Yusuph Mlela aomba pambano la ngumi na Nay wa Mitego

Msanii wa filamu nchini Yusuph Mlela aamemshutumu rapa Nay Wa Mitego kwa kile anachodai kuwa msanii huyo anapotosha jamii juu ya maandamano waliofanya baadhi ya wasanii wa filamu nchini.

Baada ya wasanii hao kuandamana wakipinga uingizwaji wa filamu za nje ambazo hazilipi kodi, kwa madai ziwaaribia soko lao la filamu za ndani, rapa Nay wa Mitego alisikika akisema kuwa baadhi ya wasanii wa filamu ambao waliandamana ni mataahira kwani kitendo cha wao kutaka filamu za nje zizuiliwe, hakina tija na mantiki yoyote.

“Walichokifanya baadhi ya Bongo Movie mataahira ni sawa na sisi wasanii tugome kuimba kisa nyimbo za wasanii wa nje zinapigwa sana Tanzania huyo ni utaahira,” alisema Nay wa Mitego kupitia video ambayo ameisambaza mtandaoni.

Kutokana na maneno ya kejeli ya Nay wa Mitego, muigizaji wa filamu Yusuph Mlela alishindwa kuvumilia na kuamua kumtolea povu rapa huyo.

“Nay True Boy wewe jamaa si ulikuwa chokoraa wewe, leo umeyapatia kidogo unasahau kwamba nyuma yako kuna kundi la vijana wanatamani kuwa waigizaji\wanamuziki wakubwa….Acha kupotosha jamii yetu Kwa sababu zako binafsi… sisi wasanii hatujakataza movie za nje. Tunataka wanaozisambaza wafuate taratibu za kisheria ili uwiano wa biashara uwepo ndiyo lengo la maandamano” aliandika Mlela Instagram.

Aliongeza, “Nay wa Mitego acha kutafuta sifa… nakushangaa kuwa na ufikirivu mdogo kama wewe siyo msanii…halafu huwezi kufananisha filamu na muziki….. Wewe si mtoto wa Manzese unajifanya unajua kupiga ngumi nataka Round 3 tu za boxing kwenye stage ili Tanzania ijue nani taahira nikutie adabu….. This is serous coz we mtoto mdogo tu kwangu ********** kuongea sana tabia za kike, wewe si hip hop na unajiamini njoo uwanjani chagua popote pale” Yusuph Mlela

Jiunge na Bongo5.com sasa Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!Share on Whatsapp

Bongo5

Read more


Habari Zinazoendana

12 months ago

MillardAyo

EXCLUSIVE: Majibu ya Nay wa Mitego baada ya kuombwa pambano la ngumi na Yusuph Mlela

Siku chache sasa zimepita tangu muigizaji staa wa Bongo movie Yusuph Mlela kuomba pambano la ngumi dhidi ya rapa Nay Wa Mitego, sasa kinachoendelea ni kwamba ujumbe huo umemfikia mhusika. Kutokana na ujumbe huo wa Yusuph Mlela kwenye EXCLUSIVE interview na Ayo TV Entertainment na millardayo.com Nay ameelezea majibu ya ombi hilo ambapo mbali na kuzungumzia pambano […]

The post EXCLUSIVE: Majibu ya Nay wa Mitego baada ya kuombwa pambano la ngumi na Yusuph Mlela appeared first on...

 

1 year ago

Bongo Movies

Yusuph Mlela Amfungukia Nay wa Mitego

Msanii wa filamu nchini Yusuph Mlela amemtusi rapa Nay wa Mitego kwa kile anachodai kuwa msanii huyo anapotosha jamii juu ya maandamano waliofanya baadhi ya wasanii  wa filamu nchini.

Yusuph Mlela ambaye kwenye post yake ameonekana kushindwa kutumia lugha ya staha huku akionesha kutokwa na povu jingi kutokana na mapokeo ya mashabiki wa filamu ambao walio wengi wamekuwa wakiwachana wasanii hao na kuwataka kufanya kazi zenye ubora.

Rapa Nay wa Mitego alisikika akisema kuwa baadhi ya wasanii...

 

12 months ago

Bongo Movies

Yusuph Mlela Ataka Wazichape na Nay wa Mitego

Muigizaji wa filamu za bongo Yusuph Mlela leo amezungumza na kumtaka msanii wa muziki wa hip hop na Bongo fleva Nay wa Mitego, kuheshimu na kutoziingilia kazi za wasanii wengine kama anavyoheshimu kazi zake.

Muigizaji wa filamu za bongo Yusuph Mlela

Yusuf Mlela aliendelea kwa kusema kuwa kama Nay wa Mitego anaona ameshafanikiwa kimaisha basi awapishe wasanii wengine waendelee kujitafutia riziki kwani bado wana safari ndefu kimaisha.

‘Mimi namuomba sana Nay ajiheshimu sana, asiingilie kazi za...

 

1 year ago

Bongo Movies

Beef ya Nay wa Mitego na Yusuph Mlela Yafika Pabaya

Baada ya muigizaji wa filamu, Yusuph Mlela kuomba pambano la ngumi na rapa Nay wa Mitego, rapa huyo amemjibu muigizaji huyo kwa maneno ya kejeli.

Wawili hao waliingia kwenye bifu hilo baada ya Nay wa Mitego, kuwaita wasanii wa filamu ‘mataahira’ kisa kuandamana kupinga biashara ya filamu ‘feki’ za nje ambazo hazilipi kodi.

Rapa huyo amedai hawezi kupigana na muigizaji huyo huku akimkejeli kwa kumuita Mlela ni mwanamke.

“Nasikia kuna mwanaume/mwanamke yupo Bongo Movie anataka kupigana na...

 

1 year ago

Malunde

MSANII WA FILAMU YUSUPH MLELA AMMWAGIA MATUSI RAPA NAY WA MITEGO

Msanii wa filamu nchini Yusuph Mlela amemtusi rapa Nay wa Mitego kwa kile anachodai kuwa msanii huyo anapotosha jamii juu ya maandamano waliofanya baadhi ya wasanii  wa filamu nchini.
Yusuph Mlela ambaye kwenye post yake ameonekana kushindwa kutumia lugha ya staha huku akionesha kutokwa na povu jingi kutokana na mapokeo ya mashabiki wa filamu ambao walio wengi wamekuwa wakiwachana wasanii hao na kuwataka kufanya kazi zenye ubora.
Rapa Nay wa Mitego alisikika akisema kuwa baadhi ya wasanii wa...

 

1 year ago

Bongo5

Meek Mill aomba pambano la ngumi na Drake

Baada ya pambano la Soulja Boy na Chris Brown kuwa na mvuto mkubwa duniani, rapper Meek Mill ameomba pambano la ulingoni na Drake.

Ijumaa hii kimesambaa kipande cha video mitandaoni kikimuonyesha Meek akizungumza kuwa anahitaji pambano na Drake lakini sharti lake anataka alipwe dola milioni tano huku akimtaka ex wake Nicki Minaj awe ni mrembo wa ulingoni [Ring girl]. “I’ll break Drizzy the fuck up for five mill. Of course, I would,” amesema Meek katika video hiyo.

“We gonna let Nicki...

 

3 years ago

Vijimambo

BONDIA WA MOROGORO AOMBA PAMBANO LA NGUMI KWA MAPROMOTA

Na Mwandishi Wetu 


PIUS KAZAULABONDIA Pius Kazaula wa Morogoro KG 66 amejitokeza hadharani na kuwaomba wadau wa mchezo wa masumbwi pamoja na mapromota kumwandalia mpambano kwa ajili ya kupima kiwango chake kwa kuwa mapromota wengi wapo Dar es salaam wao wa mikoani wanasahaulika

akizungumza na mwandishi wa habari kwa njia ya simu amesema mabondia wa uzito wake wapo wengi ingawa kila siku wanapangiwa wao kwa wao mana unaweza kukuta bondia mmoja kacheza na mtu mmoja mara nne wakati mabondia...

 

12 months ago

Bongo Movies

Nay wa Mitego Akubali Yaishe Aomba Msamaha

Baada ya kuporomoshewa maneno ya kashfa kwenye mitandao na mzazi mwenzake kwa kushindwa kumtunza mtoto zaidi ya kumuweka tuu kwenye mitandao ya kijamii na kujisifu, Nay wa mitego amekiri kubadilika na kuanza kumuhudumia binti yake.

Nay wa Miteho leo Rapa kupitia ukurasa wake wa Instagram ameamua kuudhihirishia umma kuwa kuanzia sasa atakuwa baba mwema na ataanza kuwahudumia watoto wote kwani yeye ni kama kioo hivyo hana budi kutekeleza hayo.

Nay wa Mitego wiki iliyopita aliandamwa na matusi...

 

3 years ago

Raia Tanzania

Yusuph Mlela: Nikikupikia biriyani…

YUSUPH  Mlela ni msanii maarufu wa  filamu nchini  aliyeweza   kujijengea jina kutokana na kumudu kazi yake kwa kuigiza sehemu  tofauti bila kujali uhusika anaouvaa.

Ni miongoni mwa wasanii wachache ambao  wameweza kutunza heshima yao  tofauti na wasanii wengine wanaotafuta umaarufu kwa kufanya mambo yanayokwenda kinyume na maadili.

Raia Tanzania imezungumza na Mlela  ili kujua mambo mbalimbali ya maisha yake  awapo nje ya sanaa kama ifuatavyo:

Raia Tanzania: Ukimzungumzia mlela...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani