WAZIRI MKUU AKEMEA MADUDU USHIRIKA MBINGA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mbinga Mjini, kwenye mkutano wa hadhara aliyouitisha kwenye Uwanja wa Michezo Mbinga Mjini Wilayani Songea, Mkoani Ruvuma. Januari 5, 2018.
*Aagiza uchunguzi ufanyike kuanzia leo, maafisa wa MBICU, MBIFACU kikaangoni*Apiga marufuku ununuzi wa kahawa kwa mfumo wa MAGOMA*Aitisha kikao cha wadau wa kahawa Dodoma Jan. 14
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amebaini madudu kwenye Vyama Vikuu vya Ushirika vya Mbinga (MBICU na MBIFACU) na kuagiza uchunguzi ufanyike kuanzia leo.
“Nikiondoka hapa jukwaani, viongozi wote wa zamani na wa sasa waripoti kwa Mkuu wa Wilaya, na OCD hakikisha ofisi za chama hazifunguliwi hadi kesho asubuhi (leo) kazi itakapoanza, ili wasije kubadilisha nyaraka kwenye ofisi yao. Timu yangu ya uchunguzi iko hapa Mbinga, kesho waende wote kwenye ofisi hizo,” alisema huku akishangiliwa na wananchi.
Ametoa agizo hilo jana jioni (Ijumaa, Januari 5, 2018) wakati akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mbinga, kwenye viwanja vya CCM, mjini Mbinga.
“Natambua kuwa MBICU ilishakufa ikiwa na madeni makubwa na mkaunda tena MBIFACU, ambayo nayo inasuasua, lakini viongozi wote hawa watafutwe, waje waonane wa timu  yangu na waeleze fedha za chama zimeenda wapi na kama walizikopea zilifanya nini,” alisisitiza.
Alisema timu hiyo ya uchunguzi itakiangalia chama hicho na kukifumua chote, na wote wakaobainika kuhusika watachukuliwa hatua za kinidhamu. “Tunataka MBICU na madeni yenu yaliyoko kwa Msajili wa HAZINA yajulikane, tunataka turudishe hoteli yetu, mashamba yetu na majengo yetu,” alisema.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Channelten

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Kilimo na Ushirika kuifanyia marekebisho Bodi ya Korosho

majaliwa

Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Kilimo na Ushirika Charles Tizeba kuifanyia marekebisho Bodi ya Korosho Tanzania kutokana na kushindwa kulisimamia zao hilo kikamilifu.

Waziri Mkuu Majaliwa amebainisha kwamba Bodi ya Korosho Tanzania inaonekana kuingilia kazi za minada ya korosho na kuzuia wafanyabiashara  wengine wasiweze kununua zao hilo, hali inayoonyesha wazi kuwa kuna wafanyabiashara  waliopangwa kununua koroshoo bila ya kufuata utaratibu.

Akihutubia  mkutano wa...

 

1 year ago

Michuzi

WAZIRI MKUU AKEMEA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Aonya wanaokata miti ovyo, asisitiza utunzaji wa vyanzo vya maji
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaonya wakazi wa Ruangwa wanaokata miti kwenye misitu waache kufanya hivyo mara moja ili kuokoa ardhi chepechepe waliyokuwa nayo.
Amesema ukataji miti huo unafanywa zaidi na watu wanaoanzisha mashamba ya ufuta na wapo walioamua kulima karibu na vyanzo vya maji hali iliyosababisha maji yakauke kwenye maeneo mengi.
“Zamani kuna maeneo ulikuwa haupiti hadi ukunje suruali, na kama una gari napo pia...

 

1 year ago

Dewji Blog

Waziri Mkuu achoshwa na madudu bodi ya korosho

*Aagiza ifanyiwe marekebisho makubwa

*Aishangaa kung’ang’ania minada

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba kuifanyia marekebisho makubwa Bodi ya Korosho na menejimenti yake  baada ya kushindwa kusimamia zao hilo ipasavyo.

Amesema Serikali itafanya mapitio ya bodi zote za mazao ya biashara na imeanza na zao la korosho kisha zao la pamba, tumbaku, kahawa, katani na chai. Katika tathmini na mapitio hayo , bodi itakayobainika kushindwa...

 

1 year ago

Michuzi

WAZIRI MKUU ANUSA MADUDU MRADI WA NGAKA

*Aahidi kutuma Gavana, CAG, Msajili wa Hazina kufanya ukaguzi*Asema Serikali haitaruhusu uagizaji wa makaa hayo kutoka nje ya nchi*Autaka uongozi wa kampuni uimarishe teknolojia ili kuongeza uzalushaji
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa atamtuma mara moja Msajili wa Hazina aende kufanya uchunguzi wa kina na wa kijinai (forensic investigation) ili kijiridhisha kama mapato na matumizi ya kampuni ya TANCOAL ni halali.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Januari 6, 2017) mara baada baada ya kupokea...

 

12 months ago

Michuzi

WAZIRI MKUU ANUSA MADUDU MINADA YA MADINI

*Amuagiza Kamishna wa Madini aende Mererani WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema anafuatilia kwa makini minada ya madini inayofanyika nchini kwa sababu anazo taarifa za kukiukwa utaratibu kwenye minada hiyo.
Amesema ukiukwaji huo unachangia kutobadilika kwa mapato ya mauzo yatokanayo na mnada hata kama kuna vito viliyokakatwa au havijakatwa.
Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumatatu, Februari 27, 2017) wakati akihitimisha kikao alichokiitisha kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam...

 

6 months ago

Michuzi

WAZIRI MKUU AKEMEA MATUKIO YA UHALIFU ULYANKULU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi wanaoishi kwenye makazi ya wakimbizi ya Ulyankulu waache kujihusisha na matukio ya uhalifu.
Ametoa onyo hilo leo mchana (Ijumaa, Agosti 11, 2017) wakati akiwahutubia mamia ya wakazi wa tarafa ya Ulyankulu katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya VETA, wilayani Kaliua mkoani Tabora.
Amesema matukio ya ujambazi, mauaji na umiliki wa silaha yanayofanyika kwenye tarafa hiyo ni mengi ikilinganishwa hali ilivyo kwenye maeneo mengine ya...

 

2 months ago

Michuzi

WAZIRI MKUU AKEMEA MAKUNDI MANISPAA YA SONGEA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewakemea watumishi wa umma na madiwani ambao wameunda makundi ndani ya Manispaa ya Songea kwa kuweka mbele maslahi yao binafsi na akawataka wajirekebishe mara moja.

Ametoa onyo hilo jana (Jumamosi, Desemba 23, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa manispaa na madiwani kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Songea, mjini Songea mkoani Ruvuma.
“Watumishi wa umma ni lazima muelewe kwamba katika Halmashaurti zenu mnafanya...

 

2 years ago

Channelten

Waziri Mkuu abaini madudu katika ziara ya ghafla

BAN-1

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara ya ghafla kwenye kitengo cha upimaji mafuta bandarini (Oil Flow Metres) na kukuta zimejaa kutu baada ya kutelekezwa kwa miaka zaidi ya mitano. Pia alitembelea mita za kupimia mafuta zinazoendelea kujengwa Kigamboni.

Waziri Mkuu amempa saa nne tu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Bi. Magdalena Chuwa aandike barua ya kujieleza ni kwa nini aliamua kufunga mita hizo zisitumike kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita na amletee barua hiyo...

 

1 year ago

Michuzi

WAZIRI MKUU ABAINI MADUDU UUZAJI VIWANJA CDA

*Kiwanja chauzwa kwa sh. milioni 240 lakini zilizoingia CDA ni milioni 6 tu*Ahimiza kasi ya upimaji viwanja, asema waliolipa nusu wasinyang’anywe
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge), Bw. Uledi Mussa afuatilie malipo ya kiwanja kilichouzwa na CDA kwa sh. milioni 240 lakini fedha iliyoingia ofisini ni sh. milioni 6 tu.
“Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, ninataka ufuatilie mauzo ya kiwanja namba 26 block AA eneo la Kikuyu East ambacho...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani