WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWAONYA MAWAZIRI WATUMIE VIZURI MADARAKA YAO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaonya mawaziri na kuwataka watumie madaraka yao kwa manufaa ya Taifa na kamwe wasiyatumie kama fursa ya kujitajirisha wao binafsi.

Kassim Majaliwa amesema hayo leo Oktoba 16, 2017 alipozungumza na baadhi ya Mawaziri, Manaibu na Makatibu Wakuu katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam. 

Aidha Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli amesisitiza kwamba amewateua ili wafanye kazi na kamwe wasitumie madaraka waliyopewa kwa maslahi yao binafsi.

“Madaraka haya ya Uwaziri si fursa ya kujipatia utajiri, tunatakiwa tufanye kazi kwa weledi, uadilifu, bidii na uaminifu mkubwa ili kuondoa kero za wananchi kwa wakati.”

Waziri Mkuu amesema Mawaziri hao wanatakiwa wasimamie utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa Taifa wa miaka kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021. Pia utekelezaji wa ahadi zote zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 pamoja na ahadi alizozitoa Rais Dkt Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi.

Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka Mawaziri hao wakapunguze urasimu katika utekelezaji wa malengo ya Serikali kwa sababu wananchi wanahitaji kuhudumiwa kwa wakati 

Mawaziri waliohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Bw. Suileiman Jaffo pamoja na Manaibu wake Bw. Joseph Kandege na Bw. George Kakunda, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Ummy Mwalimu na Naibu wake Dkt. Faustine Ndungulile.

Wengine ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe na Naibu wake Bw. Jumaa Aweso, Waziri wa Viwanda na Biashara Bw. Charles Mwijabe na Naibu wake Mhandisi Stella Manyanya.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na Naibu wake Bw. Josephat Hasunga, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Naibu wake Bw. William Ole Nasha, Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Bw. Abdallah Ulega pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara hizo.

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Dewji Blog

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awaonya wanao wazulumu wakulima wa korosho

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wananchi wa kijiji cha Mibure wilaya ya Ruwangwa na Waziri Mkuu alitumia nafasi hiyo kuwataka wanunuzi wa korosho kufuata taratibu za ununuzi wa korosho ili wakulima wafaidike na zao hilo vinginevyo serikali haitasita kutaifisha magari pikipiki zitakazokamatwa kubeba korosho walizonunua kwa kutumia utaratibu wa Kangomba.

imgm9324Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wananchi wa kijiji cha Mibure wilaya ya Ruwangwa katika Mkoa wa Lindi kwa ziara ya kikazi.

imgm9369Mke...

 

3 months ago

Michuzi

MAWAZIRI MSITOE MATAMKO YASIYOTEKELEZEKA- WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri na Naibu Mawaziri wajiepushe na utoaji wa matamko yasiyotekelezeka ili kuepuka mikanganyiko Serikalini.
Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Novemba 7, 2017) wakati akifungua Kikao Kazi cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema ni vema  viongozi hao kabla ya kutoa matamko wakajiridhisha iwapo jambo hilo halitaleta athari za kibajeti na kisera na kama lipo katika bajeti za wizara zao.
Pia...

 

3 months ago

Michuzi

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKIWASIKILIZA MAWAZIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. Selemani Jaffo wakati wa Kikao cha kwanza Mkutano wa tisa wa Bunge kilichoanza leo Novemba 7, 2017 mjini Dodoma.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Umi Mwalimu wakati wa Kikao cha Kwanza Mkutano wa tisa wa Bunge kilichoanza leo Novemba 7, 2017 Mjini DodomaPICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

 

1 year ago

Channelten

Wadaiwa Sugu wa TTCL Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka taasisi zinazodaiwa kulipa madeni yao Juni 30

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka taasisi mbalimbali za umma zinazodaiwa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ziwe zimelipa madeni yao ifikapo Juni 30, mwaka huu.

TTCL inazidai taasisi mbalimbali za umma jumla ya sh. bilioni 11.5 ikiwa ni gharama ya huduma walizozitoa kwa taasisi hizo, hivyo kukwamisha utendaji wa kampuni hiyo.

Ametoa agizo hilo wakati akizindua huduma za simu ya mkononi kwa teknolojia ya 4G LTE ya TTCL mjini Dodoma ambapo amemtaka Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na...

 

2 years ago

Michuzi

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA KIKAO CHA KAZI CHA BARAZA LA MAWAZIRI DODOMA

Waziri Mkuu Mhe.  Kassim Majaliwa akiongoza Kikao cha Kazi cha Baraza la  Kazi la  Mawaziri kwenye ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma mwishoni mwa juma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

2 years ago

CCM Blog

PICHA RASMI ZA WAZIRI MKUU MAJALIWA KASSIM MAJALIWA NA MKEWE MAMA MARY MAJALIWA

 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa
Mke wa waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa

 

1 year ago

CCM Blog

KATIBU MKUU WA CCM KINANA AKUTANA NA WAZIRI MKUU MAJALIWA KASSIM MAJALIWA, LEO

 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akikabirishwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipofika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, kwa ajili ya mazungumzo na Katibu mkuu huyo wa CCM, leo.
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenda eneo la kufanyika mazungumzo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni baada ya...

 

2 years ago

Dewji Blog

Breaking News: Waziri Mkuu mteule ni Kassim Majaliwa Kassim!

BRAEKI

kasim

Kassim Majaliwa

Tayari dakika chache zilizopita kutoka ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dk, John Pombe Magufuli ametuma jina la Waziri Mkuu,  ambaye  ni Kassim Majaliwa aliyekuwa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Jina hilo limefikishwa kwa mbwembwe likiwa ndani ya bahasha tatu huku likiwa limeandikwa kwa mkono. Kwa hatua hiyo sasa  Bunge limeenda mapumziko na dakika chache kutoka sasa litarejea kwa ajili ya kupigia kura na wabunge...

 

1 year ago

Michuzi

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MSAIDIZI WA MTENDAJI MKUU WA OFISI YA WAZIRI MKUU


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Msaidizi wa Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Marehemu Margareth Lwekama katika ibada ya kumuombea marehemu iyoyofanyia kwenye Kanisa la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam Oktoba 24, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani