Yanga, Simba, Azam mawindoni

hans-pluijmNA WAANDISHI WETU

VIGOGO wa soka nchini timu za Simba, Yanga na Azam, leo zinatarajiwa kushuka dimbani katika viwanja tofauti kuchuana vikali katika mechi za mwendelezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), iliyoanza kutimua vumbi Jumamosi iliyopita.

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga, wapo kileleni kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa huku wapinzani wao, Simba na Azam wakifuatia jambo linalofanya ushindani wa mechi za leo kuwa mkubwa kutokana na timu hizo kuwa kwenye vita ya ubingwa.

Yanga itabaki kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuwakaribisha maafande wa Tanzania Prisons, ambao walianza vibaya Ligi Kuu kwa kupata kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Azam Jumamosi iliyopita.

Kocha Mkuu wa Wanajangwani hao, Hans van Pluijm, aliliambia MTANZANIA jana kuwa wamejiandaa vya kutosha kwa mchezo huo na anafahamu vizuri staili ya uchezaji wanayoitumia maafande wa Tanzania Prisons.

“Jambo la msingi ni wachezaji kucheza kwa kujituma uwanjani na kuelekeza nguvu zao kwenye mchezo huo kuanzia mwanzo hadi mwisho kuhakikisha wanaibuka na ushindi kama walivyofanya awali kwa Coastal Union,” alisema.

Simba walioichapa African Sports bao 1-0 katika mechi ya awali, wataendelea kuwa ugenini kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kwa kumenyana na Mgambo JKT ya huko.

Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, amejihakikishia ushindi mnono dhidi ya maafande hao huku akionekana kuwapa mazoezi makali wachezaji wake, akiwataka kupiga pasi 100 bila kupoteza kwa adui katika mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Disuza jana.

Jambo linalomnyima raha Kerr ni kitendo cha kukutana na Mgambo huku akiwa hafahamu mfumo unaotumiwa na Kocha wa Mgambo, Bakari Shime, lakini amejipa moyo kwamba watatumia uzoefu kwa kupata kikosi bora cha ushindi.

Katika mchezo huo Simba watamkosa mshambuliaji wao wa kulipwa, Daniel Lyanga, kutokana na kukosa hati ya uhamisho wake wa kimataifa (ITC) kutoka timu yake ya awali ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambao bado hawajaituma.

Kwa upande wake kocha Shime wa Mgambo Shooting, alisema kamwe Simba haiwezi kuvunja mwiko kupata ushindi kwenye uwanja wao wa nyumbani huku akidai kikosi chake kipo fiti kuwavaa wapinzani wao.

Azam iliyosafiri hadi mkoani Shinyanga itakuwa ikisaka pointi tatu nyingine kwa kuivaa Stand United ya huko, kocha mkuu wake, Stewart Hall, amesema ataendeleza wimbi la ushindi kwenye mechi hiyo na nyingine zinazofuata.

Wakati Azam ikianza vema mbio za kuwania ubingwa wa ligi hiyo kwa kuichapa Tanzania Prisons mabao 2-1, Stand United ilichapwa nyumbani na Mtibwa Sugar bao 1-0 nyumbani.

“Katika mechi yetu na Prisons tungeshinda zaidi ya mabao manne au matano lakini washambuliaji walipoteza nafasi nyingi, hata hivyo, katika kipindi hiki tutawekana sawa kuhakikisha tunakamilisha malengo yetu kwa kushinda dhidi ya Stand United na mechi zinazokuja,” alisema.

Katika mechi nyingine, Mtibwa Sugar iliyoanza kwa ushindi dhidi ya Stand United, watakuwa ugenini kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kuchuana na Toto African, mchezo ambao umetabiriwa ugumu na kocha wake, Mecky Mexime. Toto nayo ilipata ushindi huo walipoivaa Mwadui.

Majimaji watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Majimaji Songea huku Mbeya City wakitarajiwa kufuta machungu ya kufungwa kwa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Ndanda FC watawakaribisha Coastal Union kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, baada ya kujeruhiwa na Yanga kwa kufungwa mabao 2-0 Jumapili iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

HABARI HII IMEANDIKWA NA ONESMO KAPINGA, TANGA NA JUDITH PETER, MWALI IBRAHIM, ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Mtanzania

Yanga, Azam mawindoni Ligi Kuu

yanga-azamNa ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

LIGI Kuu Tanzania Bara inatarajia kuendelea leo kwa kuchezwa michezo saba kwenye viwanja tofauti, huku mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Yanga wakiwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kucheza na Majimaji ya Songea.

Yanga ina pointi nne hadi sasa baada ya kucheza mechi mbili, wataingia uwanjani wakiwa na machungu ya kuambulia pointi moja mkoani Mtwara walikocheza na Ndanda FC Jumatano iliyopita.

Yanga inayonolewa na kocha Hans van Pluijm, inatarajia kuwatumia...

 

3 years ago

Mtanzania

Vigogo Simba, Yanga mawindoni

Simba-YangaJUDITH PETER NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM
VIGOGO wa soka nchini, Simba na Yanga, watashuka dimbani leo kusaka pointi muhimu kwenye viwanja tofauti ikiwa ni mwendelezo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) mzunguko wa pili unaoelekea ukingoni.
Yanga ambao Jumapili iliyopita waliichakaza FC Platinum ya Zimbabwe kwa mabao 5-1 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar kwenye uwanja huo.
Simba nao wamesafiri hadi...

 

6 months ago

Michuzi

AZAM WAZIKARIBISHA SIMBA NA YANGA AZAM COMPLEX

Afisa habari  wa Azam Fc Jaffar Iddy.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UONGOZI wa Klabu ya Azam umefurahiswa na maamuzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kwa kuamua kutumia Uwanja wa Azam Complex kwa michezo ya nyumbani ya timu hiyo.
Hilo limekuja baada ya Bodi ya Ligi kutoa ratiba mpya na kuzitaka timu za Simba na Yanga kwenda kucheza mechi zao dhidi ya Azam katika Uwanja huo.
Akizungumza kwa niaba ya klabu ya Azam, Afisa habari Jaffar Iddy ameupongeza uongozi huo chini ya Rais mpya...

 

12 months ago

Michuzi

SIMBA WAINGIA MAWINDONI KUSAKA POINTI 3 ZA MBEYA CITY JUMAMOSI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Kikosi cha Simba kimeeendellea na mazoezi katika viwanja vya Chuo cha Polisi Kilwa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa l.igi kuu dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Jumamosi kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.
Simba ambayo ipo kambini toka jana jioni, inajifua zaidi ili kuweza kutoka na ushindi kwenye mchezo huo ambapo wapo katika mbio za kuutafuta ubingwa wa ligi kuu Vodacom msimu wa 2016/2017.
Wanamsimbazi hao ambapo katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Yanga waliweza...

 

2 years ago

Habarileo

Azam, Yanga, Simba vitani

LEO ni vita ya namba. Baada ya mapumziko ya mwezi mmoja michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara itaendelea kutimua vumbi katika viwanja sita tofauti, huku Simba, Azam FC na Yanga kila moja ikiingia katika vita ya namba kusaka pointi tatu muhimu.

 

2 years ago

Mtanzania

Vita ya Yanga, Azam, Simba

simba,azam,yangaNA ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

TIMU za Yanga, Azam na Simba, leo zinaingia kibaruani kwa mara nyingine katika viwanja tofauti katika raundi ya 12 ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Yanga, wao watakuwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kuwakabili Stand United ya Shinyanga.

Yanga, wanaoongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 11, wanashuka dimbani wakitokea mkoani Tanga, ambako wamecheza mechi mbili baina ya Mgambo Shooting na Africans Sports,...

 

2 years ago

Mtanzania

Yanga, Azam, Simba vitani

Pg 32 Okt 17NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

LIGI Kuu ya Tanzania Bara inaendelea leo kwa mechi sita katika viwanja tofauti huku Yanga ikiikaribisha Azam FC katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga, Azam na Simba zitakuwa zikicheza kusaka ushindi katika mechi zao ili zijiweke katika nafasi nzuri katika mbio za kuwania taji la Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga ina pointi 15 sawa na Azam lakini inaongoza kwa kupachika mabao 13 huku Azam ikiwa na mabao 9, hivyo kila moja itakuwa ikisaka ushindi ili kuongoza...

 

2 years ago

Mwananchi

Simba, Azam ni kikwazo Yanga

Kocha wa Yanga, Hans Pluijm amesema hatima ya timu yake kutetea ubingwa wa Ligi Kuu imeshikiliwa na wapinzani wake wakubwa Azam na Simba.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani