YANGA NA SIMBA ZAPIGWA FAINI, SIMBA YAPEWA ONYO KALI KWA KOCHA WAKE MSAIDIZI

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imepitia ripoti za michezo yote ya Ligi Kuu Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja Pili (SDL) na kufanya uamuzi ufuatao.

Mechi namba 54 (Simba 4 v Njombe Mji 0).


Klabu ya Simba imepewa Onyo Kali kutokana na Kocha wake Msaidizi Masoud Djuma kuanza kufundisha bila kuwa na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini. Uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 40(13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.


Pia klabu hiyo imetakiwa kufikia Novemba 10 iwe imewasilisha Bodi ya Ligi nakala ya vibali hivyo, na kukumbushwa kuwa mahitaji ya nyaraka hizo ni kwa mujibu wa Kanuni za Ligi, lakini pia sheria za nchi.


Vilevile klabu ya Simba imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa timu yake kuwasilisha orodha ya wachezaji wake (team match list) nje ya muda wa kikanuni. Kitendo cha timu hiyo ni kukiuka Kanuni ya 14(2k) ya Ligi Kuu. Adhabu dhidi yao imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu.


Klabu ya Njombe Mji imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kuonesha vitendo vinavyoashiria imani za ushirikina katika mechi hiyo wakati ikiwasili uwanjani. Adhabu dhidi ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.


Mechi namba 56 (Stand United 0 v Yanga 4). Klabu ya Stand United imetozwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kutokana na golikipa wao kuvaa jezi yenye namba tofauti na ile iliyosajiliwa, kitendo ambacho ni ukiukaji wa Kanuni ya 60(11) ya Ligi Kuu kuhusu Usajili. Adhabu dhidi yao imezingatia Kanuni ya 60(12) ya Ligi Kuu.


Mechi namba 57 (Azam FC 1 v Mbeya City 0). Mwamuzi Shakaile Ole Yanga Lai amefungiwa miezi mitatu kwa kutoripoti na kuchukua hatua dhidi ya kitendo cha Kipa Owen Chaima wa Mbeya City kumpiga kofi mshambuliaji wa Azam FC. Kitendo cha Mwamuzi huyo ni ukiukaji wa Kanuni ya 38(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi wakati adhabu dhidi yake imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu.


Naye Kamishna wa mechi hiyo, David Lugenge amefungiwa miezi mitatu kwa kushindwa kuripoti tukio hilo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 39 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Kamishna.


Mechi namba 58 (Yanga 1 v Simba 1). Klabu ya Yanga imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na mashabiki wake kurusha uwanjani chupa zinazosadikiwa kuwa na mikojo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 42(1) kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Michuzi

AZAM, SIMBA, YANGA ZAPIGWA FAINI

Kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania  kilichoketi jumanne ya tarehe 24, Machi 2015 jijini Dar es salaam, kimepitia taarifa mbalimbali za michezo iliyochezwa na kutoa adhabu kwa wachezaji na vilabu vya Ligi Kuu ya Vodacom.

Katika mechi namba 107 iliyowakutanisha wenyeji Ndanda FC dhidi ya Coastal Unioni, klabu ya Ndanda imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu ya Vodacom  kutokana na washabiki wake kumrushia chupa...

 

11 months ago

Mwanaspoti

Simba yapewa onyo mechi ya Kagera

achezaji waliowahi kuichezea Simba waliopo katika kikosi cha Kagera Sugar wameitahadharisha timu hiyo kuwa hawatakuwa na undugu watakapokutana kesho kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

 

1 year ago

Michuzi

TFF YAMFUNGIA MWAMUZI SEIF, MANARA, SIMBA, AZAM ZAPIGWA FAINI.

Ofisa wa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini(TFF), Alfred Lucas akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.MWAMUZI Ahmed Seif amefungiwa kuchezesha mpira kwa miezi sita baada ya kutoa penati iliyokuwa sio sahihi pamoja na kupata alama chache ambazo haziruhusu kuchezesha ligi kuu katika mchezo baina ya African Lyon na Mbao uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF,kupitia kwa Ofisa habari wake Alfred...

 

2 years ago

Global Publishers

Kiiza aandikiwa barua ya onyo kali Simba

HAMISI-KIIZA.jpgMshambuliaji wa Simba, Kiiza.

Wilbert Molandi na Hans Mloli
KATIKA kuhakikisha wanatengeneza nidhamu kwenye timu, uongozi wa Simba umeliagiza Benchi la Ufundi la timu hiyo kumuandikia barua ya onyo kali mshambuliaji wake Mganda, Hamis Kiiza.

Hatua hiyo imekuja siku chache tangu uongozi wa Simba utangaze kumsimamisha beki na nahodha wake msaidizi, Hassani Isihaka kwa kile kilichodaiwa kuonyesha utovu wa nidhamu kwa kocha wao Mganda, Jackson Mayanja.
Mara ilivyotangazwa kusimamishwa kwa...

 

1 year ago

Mwananchi

Yanga, Simba zapigwa mkwara

Viongozi na mashabiki wa klabu za Simba na Yanga wanasifika kwa kuwakuza wachezaji, lakini wamekuwa chanzo cha kushuka viwango vya nyota wao katika klabu zao

 

1 year ago

Habarileo

Clouds tv yapewa onyo kali

KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), imetoa onyo kali kwa televisheni ya Clouds kwa kukiuka kanuni za huduma za utangazaji.

 

1 year ago

Habarileo

Yanga yapiga hesabu kali kwa Simba SC

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi ameanza kupandisha homa ya pambano la watani wao Simba baada ya jana kujinasibu kuondoka na pointi tatu katika mchezo huo utakaochezwa Oktoba Mosi, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

 

2 years ago

Dewji Blog

Kocha msaidizi wa Simba SC, Selemani Matola aachana rasmi na klabu hiyo!

Matola5                                       Kocha Seleman Matola 

Na Rabi Hume

Kocha msaidizi wa klabu ya Simba SC, Selemani Matola ametangaza rasmi kuacha kufanya kazi na Simba kufuatia kutokuwepo kwa maelewano mazuri na kocha mkuu, Dyran Kerr.

Matola amesema kuwa kwa kipindi kirefu amekuwa hana maelewano mazuri na kocha huyo kwa kila jambo ambalo anamshauli kocha mkuu Kerr kuwa akikataa na hata muda mwingine kumtolea maneno ya dharau.

Aidha Matola amesema kuonyesha kuwa kocha huyo hakuwa...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani