WAZIRI MWAKYEMBE AKANUSHA KUFUNGIA MASHINDANO YA MISS TANZANIA NA TUZO ZA MUZIKI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ametolea ufafanuzi kauli yake na kusema kuwa hajasitisha mashindano ya Miss Tanzania na tuzo za muziki nchini bali ametoa angalizo kwa waandaaji wa mashindano hayo kuwa na uhakika wa kuyaendesha.

Dk Mwakyembe amesema hayo leo Jumatatu kwenye ziara yake mjini Mtwara baada ya taarifa kuenea kuwa amefuta shindano hilo.
Mwakyembe yuko mkoani Mtwara katika ziara ya kuzungumza na watendaji walio chini ya wizara yake na kuzungukia viwanja vya michezo.
Amesema mashindano na tuzo hapa nchini huanzishwa bila kuwa na andiko la uendelezaji, hivyo ametoa agizo kwa Baraza la Sanaa (Basata) kwamba mtu yeyote akija na shindano au wazo la tuzo watamruhusu pale tu atakapotoa msingi wa mwendelezo na siyo kwa kuwa amepata mfadhili wa muda.
“Hata mashindano ya ulimbwende tumeshachoka watoto wa kike wanahangaika, watajipodoa lakini zawadi zikitangazwa unaambiwa mshindi wa kwanza gari namba mbili pikipiki ila sijawahi kuona hata mmoja ambaye amewahi kuzipata au ikatokea utoaji wa zawadi usio na kelele,” amesema.
Dk Mwakyembe amesema amekuwa akifuatwa na warembo kadhaa ofisini kwake wakilalamikia kutopewa zawadi zao mara baada ya mashindano ya Miss Tanzania, amesema alikaa na Basata miezi miwili iliyopita na kuwapa maagizo, “Kuanzia sasa chombo chochote au kampuni inayoendesha mashindano ya ulimbwende ambayo iliwahi kuahidi vijana wetu wa Kitanzania zawadi na haijatoa tusigombane, watoe zawadi zote wawatafute warembo wawape.”

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

5 months ago

Malunde

MWAKYEMBE APIGA MARUFUKU TUZO ZA MUZIKI NA MASHINDANO YA MISS TANZANIA

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe amepiga marufuku mashindano ya Miss Tanzania na tuzo za muziki kutokana na ubabaishaji wa waandaaji wa mashindano ya tasnia hizo.

Mwakyembe amesema mashindano ya Miss Tanzania yamegubikwa na ubabaishaji kwenye utoaji wa tuzo na kumekuwa na tabia ya kuchelewa kuwapa washindi zawadi wanazoahidiwa jambo linaloleta usumbufu.

Waziri huyo ameongeza kuwa watakaotaka kuandaa mashindano hayo ni lazima zawadi wanazoahidi kuwapa washindi zipekwe...

 

5 months ago

Zanzibar 24

Mwakyembe akanusha kuzuia mashindano ya Miss Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ametolea ufafanuzi kauli yake na kusema kuwa hajasitisha mashindano ya Miss Tanzania na tuzo za muziki nchini bali ametoa angalizo kwa waandaaji wa mashindano hayo kuwa na uhakika wa kuyaendesha.

Dk Mwakyembe amesema hayo wakati akiwa kwenye ziara yake mjini Mtwara kuzungumza na watendaji walio chini ya wizara yake na kuzungukia viwanja vya michezo.

Amesema mashindano na tuzo hapa nchini huanzishwa bila kuwa na andiko la...

 

10 months ago

Michuzi

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA UONGOZI WA CHAMA CHA NGOMA NA MUZIKI ASILI TANZANIA

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na uongozi wa Chama cha Ngoma  na Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) wakati alipokutana nao ofisini kwake Mjini Dodoma kujadili masuala mbalimbali ya Sanaa za Ngoma na Muziki Asili Tanzania leo April 21, 2017. Mwenyekiti wa Chama cha Ngomana Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) Wanne Salim Kutoka Kikundi cha  Wanne Star  akieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili wasanii wa Ngoma na Muziki Asili kwa...

 

2 years ago

Michuzi

WAZIRI NAPE AZINDUA MSIMU MPYA WA MASHINDANO YA UREMBO YA MISS TANZANIA 2016


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa baraka kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 uliofanyika katika hoteli ya Ramada Resort jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza wakishuhudia uzinduzi wa nembo mpya ya mashindano ya Miss Tanzania 2016 yaliyobeba kauli mbiu ya "Mrembo na Mazingira Safi"

 

2 years ago

Dewji Blog

Kamati ya Miss Tanzania yazindua msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 jijini Arusha

Baada ya kupewa baraka jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 yamezinduliwa tena jijini Arusha na Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu katika ukumbi wa klabu ya Triple A jijini humo na zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali yaliyojiri katika uzinduzi huo.

Hashim Lundenga

Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia)...

 

2 years ago

Michuzi

WAZIRI NAPE NNAUYE KUZINDUA MSIMU MPYA WA MASHINDANO YA UREMBO YA MISS TANZANIA 2016 JIJINI DAR

Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Lino International Agency LTD,Hashim Lundenga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani),katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO),kuhusiana na msimu mpya wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016.Lundenga amesema kuwa msimu huo mpya unatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya jumamosi Machi 19,2016 katika hotel ya Ramada Resort iliyopo eneo la Kunduchi jijini Dar.Katika uzinduzi huo utakaokuwa wa aina yake Mgeni rasmi amepangwa kuwa ni Waziri...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani