Waziri Mpina akutana na Taasisi za kusimamia Kemikali nchini

Na Lulu Mussa, Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, hii leo amekutana na taasisi zizohusika na uratibu na usimamizi wa kemikali hapa nchini. Akiongea na Taasisi hizo, Waziri Mpina amewaagiza watendaji hao kudhibiti na kusimamia kemikali hatarishi nchini ikiwa ni pamoja na kuratibu usafirishaji, usambazaji na matumizi ya kemikali hizo hapa nchini kwa namna bora zaidi.
Waziri Mpina amezitaka taasisi hizo kutoa taarifa za utendaji wa kazi kila robo ya mwaka kwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimizi wa Mazingira kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira kifungu namba 170. “Nawaagiza kuwasilisha takwimu za kemikali zinazozalishwa nchini, zinazoagizwa au kusafirishwa nje ya nchi, pamoja na kuainisha viwanda vinavyozalisha kemikali vilivyosajiliwa na maghala yaliyosajiliwa kuhifadhi kemikali hizo” alisisitiza Mpina.
Katika kikao hicho Waziri Mpina pia ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini ndani ya miezi miwili kuandaa muongozo na kuupitisha katika hatua zote wa namna bora ya kuteketeza taka hatarishi bila kuathiri mazingira.
Aidha Waziri Mpina ameagiza kuandaliwa kwa andiko litakalobainisha umuhimu wa kuteketeza taka hatarishi. “Kama taifa ni lazima tuwe na “dedicated Incinerator” kubwa kutekeza taka hizo hatarishi kwa kuzingatia taka zinazozalishwa hapa nchini” Mpina alisisitiza.
Katika hatua nyingine, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini, Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania, Tume ya Nguvu za Atomiki, Taasisi ya Utafiti ya Viuatilifu katika Kanda za Kitropiki, Mamlaka ya Chakula na Dawa, OSHA na Mkemia Mkuu wa Serikali kwa pamoja wametakiwa kuanda Hati ya Makubaliano ya kuratibu utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuhuisha Sheria zao na kuleta mapendekezo Serikali ya vifungu vya kufanyiwa marekebisho.
Taasisi alizokutana nazo ni pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC), Taasisi ya Nguvu za Atomiki, Mamlaka ya Chakula na Dawa na Mkemia Mkuu wa Serikali.Bw. Justine Ngaile Mkurugenzi wa Kinga na Mionzi kutoka Tume ya Atomiki akiwasilisha mada kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Luhaga Mpina. Waziri Mpini alikutana na Taasisi zinazohusika na usimamizi wa kemikali kujadilili mkakati wa pamoja wa kusimamia kemikali nchini. Baadhi ya wataalamu kutoka Taasisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Chakula na Dawa na Tume ya Nguvu za Atomiki wakifuatilia majadiliano na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (hayupo pichani), kikao kazi hicho kimefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais Dodoma.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Michuzi

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA TAASISI YA SEKTA BINAFSI NCHINI

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania  (TPSF) ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

9 months ago

Michuzi

NAIBU WAZIRI MPINA ATEMBELEA TAASISI ZA MUUNGANO KWA UPANDE WA ZANZIBAR

Naibu Waziri Ofisi ya Makmu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ameendelea na ziara yake Mjini Ugunja na kutembelea taasisi za Muungano ikiwa ni pamoja na Bank kuu ya Tanzania tawi la Zanzibar na Tume ya Sayansi na Teknolojia iliyopo chini ya Wizara ya Elimu na Sayansi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya uwasilishwaji wa taarifa fupi ya utekelezaji wa Bank kuu tawi la Zanzibar, na Naibu Gavana wa Bank hiyo Dkt. Natu Mwamba, Bw. Mansour Abdalla Meneja...

 

1 year ago

Michuzi

NAIBU WAZIRI LUHANGA MPINA AKUTANA NA WATENDAJI WA NEMC


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Mheshimiwa Luhaga Mpina (aliyekaa mbele), akizungumza na baadhi ya watendaji wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakati alipotembelea kwa mara ya kwanza Makao Makuu ya Ofisi ya Baraza hilo jijini Dar es Salaam leo. Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Mheshimiwa Luhaga Mpina (aliyekaa mbele), akisisitiza jambo kwa Wafanyakazi wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), wakati...

 

9 months ago

Michuzi

NAIBU WAZIRI MPINA AIASA TAASISI YA MUUNGANO KUFANYA TAFITI ZENYE TIJA KWA SERIKALI NA UMMA

Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anaeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. Luahaga Mpina Ametoa wito kwa taasisi za Muungano zinazofanya tafiti za kisayansi, kufanya tafiti hizo ziwe na tija kwa Serikali na Umma.
Mpina aliyassema hayo, alipotembelea taasisi ya Muungano ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha DSM ..iliyopo katika Wilaya ya Magharibi B nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar, iliyopo chini ya Wizara ya Wizara ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi ya Jamuhuri...

 

7 months ago

Michuzi

WAZIRI MWIGULU AKUTANA NA WAKUU WA TAASISI NA IDARA WA WIZARA YAKE.

 Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na wakuu wa Taasisi na Idara za wizara (hawapo pichani), wakati wa kikao cha  kujadili masuala mbalimbali ya mipango na maendeleo ya wizara. Kulia ni Naibu Waziri  Mhandisi Hamad Masauni. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam. Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na wakuu wa Taasisi na Idara za wizara wakati wa kikao cha  kujadili...

 

3 years ago

Michuzi

WAZIRI LAZARO NYALANDU AKUTANA NA TAASISI ZA UHIFADHI WANYAMAPORI JIJINI NEW YORK

 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa Taasisi ya Vulcan ya nchini Marekani  Bw. Dave Stewart (kushoto) na Bi. Lauren Ryder, inayojihusisha na masuala ya kuidadi tembo katika nchi 18 barani Afrika ikiwemo Tanzania, baada ya kufanya mazungumzo maalum ya ushirikiano yaliyofanyika katika jiji la New York nchini Marekani jana. Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu  akiagana na Bw....

 

8 months ago

Dewji Blog

Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla akutana na Ujumbe kutoka taasisi ya Touch Foundation

Naibu  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema siku ya Agosti 11.2016 amekutana na  wadau wa Sekta ya Afya  kutoka taasisi Touch Foundation kuangalia namna ya kusaidia sekta ya Afya hasa kwa maeneo ya pembezoni mwa  Nchi ili kuimalisha hudumm hizo.

Ugeni huo kutoka katika Taasisi ya Touch Foundation ya nchini Marekani umeonyesha nia yake ya dhati ya kuendelea kusaidiana na Wizara ya Afya ya Tanzania ikiwemo huduma za akina mama...

 

10 months ago

Michuzi

WAZIRI WA ARDHI AKUTANA NA TAASISI NA MAKAPUNI ILI KUFANIKISHA SHERIA YA UMILIKI WA SEHEMU ZA JENGO.

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willium Lukuvi wakati  akifungua mkutano wa Kujadili Matatizo na Ufumbuzi wa Utekelezaji wa Sheria ya Umiliki wa Sehemu za Jengo (Unit Tittle Act) iliyofanyika na wadau wa ardhi kutoka taasisi na makapuni mbali mbali ya ujenzi katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).Baadhi ya wawakilishi wa taasisi na makapuni mbali mbali ya ujenzi yakiwa katika mkutano huo.

 

1 year ago

Global Publishers

Waziri Makamba na Naibu Waziri Mpina Wakabidhiwa Ofisi

mah1Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa  Rais- Mazingira na Muungano Mh. January Makamba akipokea nyaraka za  Ofisi wakati akikabidhiwa Ofisi na Waziri aliyemaliza muda wake Dk.  Binilith Mahenge Ofisini Mtaa wa Luthuli Dar es Salaam.mah2Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa  Rais- Mazingira na Muungano Mh. Luhaga Mpina akikabidhiwa nyaraka za  Ofisi na Naibu Waziri aliyemaliza muda wake Mh. Stephen Masele .  Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini jijini Dar es Salaam.mah3Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa  Rais...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani