YANGA YAANZA KUNUKIA, SPORTSPESA KUMWAGA MANOTI


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


IKIWA katika hali ya kuyumba kiuchumi na kushindwa kuwalipa wachezaji wao mishahara kwa wakati, neema imeanza kuwaangukia baada ya kampuni ya SportsPesa ya Kenya kutaka kuwamwagia fedha iwapo mkataba wao utafanikiwa.

Yanga itakuwa ni ya tatu kwa timu za Afrika Mashariki kuingia mkataba wa fedha nyingi iwapo watakapofanikiwa kumalizana kumalizana na Kampuni ya SportsPesa ya Kenya.
Iwapo mkataba huo utafanikiwa, Yanga na kampuni hiyo ya SportsPesa watasaini mkataba wenye thamani ya bilion 4.5 ambapo utakuwa ni wa miaka mitano ambapo kwa mwaka utakuwa na thamani ya Sh milioni 900.
Uongozi wa Yanga leo unatarajiwa kutakutana na wawakilishi wa kampuni hiyo, ambapo wakikubaliana wataingia mkataba huo wa miaka mitano ambao kila mwaka utakuwa na nyongeza ya asilimia sita ya fedha.
Awali, SportsPesa walileta mapendekezo katika klabu ya Yanga kuhusiana na mkataba huo lakini ulikatiliwa kutokana na mkataba huo kutokukidhi vigezo nan kuwa na maslahi na wakawapelekea mapendekezo yao na namna gani wanataka mkataba huo uweje.
"\Leo wawakilishi wa SportPesa watakutana na uongozi wa Yanga ili kumalizana nao juu ya mkataba wanaotaka kuingia na hiyo ni kutokana na kufika makubaliano ya kimkataba," kiisema chanzo kutoka kamati ya utendaji ndani ya klabu hiyo.
Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, ambaye alisema wapo kwenye hatua za mwisho za kuingia mkataba na SportsPesa.
"Napenda nizungumze kitu kilichokua tayari au kimekamilika hatua ya kuingia mkataba na SportsPesa bado, ila tutakutana nao kwa mazungumzo ya mwisho ambayo yatatoa jibu kama watatudhamini au la.
"Tunazungumza na SportsPesa kwa kuwa hawa wamekuja moja kwa moja kwetu tofauti na kampuni nyingine ambazo zinataka kutudhamini, lakini ipo kampuni tuliyoipa jukumu la kufanya mazungumzo nao nasi kutuletea taarifa ya kila kinachoendelea." alisema Mkwasa.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

5 months ago

Michuzi

KRISMAS YAANZA KUNUKIA

Mfanyabiashara ndogondgo (mmachinga) akiwa amebeba mti wa Krismas kwa ajili ya kuuza ikiwa ni muda muafaka kabisa wa maandalizi ya msimu wa sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya.

 

1 year ago

Mtanzania

Coastal Union yasaka manoti kwa Yanga

Kikosi-cha-Coastal-Union-01NA ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa timu ya Coastal Union ya Tanga, umeahidi kuwazawadia fedha wachezaji wake iwapo itaifunga Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Inadaiwa wachezaji wa timu hiyo wameahidiwa donge nono iwapo wataifunga Yanga katika mchezo huo ambapo bingwa ataiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Coastal Union imetinga hatua hiyo baada ya kuiondoa Simba kwenye hatua ya...

 

1 year ago

Habarileo

Halmashauri Longido yadaiwa kunukia ufisadi

HALMASHAURI ya Wilaya ya Longido mkoani Arusha, imetakiwa kuandaa upya taarifa ya ukaguzi iliyoiwasilisha kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mwaka 2013/14 na kuiwasilisha upya katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC).

 

3 years ago

Mwananchi

Simba wajazwa ‘manoti’

>Uongozi wa  Simba umewazawadia wachezaji wake  kitita cha Sh60 milioni baada ya kufanikiwa kuichapa Yanga mabao 3-1 katika pambano la Hisani lililopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

 

1 year ago

Habarileo

Twiga wajazwa manoti

WACHEZAJI wa timu ya soka ya taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ jana walikabidhiwa fedha kiasi cha Sh 300,000 kila mmoja ikiwa ni motisha kabla ya kurudiana na Zimbabwe katika michuano ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake baadaye mwaka huu huko Cameroon.

 

8 months ago

Michuzi

BWANA DAVID MANOTI AUGA UKAPERA.

Bwana Harusi David Saire Manoti akiwa na Mke wake mpenzi Nezia Manumbu  Baada ya Kufunga Pingu za Maisha katika Kanisa la St. Peters Jijini Dar. Maharusi wakipata Picha ya pamoja na Wasimamizi waoMaharusi wakipata picha  na wasimamizi wao pamoja na wasindikizaji walionogesha Harusi hiyo.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA.

 

2 years ago

Michuzi

SHIMUTA, NSSF WAMJAZA MANOTI MJANE WA GURUMO

Hatimaye mjane wa marehemu Muhidini Gurumo, Pili Kitwana amepokea Sh2 milioni kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF kwa ajili ya ununuzi wa Bajaji.
NSSF ilitoa fedha hizo ikiwa ni juhudi za Shirikisho la Muziki nchini (SHIMUTA), ambapo walimuahidi kumpatia mjane huyo kiasi cha fedha ambacho kitamuwezesha kununua bajaji imsaidie kuendesha maisha yake.
"Mwaka huu mwezi wa tano tulimuahidia mama Gurumo tutamsaidia kusaka fedha kwa wadau mbali mbali tuweze kufanikisha azma yetu ya...

 

3 years ago

GPL

Thomas Ulimwengu noma, amwaga manoti ukumbini

Mshambuliaji wa TP Mazembe ya DR Congo, Thomas Ulimwengu akigawa manoti. Na Issa Mnally
MSHAMBULIAJI wa TP Mazembe ya DR Congo alionyesha kweli maisha yake sasa ni ya juu baada ya kumwaga fedha kwa wanamuziki wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’. Ulimwengu alifanya hivyo kwenye shoo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar siku ya Boxing Day. Mshambuliaji huyo wa...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani