Waziri Nchemba aiombea timu ya Simba kwa hili

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk.Mwigulu Nchemba amesema kwa sasa anachoweza kukielezea kwa timu ya Simba anamuomba Mungu aifanikishe timu hiyo kushinda mchezo wa fainali wa michuano ya Sport pesa dhidi ya timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya.

Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu wametinga fainali ya michuano hiyo na kesho Jumapili watacheza mchezo wa fainali ya michuano hiyo na timu ya Gor Mahia ya Kenya.

Akizungumza na Michuzi Blog jijini Dar es Saalam jana...

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Bongo5

Waziri Nchemba atangaza kuwasaka wauza unga ‘hili linatuchafua sana’

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa siku 14 kwa maofisa wanaohusika na udhibiti wa dawa za kulevya kwenye mpaka wa Tunduma mkoa wa Songwe, kuwakamata watu wanaohusika na uvushaji wa dawa hizo kutoka nchini kwenda nchi jirani ya Zambia na nyingine zilizopo ukanda huo.
Mhe.-Mwigulu-Lameck-Nchemba

Nchemba alitoa agizo hilo janahgft7vHili linatuchafua sana, alipofanya ziara ya kukagua mpaka huo, ambapo alisema ni jambo lisilofichika kuwa kwa sasa Tanzania imechafuka kutokana na dawa za kulevya.

Alisema...

 

3 years ago

Dewji Blog

Waziri Nchemba aikataa Simba SC

Linaweza kuwa jambo la kufurahisha pale Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvivu, Mh. Mwigulu Nchemba alipovishwa mgolole na wananchi wa jimbo lake la Iramba Magharibi na kuonekana kutokufurahishwa na mgolole huo kwa sababu una rangi nyekundu.

Hayo yalitokea siku za karibuni wakati Waziri Nchemba alipotembelea jimboni kwake kwa ajili ya kuwashukuru wapiga kura wa jimbo hilo ambao walimpigia kuara na kumsaidia kurejea bungeni kwa awamu nyingine.

Sababu ya kutokufurahishwa kwake ni rangi ya mgolole...

 

3 years ago

MillardAyo

PICHA 10: Waziri Nchemba alivyowapatia ushindi wabunge wa Yanga vs Simba

img-20160925-wa0007

Septemba 25 2016 ilikuwa ni siku ambayo wabunge wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walicheza mchezo wa hisani kwa ajili  ya kukusanya fedha za watu waliopata na tetemeko la maafa Bukoba, wabunge walijigawa katika timu mbili wale wabunge ambao wanaishangilia Yanga na wabunge wa Simba. Mashabiki ambao walikuwa wamejitokeza uwanjani kuangalia wabunge hao wakiwa […]

The post PICHA 10: Waziri Nchemba alivyowapatia ushindi wabunge wa Yanga vs Simba appeared first on millardayo.com.

 

3 years ago

Bongo5

Hili ndio rungu la CAF kwa timu ya Yanga

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limeipiga faini ya dola 5,000 Klabu ya Young African kwa kosa la kuchelewesha mchezo baada ya wachezaji wake kumzonga mwamuzi wakati mchezo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya GD Sagrada Esperanca uliofanyika Angola Mei 18, 2016.

coupe-caf-dim

Uamuzi wa mchezo huo Na. 100 ulifanywa na Kamati ya Nidhamu ya CAF inayoundwa Mwenyekiti Raymond Hack – Raia wa Afrika Kusini na wajumbe Mustapha Samugabo (Burundi) na Gbenga Elegbeleye...

 

3 years ago

Bongo5

Hili ndiyo jibu la Pogba kwa timu zinazomnyatia

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya juventus, Paul Pogba ameziacha njia panda timu zinazomuania kwenye usajili unaoendelea barani Ulaya.

3458492

Pogba ambaye anawaniwa na klabu yak e ya zamani ya Manchester United na Real Madridi huku thamani yake ya usajili ikionekana kuwa ni zaidi ya paundi milioni 100 ambayo itaweka rekodi ya usajili ya dunia.

Akihojiwa wakati wa utoaji tuzo za ESPY Awards, Pogba aliishika jezi ya Juventus ambayo ilikuwa mojawapo kati ya jezi tatu zilizowekwa mbele...

 

3 years ago

Global Publishers

Mauzauza nyumbani kwa Waziri Nchemba

MWIGULU (5)Bibi kizee alivyonaswa usiku akirandaranda na tunguri nyumbani kwa Waziri Mwigulu Nchemba.

Stori: Francis Godwin, Risasi Jumamosi

DODOMA: Katika hali isiyo ya kawaida bibi kikongwe mmoja ambaye hakuweza kujulikana jina lake, amezua sintofahamu baada ya kukutwa nyumbani kwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akizunguka nyumba yake usiku huku akiwa na tunguri na wembe wenye damu.

MWIGULU (4)Tukio hilo lilitokea Mei 31, mwaka huu majira ya saa 6 usiku katika eneo la Kilimani mjini Dodoma...

 

2 years ago

MillardAyo

VIDEO: ‘Hatutamhukumu mtu kwa kazi anayoifanya, tutamhukumu kwa kosa analolifanya’-Waziri Nchemba

k67gk

Ikiwa imepita siku moja tangu waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba kusema kuwa watakaofanya unyama wa kuua au kuchinja watu au wanyama kwa mapanga na sime wataona chamoto, bado kauli hiyo imekaidiwa kwa baadhi ya watu wanaosadikika kuwa ni wa jamii ya kifugaji baada ya kumjeruhia kichwani kwa sime Rajabu Ayub (36) […]

The post VIDEO: ‘Hatutamhukumu mtu kwa kazi anayoifanya, tutamhukumu kwa kosa analolifanya’-Waziri Nchemba appeared first on millardayo.com.

 

3 years ago

Mtanzania

Jerry Muro aiombea Yanga kwa TB Joshua

jery muro*Ataka ubingwa Ligi Kuu, Shirikisho utue Jangwani

*Wapinzani wao Esperanca wagawa pointi Angola

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

OFISA Habari wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro, amesema ameiombea klabu yake hiyo kwa Nabii maarufu nchini Nigeria, T.B Joshua, alipokwenda nchini humo kwa ajili ya shughuli zake binafsi.

Muro ni mmoja wa Watanzania walioshiriki misa ya Jumapili katika kanisa la nabii huyo maarufu Afrika, ambaye anasifika kwa utabiri wa kweli.

Umaarufu wa TB Joshua ulishika kasi nchini...

 

2 years ago

Dewji Blog

Maagizo matatu ya Waziri Nchemba kwa Jeshi la Magereza nchini

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba leo Machi 17, 2017 ametoa maagizo matatu mazito kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza yaliyolenga kuboresha utendaji kazi wa idara hiyo nyeti hapa nchini.

Nchemba ametoa maagizo hayo, wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza uliofanyika katika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Agizo la kwanza alilolitoa ni jeshi hilo kuhakikisha linadhibiti wafungwa wa makosa ya jinai...

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani