Ziara ya Waziri Mkuu, Serikali kuhakiki mipaka maeneo ya hifadhi

IMGS8652

SERIKALI imewataka wananchi wanaoishi pembezoni mwa vijiji vinavyopakana na maeneo ya hifadhi kutofanya maendelezo yeyote hadi zoezi la kuhakiki wa mipaka ya hifadhi hizo litakapokamilika.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa wilaya ya Kaliua mkoani tabora amesema kwa sasa serikali inaendesha zoezi la uhakiki wa mipaka ya hifadhi na kisha taarifa itakayotolewa itatumika kutoa maamuzi juu ya vijiji vilivyobainika kuwa ndani ya maeneo ya Hifadhi.

Waziri Mkuu ametoa ufafanuzi huo baada ya kuombwa na wabunge wa Kaliua na Ulyanhulu kutoa maelekezo ya serikali juu ya vijiji vilivyopo kwenye maeneo ya hifadhi licha ya kuwa na cheti halali cha kutambuliwa.

Akizungumza na wananchi wa Kaliua , waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka watanzania wenye asili ya Burundi waliopewa uraia waache kujihusisha na matukio ya uhalifu, vinginevyo serikali itaamua vingine.

Share on: WhatsApp

The post Ziara ya Waziri Mkuu, Serikali kuhakiki mipaka maeneo ya hifadhi appeared first on Channel Ten.

Channelten

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Ippmedia

Waziri Mkuu ameziagiza halmashauri kupima maeneo ya taasisi za serikali na kuweka mipaka.

Waziri Mkuu Mh. Kassimu Majaliwa ameziagiza halmashauri kupima maeneo yote ya taasisi za serikali zikiwemo shule na kuweka mipaka kisha kujenga majengo ya ghorofa kwa shule zenye ufinyu wa maeneo na ikibidi kuwahamisha wananchi wanaoishi jirani maeneo ya shule kwa kuwalipa fidia ili kumaliza adha ya msongamano wa watoto madarasani.

Day n Time: Alhamisi Saa 2:00 UsikuStation: ITV

 

1 year ago

Ippmedia

1 year ago

Channelten

Wananchi wa Mbarali walalamikia hifadhi ya taifa Ruaha kuweka mawe ya mipaka kwenye maeneo yao

DSCN2173

WAKAZI wa vijiji vya kata ya Imalilosongwe Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali wamelalamikia hifadhi ya Taifa ya Ruaha, kuweka mawe ya mipaka bila wao kushirikishwa, hivyo kumuomba Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kufikisha kilio chao kwa Rais wakiomba wabaki kwenye maeneo yao.

Wananchi wanatoa ombi hili wakati wa Mkutano kati yao na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Gabriel Makala , ambao umefanyika katika kijiji cha Mwanavala , ukiwa na lengo la kusikiliza mgogoro kati ya wananchi na hifadhi ya taifa ya...

 

2 years ago

Ippmedia

Waziri mkuu auagiza uongozi wa wilaya ya Tanganyika kuwaondoa wananchi waliovamia maeneo ya hifadhi.

Waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi kuhakikisha unawaondoa watu wote wanaoishi katika maeneo ya hifadhi na Ushoroba wa wanyama wa Lyamgoroka.

Day n Time: Jumanne Saa 2:00 Usiku Station: ITV

 

3 years ago

Michuzi

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MITARO NA MAENEO YALIYOATHILIWA NA KIPINDUPINDU JIJINI DAR

Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Mbazi Msuya (wa katika) akieleza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki (wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka (wa kwanza kulia) wakati wa ziara ya kukagua mtaro uliojengwa eneo la Buguruni kwa Mnyamani.Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka (wa kwanza kulia mwenye miwani) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki wakiangalia hali ya...

 

1 year ago

Channelten

Mipaka kwenye hifadhi za Taifa Wananchi wakwamisha zoezi la kuweka mipaka SERENGETI

Juhudi za kukamilisha kwa wakati utekelezaji wa agizo la waziri mkuu ambalo lilielekeza kuwa hifadhi zote za taifa ikiwemo ile ya Serengeti kuainisha mipaka yake yote na kuweka alama zinazo onekana wazi,zinaweza kukwama baada ya wenyeji katika baadhi ya maeneo ya vijiji mipaka hiyo hupita kuanza kuvunja nguzo ambazo zinaendelea kuwekwa kama alama.

Mwishoni mwa mwaka jana ,Akiwa mkoani Dodoma waziri mkuu Kasim Majaliwa alitoa agizo kwa Taasisi zote za kiuhifadhi ikiwemo TANAPA kuhakikisha...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani