi hilo umeanzia mkoani humo ili kupima maeneo ya wakulima na wafugaji na kutatua migogoro ya ardhi Mkoani humo.
“Serikali tumedhamiria kumaliza migogoro ya ardhi, kutimiza ndoto ya Rais...

 

1 year ago

Michuzi

SERIKALI MKOANI SIMIYU IMEDHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

Na Stella Kalinga, SimiyuSerikali  Mkoani  Simiyu imedhamiria kwa mwaka 2017 kutatua na kuondoa migogoro yote  ya  ardhi ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara kwa wananchi wa mkoa huo.
Akitoa ufafanuzi wa namna ya  kutatua kero hiyo wakati wa mkutano wake na wananchi wa jimbo la  Meatu ,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka alisema kuwa amechoshwa kusikia na kuona migogoro ya ardhi  inayojitokeza ndani ya mkoa wake, hivyo mwaka 2017 ndio utakuwa mwisho wa kero hizo.
Mtaka amesema kuwa kamwe...

 

2 years ago

Dewji Blog

Waziri Lukuvi aeleza jinsi serikali imevyojipanga kumaliza migogoro ya ardhi

Waziri wa Aridhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa Serikali imeanza kazi ya kupima ardhi nchi nzima kuanzia mkoani Morogoro.

Akizungumza katika kipindi kipya cha “TUNATEKELEZA” kinachoandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO na TBC1 ,alisema utekelezaji wa zoezi hilo umeanzia mkoani humo ili kupima maeneo ya wakulima na wafugaji na kutatua migogoro ya ardhi Mkoani humo.

“Serikali tumedhamiria kumaliza migogoro ya ardhi, kutimiza ndoto ya Rais Magufuli ya kuondokana na...

 

2 years ago

Michuzi

WAZIRI LUKUVI AWAONYA MADALALI WA ARDHI, AFANYA ZIARA KIBAHA ADHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi akikagua mafaili ya hati za ardhi za wananchi yanayodaiwa kukaa kwenye shelvu kwa zaidi ya miaka mitatu pasipo kufikishwa kwa wahusika. Anayempa maelezo ni Afisa Ardhi Mteule, Majaliwa Jaffari.  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi akikagua mafaili ya hati za ardhi za wananchi yanayodaiwa kukaa kwenye shelvu kwa zaidi ya miaka mitatu pasipo kufikishwa kwa wahusika. Anayempa maelezo ni Afisa Ardhi Mteule,...

 

1 year ago

Ippmedia

Waziri Mh. Lukuvi atoa mwezi mmoja kwa viongozi wa serikali kutatua migogoro ya ardhi nchini.

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh. William Lukuvi ametoa muda wa mwezi mmoja kwa viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa wawe wametataua migogogo ya ardhi katika maeneo yao kutokana na wao kuhusika katika ugawaji na upangaji wa maeneo uliozua migogoro.

Day n Time: Jumanne Saa 2:00 UsikuStation: ITV

 

3 years ago

Dewji Blog

Mh. Lukuvi aagiza uongozi wa mkoa wa Manyara kumaliza migogoro ya ardhi kabla ya mwezi Mei mwaka huu

1aMkuu wa mkoa wa Manyara ,Mhe.Joel Nkaya Bendera akizungumza katika kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa huo kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati, kushoto ni Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Babati, Crispin Meela.Mhe.Bendera amesisitiza nidhamu ya kazi katika kuhudumia wananchi na ameapa kuwaondoa watendaji wabovu mkoani humo.

2aWaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.William Lukuvi akizungumza katika...

 

3 years ago

Vijimambo

WAZIRI WA ARDHI WILLIAM LUKUVI AFANYA ZIARA MKOANI IRINGA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akiongea na wananchi waliojitokeza kuwasilisha kero zao katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mkoani Iringa. Alisisitiza kuwa Mkoa wa Iringa uharakishe kupima ardhi ya wananchi ili kupunguza migogoro ya ardhi. Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkoa wa Iringa wakimsikiliza Waziri Lukuvi aliposikiliza kero zao katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo Manispaa ya Iringa.


...

 

9 months ago

Michuzi

WAZIRI LUKUVI AKESHA AKISHUGHULIKIA MIGOGORO YA ARDHI.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ajikuta akikesha ofisini kwake pamoja na wananchi takriban 189 wenye Matatizo na Kero za ardhi.
Mhe. Waziri ametumia takriban saa 20 kusikiliza kero za wananchi ambao waligoma kuondoka ofisini kwake hadi kero zao zitakapopatiwa ufumbuzi. Kazi hiyo ilianza majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 9 usiku.
Hata hivyo wananchi walilazimika kulala Wizarani wakisubiri kuonana na Waziri kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya wananchi...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani