Yanga yagoma kuifuata Simba Zanzibar

katibu+yangaNA JUDITH PETER, DAR ES SALAAM

TIMU ya soka ya Yanga ni kama inawakwepa watani wao wa jadi Simba, baada ya kuachana na mpango wake wa kuweka kambi visiwani Zanzibar kujiandaa na michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza Jumamosi hii.

Awali mabingwa hao wa Ligi Kuu walipanga kuifuata Simba Zanzibar, lakini ghafla wamebadili msimamo wao na kuamua kubaki jijini Dar es Salaam kwa madai huenda wakapata tabu ya uwanja wa kufanyia mazoezi wakiwa Zanzibar.

Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha, aliliambia MTANZANIA jana kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya kugundua hakuna jipya watakaloibuka nalo kwenye kambi ya Zanzibar ambako timu za Simba na Azam zimeenda kusaka makali ya Ligi Kuu.

“Tumebadili mpango wa kwenda kuweka kambi Zanzibar kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukwepa matatizo yanayoweza kujitokeza ya kukosa uwanja wa kufanyia mazoezi,” alisema.

Alisema Yanga itaanza mazoezi rasmi kesho baada ya nyota wake waliokwenda kuzitumikia timu za taifa kuungana na wenzao ili kuanza mikakati kabambe ya kupambana kwenye ligi hiyo.

Wachezaji hao ni Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ Salum Telela, Deus Kaseke, Simon Msuva walioichezea timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ juzi ambao wanatarajiwa kuungana na wenzao baada ya kambi yao kuvunjwa.

Tiboroha alisema nyota wao wa kulipwa, Vicent Bossou na Thabani Kamusoko, tayari wamerejea nchini tangu juzi na kiungo Haruna Niyonzima na mshambuliaji, Amissi Tambwe, walitarajiwa kutua jana usiku.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Mholanzi, Hans van der Pluijm, alikuwa akiwasubiri kwa hamu nyota hao ambao alijivunia kuwa uwepo wao kwenye timu za taifa, unaweza kuleta mafanikio kwenye kikosi hicho kutokana na majukumu waliyokabidhiwa.

Yanga itafungua pazia la Ligi Kuu kwa kuwakaribisha Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuwafunga wapinzani wao hao mabao 8-0 katika mechi ya mzunguko wa pili msimu uliopita.

 

 

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

BBCSwahili

Yanga kuifuata Mediama

Mabingwa soka Tanzania bara Yanga wainatarajia kuondoka jijini Dar es salaam kwenda Ghana kuwafuata wapinzani wao Medeama.

 

3 years ago

Mwananchi

Yanga kuikwepa , kuifuata Azam

Yanga inaingia uwanjani kuikabili timu ngumu ya Al- Khartoom ya Sudan leo katika mchezo wa kukamilisha ratiba, lakini wenye kutoa msimamo halisi wa Kundi A la Mashindano ya Kagame.

 

3 years ago

Vijimambo

30 Yanga SC kuifuata Platinum JumatanoNa Bertha Lumala, Dar es SalaamMsafara wa watu 30 wa Yanga SC, wakiwamo viongozi, utaondoka jijini hapa Jumatano kwenda Zimbabwe kwa ajili ya mechi yao ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Platinum FC, mtandao huu umeelezwa.Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro, katika mahojiano na mtandao huu jijini hapa muda mfupi uliopita, amesema kikosi chao kilichopiga kambi jijini hapa, kitasafiri kuwafuata wapinzani hao Aprili Mosi, yaani Jumatano.
Amesema kila kitu...

 

2 years ago

Habarileo

Yanga kuifuata Ahly Jumamosi

KLABU ya Yanga inatarajia kuanza safari ya Misri kurudiana na Al Ahly ya huko katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya mchezo wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Jumamosi ya wiki hii.

 

1 year ago

Mwananchi

Yanga kuifuata Mtibwa kesho asubuhi

Dar es Salaam. Kikosi cha Yanga kinaondoka kesho asubuhi kuelekea mkoani Morogoro kuumana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu unaotarajiwa kupigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Jamhuri.

 

1 year ago

BBCSwahili

Yanga kuifuata Mouloudia Club Alger

Yanga inakwenda kwenye mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Mouloudia Club Alger Jumamosi , mjini Algiers.

 

2 years ago

Global Publishers

Simba Hii Tishio, Azam Yagoma Kucheza Nayo

SIMBA DAY (19)

Mshambuliaji mpya wa Simba, Mrundi Laudit Mavugo.

Nicodemus Jonas, Dar es Salaam
KIWEWE? Katika kile kinachoonekana kuwa Simba ni tishio msimu huu, uongozi wa Azam umewasilisha barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutaka mechi yao dhidi ya Simba ya mzunguko wa tano ipigwe kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Chamazi badala ya Taifa.

Makamu Mwenyekiti wa Azam, Iddrisa Nassor ‘Father’ amefunguka kwa mapana kuhusu barua yao hiyo ambayo pia msemaji wa TFF, Alfred Lucas amekiri kuipokea,...

 

2 years ago

Habarileo

Ndanda yaeleza kiini kuifuata Yanga Dar

UONGOZI wa timu ya soka ya Ndanda FC umesema `njaa’ ya pesa ndiyo iliyowalazimu kuridhia kucheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho badala ya uwanja wao wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

 

11 months ago

BBCSwahili

Mbeya City kuifuata Yanga Dar-Es-Salaam

Kikosi cha Mbeya City Fc , leo kinaanza safari kuelekea jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara hidi ya wenyeji Yanga

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani