WAZIRI MKUU AENDA KUTOA POLE NYUMBANI KWA DK. MWAKYEMBE, RAIS JPM ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo,alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Mke wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe, aliyefariki katika Hospitali ya Agakhan leo alfajiri. Julai 16, 2017. Mke wa Waziri Mkuu Kassim Mary Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo,alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Mke wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe, aliyefariki katika Hospitali ya Agakhan leo alfajiri. Julai 16, 2017. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akizungumza na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Mke wa Dr. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe, aliyefariki katika Hospitali ya Agakhan leo alfajiri. Julai 16, 2017. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimkabidhi mchango wa rambirambi Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe,alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Mke wa Dr. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe, aliyefariki katika Hospitali ya Agakhan leo alfajiri. Julai 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)-------------------------------------------------------------------
RAIS DK. MAGUFULI ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBIRais Dk. John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison George Mwakyembe kufuatia kifo cha mkewe Linah George Mwakyembe kilichotokea usiku wa tarehe 15 Julai, 2017.
Linah George Mwakyembe amefariki dunia katika hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.


Taarifa iliyotolewa na Ikulu jjini Dar es Salaam, leo imesema, katika salamu hizo, Rais Magufuli ameelezea kushtushwa na kusikitishwa na kifo hicho, na amesema yeye na familia yake wanaungana na familia ya Dk. Mwakyembe katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.


“Nakupa pole sana Dk. Mwakyembe kwa kuondokewa na mkeo mpendwa Bi. Linah, natambua hisia za maumivu ulizonazo wewe na familia nzima, nyote nawaombea Mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.


Namuombea Marehemu Linah George Mwakyembe apumzishwe mahali pema peponi, Amina” Taarifa hiyo imemkariri Rais Magufuli akisema.

CCM Blog

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Michuzi

RAIS DKT. MAGUFULI ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA TANGA.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mama Mwantumu Mahiza, kufuatia vifo vya watu 11 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyosababishwa na Basi la Kampuni ya Simbamtoto kugongana uso kwa uso na Lori lililobeba mchanga katika eneo la Pandamlima, Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga.


Ajali hiyo imetokeo leo tarehe 11 Februari, 2016 majira ya saa 1:15 asubuhi katika...

 

10 months ago

CCM Blog

RAIS DK MAGUFULI ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA MKURUGENZI MKUU AfDB

DAR ES SALAAM, TANZANIA
Rais Dk. John Magufuli ametuma salam za rambirambi kufuatia kifo cha Mkurugezi Mkuu wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Dk. Tonia Kandiero.

“Kwa mshituko na masikitiko makubwa nimepokea taarifa za kifo cha Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Kanda ya Afrika Kusini Dk. Tonia Kandiero aliyefariki dunia ghafla jana usiku tarehe 28 Juni, 2017 akiwa ofisini kwake huko Pretoria Afrika Kusini”

Hii ni kauli ya Dk. John Magufuli aliyoitoa leo, Ikulu...

 

2 years ago

Michuzi

WAZIRI NAPE ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA ALIEKUWA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE, MAREHEMU SARA DUMBA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye ametuma salamu za rambirambi kwa  wanahabari wote kufuatia kifo cha ghafla cha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe na  Mtangazaji Mwandamizi wa zamani wa Redio Tanzania (RTD), Dar es salaam  Marehemu Sara Dumba.
“Pokeeni salamu za rambirambi zangu za dhati kwa kuondokewa na  Mwanahabari  mahiri Bi. Sara Dumba aliyekuwa mfano wa kuigwa” amesema Mhe. Nape.
“Mbali na utangazaji wake mahiri, Bi. Sara Dumba alikuwa mzalendo wa kweli...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Waziri Nape atuma Salam za rambirambi kwa familia ya Mchezaji aliyefariki uwanjani

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, Jumatatu hii ametoa salamu za rambirambi kwa wanafamilia Wa Ismail Khalfan mchezaji wa Mbao FC chini ya umri wa miaka 20, ambaye alipoteza maisha katika mchezo wa mwisho wa round ya 7 kundi A kituo cha Kaitaba, Bukoba.

Ismail Khalfan ambaye alikuwa anavaa jezi namba 4 katika mashindano hayo, ndiye aliyefunga goli la kwanza la Mbao FC dhidi ya Mwadui FC katika ushindi wa magoli 2-0.

Hii ni taarifa kutoka wizara ya habari na...

 

3 years ago

Vijimambo

MWENYEKITI WA TAWI LA CCM NY BWANA SELF AKIDA AENDA KUTOA POLE NYUMBANI KWA BWANA KIBODYA.


Nyumbani kwa Bwana Isaac Kibondya akiongea na watu walioenda kumpa pole nyumbani kwake baada ya kufiwa na mkwe wake, Kifo kimetokea huko Tanzania siku ya Tarehe July, 16. Marehemu ni mzazi wa Mke wa Bwana Kibodya na Kama inakumbukwa wote walikuwa Tanzania kumuona marehemu akiwa anaumwa mwezi uliopita.
Mwenyekiti wa tawi la CCM New York bwana Seif Akida pamoja na Ny Ebra wote kutoka New York wakiwa nyumbani kwa bwana Kibodya Vail, Springfield. MA kutoa pole.
 

3 years ago

Michuzi

RAIS KIKWETE ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KWA RAIS WA CHINA KUFUATIA VIFO VYA WACHINA 400 KATIKA AJALI YA BOTI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Xi Jinping kuombeleza vifo vya zaidi ya watu 400 ambao wamepoteza maisha yao katika ajali ya boti ya kitalii, iliyozama katika Mto wa Yangtze mwanzoni mwa wiki hii.
Meli ya kitalii ya Eastern Star ilizama katika Mto wa Yangtze, karibu na mji wa Jianli, Jimbo la Kati la Hubei, Jumatatu usiku ikiwa na abiria 456 waliokuwa wanafanya safari ya...

 

2 years ago

Zanzibar 24

Rais wa Zanzibar atuma salam za rambirambi kufuatia tetemeko la Ardhi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo na maafa mengine vilivyotokana na tetemeko la ardhi lililotokea jana Septemba 10, 2016 majira ya laasiri katika Mkoa wa Kagera pamoja na maeneo mengine ya jirani.

Kufuatia tukio hilo Rais wa Zanzibar anaungana na familia zote zilizopoteza ndugu, jamaa na marafiki na anawaombea marehemu wapumzishwe mahala pema  panapostahiki na awape subira ndugu, jamaa na marafiki wa...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani