WAZIRI TIZEBA AAGIZA MKURUGENZI WA BODI YA KOROSHO KUSIMAMISHWA KAZI

Waziri wa wizara ya kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Dodoma, Jumamosi 21 Aprili 2018. Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini taarifa ya Waziri wa wizara ya kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba ofisini kwake mjini Dodoma, Jumamosi 21 Aprili 2018.Katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akisikiliza maagizo ya kusitisha mkatanba wa kazi wa Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania, Leo Jumamosi 21 Aprili 2018.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo
Waziri wa wizara ya kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe kusitisha mkataba wa kazi wa Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndg Hassan Jarufo.
Waziri Tizeba ametoa agizo hilo kwa katibu mkuu wa wizara hiyo leo Jumamosi 21 Aprili 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Dodoma ikiwa ni muda mchache mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa.
Akielezea sababu za kuagiza kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi huyo, Mhe. Dkt Tizeba alisema kuwa hayo yamejili baada ya kuangalia mwenendo wa Ndg Jarufo na kutafakari jinsi zao la korosho linavyoendeshwa, ikiwa ni pamoja na kutoridhishwa na upatikanaji wa viuwatilifu kwa wakati.
Aidha, Mkataba huo umesitishwa kuanzia leo tarehe 21 Aprili 2018 hivyo Katibu Mkuu wa wizara hiyo atapaswa kufanya taratibu zote za kiutumishi ikiwa ni pamoja na kumpatia taarifa haraka muhusika na utekelezaji wake kuanza haraka.
Alisema ndani ya muda mfupi Wizara ya kilimo itamtangaza Kaimu Mkurugenzi wa Bodi hiyo ili kuchukua nafasi hiyo kuendeleza kusimamia sekta hiyo.

“Hizi hatua tunazochukua ni kuhakikisha kuwa wadau wakubwa wa korosho ambao ni wakulima wanaendelea kunufaika na zao lao, hivyo wakulima wasiwe na wasiwasi kwani pamoja na kuondolewa Mkurugenzi huyo lakini shughuli za serikali zitaendelea kama kawaida na maslahi yao yatasimamiwa ipasavyo” Alikaririwa Mhe. Dkt Tizeba.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

6 months ago

Michuzi

NEWZ ALERT:WAZIRI WA KILIMO DKT TIZEBA AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU WA BODI YA SUKARI TANZANIA


Na Mathias Canal, Dodoma
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amemuagiza Katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe kumsimamisha kazi mara moja Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Ndg Henry J. Semwanza kuanzia leo Novemba 9, 2017.
Kwa agizo hilo lililotolewa na Waziri wa Kilimo Dkt Tizeba, Mkurugenzi huyo atatakiwa kurejea kwa mwajiri wake ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kupangiwa kazi nyingine.
Simwanza anasimamishwa kazi kutokana na mwenendo...

 

2 years ago

Michuzi

Waziri Simbachawene aagiza kusimamishwa kazi kwa maafisa biashara wawili wa manispaa ya Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuwasimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Dodoma Bw. Elias N. Kamara na Bibi Donatila D. Vedasto (Afisa Biashara) kuanzia leo tarehe 30/12/2015 kwa kosa la kusababisha urasimu katika utoaji wa leseni za biashara.
Kutokana na hali hiyo Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kumuondoa kwenye...

 

1 year ago

MillardAyo

VIDEO: Waziri Kairuki aagiza kusimamishwa kazi vigogo watano na maofisa 106 TASAF

kairuki

Leo December 6 2016 Waziri wa nchi ofisi ya Rais, utumishi na utawala bora, Angela Kairuki amemuagiza mkurugenzi wa TASAF kuwasimamisha kazi mara moja maafisa washauri na ufuatiliaji wa TASAF 106 walioshindwa kufuatilia kaya zisizo stahili kuingia katika mpango wa kunusuru kaya maskini. Aidha Waziri Kairuki ameagiza kusimamishwa kazi kwa maafisa wa TASAF watano kutoka […]

The post VIDEO: Waziri Kairuki aagiza kusimamishwa kazi vigogo watano na maofisa 106 TASAF appeared first on...

 

2 years ago

Channelten

DC Aagiza Mganga Kusimamishwa Kazi Geita

mganga stop

MKUU wa wilaya Geita Hermani Kapufi , amemwagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Geita Alli Kidwaka kumuondoa mara moja mganga wa Zahanati ya Karoro wilaya na mkoa wa Geita Daniel Zengo , kwa madai ya kuuza dawa za Serikali kwenye duka lake binafsi.

Amesema hayo wakati akizungumza na mamia ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara ulifanyika kwenye Stand mjini Katoro lengo likiwa ni kujadili shughuli za maendeleo na kusikiliza kero za wananchi.

Kapufi amesema kuwa mganga huyo anatakiwa kuondoka...

 

1 year ago

Mtanzania

RC AAGIZA WATUMISHI WATATU KUSIMAMISHWA KAZI

 MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella

Na JUDITH NYANGE – MWANZA

 

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewaelekeza Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Clodwing Mtweve na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, George Lutengano, kuwasimamisha kazi watumishi watatu wa halmashauri hiyo kupisha uchunguzi wa matumizi ya fedha za Mpango wa Serikali wa Kuwezesha Shule za Sekondari nchini (SEDEP).

Pia amekataa kuweka jiwe la msingi katika nyumba za miradi ya SEDEP zilizopo Shule ya Sekondari...

 

2 years ago

Global Publishers

Waziri wa elimu amfuta kazi Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo

Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na ufundi, Prof Joyce Ndalichako. Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na ufundi, Prof Joyce Ndalichako amesitisha mkataba wa kazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo  George Nyatenga.  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo  George Nyatenga. Pia amewasimamisha kazi wakurugezi watatu wa Bodi hiyo ambao ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo Juma Chagonja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo.

Prof...

 

1 year ago

Bongo5

DC Hapi aagiza kusimamishwa kazi mratibu wa TASAF Kinondoni

Mkuu wa Wilaya Ya Kinondoni, Ally Hapi amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni kumvua madaraka mratibu wa TASAF wa wilaya hiyo, Onesmo Kweyamba kutokana na kasoro mbalimbali zilizosababisha upotevu wa fedha za serikali kwa kuwapatia kaya ambazo hazikustahili kupewa kupitia mradi wa TASAF.

ddfefbf12ada94b96a7efaff285bbaf2

Akizungumza na waandishi wa habari, Hapi amesema fedha taslimu kiasi cha 180,323,000/= zililipwa kwa kaya 515 ambazo hazikuwa na sifa za kulipwa kulingana na sifa zilizoainishwa huku...

 

4 months ago

Michuzi

Waziri wa Kilimo Dkt.Tizeba akagua usafirishwaji wa Korosho-Mtwara.

Waziri wa Kilimo Dkt.Charles Tizeba ametembelea Bandari ya Mkoa wa Mtwara na kukagua Usafirishaji wa Zao la Korosho Ghafi zinazokwenda nchi za India na Vietnam.Kufikia Januari 10 mwaka huu Jumla ya Tani Laki 190 za Korosho tayari zimesafirishwa, ambapo lengo ni kusafirisha Tani 230 katika Msimu huu.
Waziri wa Kilimo Charles Tizeba akiwa na Mkuu wa Bandari ya Mtwara Nelson Mlali wakikagua mizigo ya Zao la Korosho inayosafirishwa kwenda katika Nchi za India na Vietnam. 
Waziri wa Kilimo Charles...

 

2 years ago

Channelten

Kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hanang

Screen Shot 2016-04-07 at 3.28.46 PM

Mkuu wa mkoa wa Manyara Dkt Joel Bendera ametangaza kumsimamisha kazi mkurugenzi wa halmashauri ya Hanang Bw Felex Mabula kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha  zaidi ya milioni 600 ambapo uamuzi huo umeutoa mbele ya watumishi pamoja na madiwani wa hlamshauri hiyo.

Dkt Joel Bendera ametangaza uamuzi huo wa kumsimamisha kazi Bw. Felex Mabula kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha zaidi ya milioni 600 ambapo ubadhirifu huo umeibuliwa na baraza la madiwani baada ya kupokea ripoti ya...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani