Top posts kwenye Facebook

Happy EASTER to you & yours FAM..!! 🙏🏿 😇

Happy EASTER to you & yours FAM..!! 🙏🏿 😇

FidHop

Read more


#NIMEGEUKADARAJA (Sehemu ya 15) #MTUNZI: Gerald Kitalima Tulipoishia ...... Baada ya kama...

#NIMEGEUKADARAJA (Sehemu ya 15) #MTUNZI: Gerald Kitalima Tulipoishia ...... Baada ya kama dakika tatu kupita likasikika tangazo sehemu ile ambayo wanafunzi wamekusanyika wakisubiri kusajiliwa likawa linatajwa jina kamili la Khadja na kuhitajika kufika ofisi ya Dean Of student kabla ya saaa tisa alasiri. Khadja aliposikia lile tangazo wasiwasi wake ulizidi kuongezeka zaidi na zaidi lakini Amba alizidi kumsikitiza kuwa akae kimya na asiende kwenye hiyo ofisi huku akizidi kumsikitiza kuwa kuwa akicheka na nyani atavuna mabua. Khadja kwa sababu ya ugeni na woga na hivi ameshaambiwa yule ni Dean of students hivyo alianza kuwa na wasiwasi kuwa huenda anaweza kumsumbua au kuja kumbana katika baadhi ya vitu, hivyo ilibidi amuombe Amba aendee kwenye ile ofisi mara moja japo akamsikilize. Amba japo kwa shingo upande ilibidi amruhusu aende na kumwambia kuwa awe makini, akizidi kumsisitiza kuwa watu hao si watu wazuri, Khadja alimuakikishia kuwa hilo si tatizo kwake na kusema kuwa atajitahidi, wakati anainuka kwenda ilibidi ajihami aliacha kila kitu chake kwa Amba pale walipokuwa wamekaa hivyo aliinuka yeye mwenyewe na kwenda moja kwa moja kwenye ile ofisi. Alipofika tu yule mwalimu alimwita Khadja kwa majina yake yote matatu, na kumuuliza mbona mpaka muda ule alikuwa hajakamilisha kujisajili ili hali aliambiwa aende sehemu ambayo alimuelekeza, Khadja ilibidi amdanganye kuwa alikwenda na kuona pia kuna foleni na kuamua kwenda kula kwa sababu alikuwa na njaa sana. Baada ya hapo yule mwalimu alimuuliza simu yake ipo? Akamjibu kuwa simu yake ameacha kwenye begi lake kwa yule rafiki yake, mwalimu akamuuliza yule ni rafiki yako au mpenzi wako? Unawezaje kumuamini kiasi hicho na kumuachia vitu vyako ili hali wewe leo ndiyo unaingia chuoni hapa? Khadja alimweleza kuwa yule ni rafiki yake tu wala si mpenzi wake, baada ya hapo yule mwalimu aliingia mfukoni mwake kisha akatoa 'Bussines card' yake na kumpa Khadja kisha akamweleza kuwa baadaye majira ya saa kumi na mbili amshtue kwa kumtumia ujumbe mfupi. Mwalimu akarudi tena kusisitiza kuwa amtumie ujumbe mfupi tu asipige simu, yeye atajua ni yeye na kumpigia, Khadja akamwambia haina tatizo atajitahidi kufanya hivyo, baada ya hapo yule mwalimu alisimama na kuanza kutoka huku akimwambia Khadja amfuate ofisi nyingine. Kwa wanafunzi ambao walitangulia chuoni pale ambao tayari wanamjua yule mwalimu walianza kuonyeshana vidole wakijua wazi kuwa yule mwalimu anataka kutoka kimapenzi na yule binti, muda huo Amba amenuna kweli kweli kwa sababu watu wote waliona amekuja na yule binti pale lakini kitendo cha yule mwalimu kuwa karibu naye yeye ni kama anajichoresha huku watu wakimtolea mimacho. Walipoingia kwenye chumba cha usajili yule mwalimu aliwatambulisha walimu wenzake na wafanyakazi wenzake kuwa yule ni mdogo wake hivyo anaomba waweze kumsaidia kumuandikisha haraka ili arudi nyumbani, lakini sura za wale wafanyakazi wote zilikuwa zimejawa na tabasamu wengine wakicheka kabisaa sababu wanajua kuwa yule si mdogo wake lakini wanatambua kuwa huenda anafukuzia anataka kutoka naye kimapenzi, na hivi ukizingatia binti ameumbwa na kuumbika. Alipowatambulisha na kuondoka Khadja aliona na kugundua wazi kama kuna lugha za ishara zilikuwa zinaendelea pale, hivyo kitendo kile kilimfanya akose amani na kujiona kama amefanya makosa makubwa, kukubaliana na kile kitendo lakini alikuwa hana jinsi kwakuwa tayari kimeshatokea. Wakati anatoka baada ya kusajiliwa kuna dada mmoja alikuwa mstaarabu hivi na mtu fulani wa kujielewa alikuwa kwenye mstari kwa muda mrefu sana akisubiri kuingia ndani kujisajili, hivyo alimwita Khadja na kwenda naye pembeni kidogo kisha akaanza kumpa wosia kuwa anapaswa kuwa makini na yule mwalimu na kumwambia kuwa asipokuwa makini atamaliza chuo huku akiwa na maradhi na kama si hivyo basi hataweza kumaliza masomo yake pale, hivyo alimwambia kuwa anapaswa kukaa naye mbali na asiruhusu mazoea naye hata kidogo. Khadja alipopewa ule wosia alikumbuka nyuma, kipindi hicho ameanza mahusiano tu na Issah kuwa mama mmoja ambaye alikuwa anauza mbogamboga aliwahi kumpa wosia, akimtaka aache mazoea na wale vijana wa butcher na kukazana na shule lakini hakumsikiliza na baadaye alikuja kujutia kupotezea ule ushauri wa yule mama. Hivyo baada ya hapo Khadja alimshukuru sana yule dada kwa ushauri wake na kusema ataufanyia kazi, yule dada alikwenda mbali zaidi akamwambia kuwa anapaswa kujitunza sana pale kwani wanafunzi wa aina yake wengi walikutana na majaribu walioshindwa saizi wanajutia maamuzi yao na kudai wengine walishindwa na chuo kabisa. Baada ya hapo Khadja alikwenda moja kwa moja kwa Amba, alipofika tu kitu cha kwanza kilikuwa kumuomba msamaha Amba kwa yote yaliyotokea na kumweleza kuwa halikuwa kusudio lake, hivyo amsamehe baada ya hapo alimweleza yote yaliyotokea na vile ambavyo yule dada ameshauri. Amba : Siku zote watu wanapokwambia kitu huwa kuna mambo makuu mawili, inawezekana hicho kitu kinaukweli au ni uzushi hivyo lazima ufanyie kazi yale unayoambiwa ili kujiweka katika sehemu salama kabisaa, hivyo kama watu wanakwambia hivyo ujue wanakupenda na kukuonea huruma hawataki uharibikiwe. Hapa Chuo watu wameshalalamika sana juu ya huyu mwalimu, watu wengi wamepoteza ndoto zao kwa ajili yake lakini uongozi wa chuo nao unafunga huu ugonjwa, kwani hakuna hatua zozote zile ambazo anachukuliwa wala hakuna linalofanyika, hivyo shukuru wewe una watu ambao wanakueleza hili, sasa wengine hao ambao hawajui lolote lile si ndiyo wanaumia huko. Khadja : Ni kweli usemalo Amba, mimi nimekuelewa Baada ya hapo Amba alichukua ile Bussiness card na kuichana chana pale, baada ya hapo wakasimama na kuanza safari sasa kurudi nyumbani, Khadja ilibidi amuulize Amba kama kutakuwa na njia nyingine ya kupita wapite ili wasirudi tena njia ile ambapo kuna ofisi ya mwalimu huyo, Amba anamweleza kuwa ni bora wapite nyuma ambako kuna parking za magari ya watu ili waweze kutokezea sehemu ya chakula wale kabisaa na kuondoka zao nyumbani. Kumbe wakati huo yule mwalimu alikuwa ametoka ofisini kwake na yeye alikuwa huko huko sehemu ya parking ya magari kuna binti alikuwa amemwelekeza aende huko hivyo alikuwa anaongea naye, hivyo yule mwalimu alipowaona alikuwa hana namna ilibidi akae kimya na aendelee na maongezi na yule binti mwingine, walipopita usawa wake Amba akamweleza Khadja kuwa unaona haya ndiyo mammbo huyu mwalimu anashindia hapa chuo, kazi za watu hafanyi kwa wakati yeye kazi kuhangaika na wanawake tu kila siku. Namuonea huruma yule binti wa watu kama hamjui sasa ndiyo anapotea hivyo, Khadja na yeye somo ndiyo likawa linazidi kumkolea vizuri, baada ya hapo wakaingia zao kula mpaka wanamaliza kula yule mwalimu bado alikuwa anaongea na yule binti, baada ya hapo walipomaliza wakawa wanaondoka kumbe yule mwalimu amewaona hivyo aliwaacha kwanza wafike mbali kidogo. Akawasha gari yake aina ya Brevis rangi nyeusi, kisha akawa kama anaondoka maeneo ya chuo akiwa mwendo wa taratibu kabisaa baada ya umbali kidogo aliwaona kina Khadja, wakati anazidi kuwasogelea alishusha kioo cha gari na kupunguza sauti ya muziki kwennye gari uliokuwa unakita kwa base kubwa japo haukuwa na sauti kubwa sana, alipunguza japo kuweza kupata usikivu vizuri. Alipowakaribia kabisa alisikika akamwita Khadja Mwalimu : Twendeni niwapeleke (Khadja akamtazama Amba kuona anatoa ishara gani lakini Amba hakutaka hata kumuangalia akawa anazidi kusonga mbele) Khadja : Tunashukuru mwalimu kwani tayari tumeshafika Mwalimu: Kama yeye haendi basi twende nikupeleke wewe. Khadja : Ahsante mwalimu, siwezi kumuacha tumekuja pamoja shaka ondoa sisi tumefika. Mwalimu: Basi sawa, ila usisahau kunicheki kwa ile ishu sawa eehhh Khadja? Khadja aliitikia na kumuahidi kumcheki, yule mwalimu alipandisha vioo vya gari yake na kuanza kuondoka zake, Amba alipomfikisha Khadja sehemu ambayo amefikia tu na baadaye kuondoka, kila Khadja alipojitahidi kutuma ujumbe mfupi haukujibiwa, kila alipojitahidi kupiga simu haikupokelewa, ilipofika usiku Khadja hakuwa na namna huku akiwa na mawazo akijua wazi kabisaa huenda Amba amechukizwa na kitendo ambacho kimetokea. Baadaye ilibidi ajipe moyo kuwa huenda akikaa sawa anaweza kumtafuta, hivyo usiku yeye alitoka na kwenda kutafuta chakula, alipouliza kwa wenyeji pale walimuelekeza sehemu nyingine ambayo ni tofauti ni ile aliyokwenda na Amba jana usiku, alipofika hapo aliona unaweza kula chakula hapo hapo hivyo aliagiza chakula chake pale, wakati anakisubiri akawa anaongea na simu na ndugu zake mjini. Muda haukupita mrefu ghafla na yule mwalimu alikuja sehemu ile ile kula na kujikuta wamekutana pasipokutarajia na muda huo Khadja alikuwa bado hajampigia hiyo simu, hiyo sehemu mara nyingi wanafunzi huwa wanapenda sana kwenda kula hivyo watu ambao walimuona yule binti na Amba walipoona amekaa meza moja na yule mwalimu ilibidi wapate ushahidi wa picha ili kumsaidia rafiki yao. Basi wakawapiga picha bila wao kujua kisha baada ya hapo walimtumia Amba zile picha kama ushahidi...................... Je, nini kiliendelea baada ya hapo? Usikose kufuatilia muendelezo wa simulizi kesho hapa hapa. SHARE WATU WAJIFUNZE KUPITIA SIMULIZI HII na toa maoni yako pia.

 

Full Time: Copco 0-6 Azam FC Enock (8', 19', 40'), Yusuph 13', Zayd 36', Wazir 88'

Full Time: Copco 0-6 Azam FC Enock (8', 19', 40'), Yusuph 13', Zayd 36', Wazir 88'

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani