WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AAGIZA MIRADI YOTE YA REA ITUMIE NGUZO ZA TANZANIA

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameagiza kuanzia sasa miradi yote ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) itumie nguzo na transfoma zinazotengenezwa nchini.
Alisema hayo juzi mjini hapa wakati akizindua Bodi ya Nishati Vijijini. Alisema ni vyema wakandarasi wa mradi huo wakafuatiliwa mahali wanaponunua vifaa. 
“Naagiza miradi yote ya REA awamu ya tatu itumie nguzo zinazozalishwa nchini, wakandarasi wote wanunue nguzo za Tanzania, zikiisha ndio waende nje ya nchi,” alisema.
Alisema tayari amepokea malalamiko kuwa nguzo zisizo na hadhi zinataka kununuliwa na kuna nguzo nyingine hazidumu hata miaka mitatu. 
“Hata transfoma tunataka zinazotoka ndani ya nchi, kuna kampuni Wanaosambaza chakula kibovu kushughulikiwa Muhongo azuia REA kutumia nguzo na transfoma za nje 202750005 ya Tanalec waelekezwe wafanye uzalishaji wa kutosha, transfoma nyingi za kutoka nje ya nchi zina matatizo,” alisema.
Pia alitaka kampuni zote za nje ambazo zitatekeleza mradi huo zifanye kazi na wakandarasi wadogo wa Tanzania.
 “Lazima wakandarasi wote wadogo wawe wa kampuni za kitanzania na kuna madai kampuni kubwa hazilipi wakandarasi wadogo na wakandarasi wadogo hawalipi vibarua,” alisema.
Alisema hali hiyo imekuwa ikifanya vijana wanaofanya kazi ya kuchimba mashimo ya kusimika nguzo katika maeneo ya vijijini kutolipwa. W
aziri huyo aliitaka bodi hiyo kukaa na wakandarasi watakaotekeleza miradi ya awamu ya tatu ili kujiridhisha na kila mkandarasi na kampuni yake aeleze historia yake na hiyo kazi ataiwezaje. 
Alisema katika REA awamu ya pili wakandarasi wanane walishindwa kazi na kuangalia kama majina yao yameingia katika miradi ya REA awamu ya tatu.
“Bodi lazima ikae na wakandarasi watakaotekeleza miradi ya awamu ya tatu na kila mkandarasi mjue historia yake na kama hiyo kazi ataweza. REA awamu ya pili iliyoisha wakandarasi wanane walishindwa kazi na mpewe majina kama wamewekwa katika awamu ya tatu,” alisema. 
Waziri Muhongo alisema lazima bodi ikae na wakandarasi hao na kuwauliza na kuangalia uwezo wao na makampuni yao ili kujiridhisha.
“Lazima muangalie kama ana uwezo muone, ukubwa wa bajeti, vitendea kazi walivyonavyo na wataalam walionao ni lazima maofisa wa REA na wale wa Shirika la Umeme (Tanesco) wawepo,” alitaka ubora wa kazi uangaliwe.
“Wabunge walipita Njombe walitutukana sana walikuta zaidi ya transfoma 20 zilikuwa zimekufa jambo kama hili halipendezi,” alisema. 
Mkurugenzi Mkuu wa Rea, Gissima Nyamo-Hanga alisema hiyo ni bodi ya nne ambapo kila baada ya miaka mitatu bodi mpya imekuwa ikiteuliwa.
Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa James Mdoe aliwataja wajumbe wanane wa bodi hiyo ni Mwenyekiti wake Dk Gideon Kaunda, wajumbe ni Amina Hussein, Innocent Luoga,Michael Nyagogo, Stella Mandago, Stolastica Jullu, Happiness Mhina na Theobard Manumbe.

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Michuzi

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA MRADI MKUBWA WA REA WA SHILINGI BILIONI 25.7 MKOANI SIMIYU

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo leo amezindua mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili, mkoani Simiyu ambapo vijiji 170 vimeunganishwa na mradi huo. Ninawasilisha picha za matukio pamoja na captions kwa ajili ya kuchapishwa kwenye vyombo vyenu vya habari ili kuhabarisha umma. Aidha, captions zinapatikana mwishoni mwa email hii.Mwananchi kutoka katika kijiji cha Nyanguge kilichopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu akiwasilisha...

 

1 year ago

Habarileo

REA kutekeleza miradi yote ya umeme ya MCC

SERIKALI imesema miradi yote ya umeme iliyokuwa ikifadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Changamoto za Milenia (MCC) nchini, itatekelezwa kupitia mradi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

 

1 year ago

Michuzi

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO ZIARANI LUSHOTO KUKAGUA MIRADI YA UMEME VIJIJINI

 Waziri  wa Nchi - Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba akielezea hali ya upatikanaji wa umeme katika jimbo lake, mara Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhogo alipofanya ziara katika jimbo lake. Profesa Muhongo yupo mkoani Tanga kwa ajili  ya kukagua miradi ya  umeme  vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) pamoja na kuzungumza na wananchi.


 Mbunge wa Lushoto, Shaban Shekilindi akielezea utekelezaji wa...

 

3 years ago

Vijimambo

KANUSHO KUTOKA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KUHUSU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb)--JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA NISHATI NA MADINIKatika gazeti la NIPASHE la Jumatatu tarehe 08 Desemba, 2014 ziliandikwa habari kuhusu Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb) chini ya kichwa cha habari “Wanaomtetea Muhongo Wajibu haya”. Hoja zilizotolewa katika gazeti hilo zililenga kupotosha ukweli. Wizara inapenda kutoa maelezo kuhusu hoja zilizotolewa kama ifuatavyo:

Utendaji wa Wizara chini ya Waziri wa...

 

3 years ago

Michuzi

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA SIMIYU KUKAGUA MIRADI YA UMEME NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya Ziwa na Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Profesa Muhongo anafanya ziara katika mikoa ya Simiyu, Tabora na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Taneesco.Mkazi wa kijiji cha Ihale kilichopo wilayani Busega mkoani Simiyu...

 

3 years ago

Michuzi

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO APATA MAPOKEZI MAKUBWA WILAYANI KISHAPU MKOANI SHINYANGA. AITWA “MZEE WA NGUZO” NA KUKABIDHIWA ZAWADI KWA KUSAMBAZA UMEME KWA KASI KUBWA WILAYANI HUMO

 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu.

 Wakazi wa kijiji cha Ndoleleji  wilayani Kishapu wakimsikiliza kwa makini  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani). Profesa Muhongo ameahidi kuwapatia umeme kabla  ya tarehe 30 Aprili, mwaka huu.

 Wakazi wa Bubiki wilayani Kishapu wakimkabidhi  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto)  zawadi ya mbuzi...

 

3 years ago

GPL

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA, WASHINGON, DC‏

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akitambulisha Mhe. Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo kwa Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka siku ya Jumatatu June 9, 2014 Waziri wa Nishati na Madini na ujumbe wake walipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ulipo mtaa wa 22, jijini Washington, DC. Balozi wa Tanzania nchini… ...

 

1 year ago

Michuzi

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AWAAGIZA WACHIMBAJI MADINI KUPELEKA ORODHA YA WACHIMBAJI WADOOWADOGO MADINI YA JASI NA MAKAA YA MAWE.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo akizungumza na wadau mbalimbali wa uchimabji wa madini ya Jasi (Gypsum) na Makaa ya mawe nchini leo Jijini Dar es salaam na kuwaagiza wawakilishi wa wachimbaji wa madini ya Jasi (Gypsum) kutoka kanda zote hapa nchini kufikia Agosti 10-11 kupeleka orodha kamili ya majina ya wachimbaji wadogo wadogo wa madini ya Jasi (Gypsum) na makaa ya mawe katika wizara ya Nishati na madini.
Hayo ameyasema wakati akizungumza na wadau mbalimbali wa...

 

3 years ago

Michuzi

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI GEORGE SIMBACHAWENE AFUNGUA MKUTANO WA KUJADILI NISHATI ENDELEVU NCHINI KWA WOTE

 Waziri wa Nishati na Madini  George Simbachawene akifungua mkutano  kwa ajili ya  kujadili nishati endelevu  nchini kwa wote ( Tanzania Sustainable  Energy for  All)  ulioshirikisha  sekta binfasi,  wataamu  kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na wadau wa nishati nchini.  Mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya   Protea jijini  Dar es Salaam  lengo lake lilikuwa ni kubadilishana uzoefu kwa ajili ya kuboresha  sekta ya umeme  nchini. 

 Meneja   Hifadhi kutoka Shirika la WWF Nchini Dk....

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani